Nawashukuru wana JF: Siku ya harusi yangu

Nawashukuru wana JF: Siku ya harusi yangu

Hongereni, kama mlimshirikisha Mungu ndoa yenu itadumu mpaka mtaiona miaka 70 mkiwa na furaha na amani, kikubwa ni uaminifu na upendo wa kweli. Kuna wachumba wanaokaa maisha ya uchumba kwa muda mrefu lakini wakishaoana tu wanaanza mafarakano na pengine kuvunja ndoa. Na wapo wanaodumu uchumba kwa muda mfupi sana lakini wanakuja kuishi maisha ya amani na upendo. Kikubwa cha kuzingatia ni Uaminifu na upendo wa kweli, mjueni na kumfuata Mungu. Kitu cha kuepuka ni Ubinafsi katika ndoa unaosababisha kila mtu kutaka chake ni chake badala ya kujua chake ni cha wote, urafiki mbaya na kila chukizo linaloweza kuhatarisha ndoa yenu. God bless you! God be with you! BE THOU FAITHFULL UNTO DEATH!
 
Vipimo bado vipo maabara. Subiri baada ya wiki mbili
Sasa kumbe hata majibu ya vipimo huna, umethibitisha vipi sasa kuwa ninaumwa? Nyie ndio mnaopasua watu miguu badala ya vichwa.
 
Hongera mdada
Mungu awatangulie tunasubiri kadi ya pilau
 
Habari zenu wanajamvi,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wanaJF wote, zaidi sana wale walijitokeza nilipotoa tangazo la kutafuta Mr. Right.

Napenda kuwataarifu kuwa tumeendelea na mikakati na taratibu za harusi na my Mr. Right ambaye nilimpata kupitia tangazo langu la mwezi Jan.2016,
binasi sikutarajia kama mambo yatakwenda kwa speed kubwa namna hii lakini ndivyo ilivyokuwa.

Taratibu zote zimekamilika na Jana tu ndo mahari yote imelipwa, kweli nina furaha na amani sana kwa hatua niliyofikia, namshukuru mchumba wangu kwa seriousness alionionesha.

Wandugu tarehe ya harusi imepangwa na Jumapili ya tarehe 6 march 2016 tangazo la kwanza la harusi yangu litatangazwa.

Tarehe ya harusi imeshapangwa na vikao vinaanza kesho, naomba tarehe nisiiweke wazi kwanza, nitaiweka wazi siku tatu kabla ya harusi. Asanteni
sana.

Wewe ambaye umetupia tangazo lako amini tu utampata unae mtaka.Usichoke wala kukata tamaa.
hongera sana bestito ila naomba tenda ya kukutengenezea kadi za mwaliko za harusi, kutenegeneza keki na kupamba mkuu kimojawapo kati ya hizo bestito usinisahau katika ufalme huu umpya ulioupata humu Mungu amekutendea hongera sana
 
Back
Top Bottom