Nawashukuru ICC-Mahakama ya Kimataifa kwa kunijibu na kunipa mwongozo wa kumshitaki Rais kuvunja Katiba ya Nchi

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
ICC WAPO KIKAZI KWELI.

Asante Sana Mahakama ya Kimataifa-ICC kwa mwongozo mlionipa baada ya kuwatumia malalamiko yangu juu ya Rais kuvunja KATIBA na Mateso niliyoyapata gerezani. Nafanyia marekebisho nakuwarejeshea Tena.@Don Nalimison.

Screenshot_20201215-163501.png
Screenshot_20201215-163524.png
 
Don Damilison juzi tu hapa ulitaka kuanzisha maandamano Nchi nzima kupinga Katiba na Rais aliyeapishwa 2020, sasa unasema umetoka ICC. unasema jana ulikuwa umefungwa, akapata mateso.

sasa Katiba na kuachiliwa kifungoni mbona unataka kurudi tena na kuturudisha member wa JF? Ungeelezea ni kipi kinachokusibu tukakuonesha Jukwaa au mahali muafaka ukapeleka malalamiko yako, mm huku ni kunipambanisha na TCRA nikakosa hata mahali pa kupata yanayotokea duniani kuna mitandao na magazeti hayajafunguliwa p/se
 
Deo mateso gani uliyopata huko gereza la kilimo Kitengule wakati wewe ni msukuma uliyekulia kwenye jembe

Au ulilazimishwa kuwa mke wa pili wa nyampara maana mpaka ufike ICC yatakuwa ni mateso makali kwelikweli
 
ICC WAPO KIKAZI KWELI.

Asante Sana Mahakama ya Kimataifa-ICC kwa mwongozo mlionipa baada ya kuwatumia malalamiko yangu juu ya Rais kuvunja KATIBA na Mateso niliyoyapata gerezani. Nafanyia marekebisho nakuwarejeshea Tena.@Don Nalimison.
View attachment 1650762View attachment 1650763

Ni hatua nzuri kwamba wamekujibu na kukupa mwongozo. Pata ushauri wa ziada wa wanasheria tofauti kupitia evidence ulizonazo kama zinakidhi vigezo vya ICC ndio uchukue hatua za ziada. Hapa Jukwaani utapewa kila aina ya matusi na kupachikwa kila aina ya majina mabaya, ila usife moyo. Hata Mtikila alipokuwa anafungua zile kesi zake za mgombea binafsi nk alitukanwa sana ila mwisho wake kila mmoja anaujua. Keep moving Don Nalimison
 
Kwa kifupi jamaa wamekujibu kwa lugha ya kistaarabu acha kupoteza muda wao; awaangaiki na matatizo ya mtu mmoja mmoja.
 
Don Damilison juzi tu hapa ulitaka kuanzisha maandamano Nchi nzima kupinga Katiba na Rais aliyeapishwa 2020...
Tatizo uelewa wako upo chini sana, habari hapa ni jinsi ICC walivyo makini kwenye utendaji wao.

Tayari washatoa muongozo kwa mhusika jinsi ya kufanya ili waweze kutimiza ndoto za mlalamikaji.
 
Deo mateso gani uliyopata huko gereza la kilimo Kitengule wakati wewe ni msukuma uliyekulia kwenye jembe

Au ulilazimishwa kuwa mke wa pili wa nyampara maana mpaka ufike ICC yatakuwa ni mateso makali kwelikweli
Tulieni muende mkatundikwe huko kwa pilato
 
Mwanzo Mzuri Don, aanzia hapo pa crime of aggression. Fuata miongozo yao. watu wanakuita kichaa , siku ukitoboa ndio watakuwa marafiki zako.. ubarikiwe kwa kuongoza njia ingawaje unaitw majina ya kila namna bila kukata tamaa...kudos
Mkuu tatizo la watanzania ni kuwa na maneno mengi ya kizandiki tu,huyu jamaa inabidi kupongezwa hata kwa huo udhubutu tu na kupata bahati ya kujibiwa
 
Ni hatua nzuri kwamba wamekujibu na kukupa mwongozo. Pata ushauri wa ziada wa wanasheria tofauti kupitia evidence ulizonazo kama zinakidhi vigezo vya ICC ndio uchukue hatua za ziada. Hapa Jukwaani utapewa kila aina ya matusi na kupachikwa kila aina ya majina mabaya, ila usife moyo. Hata Mtikila alipokuwa anafungua zile kesi zake za mgombea binafsi nk alitukanwa sana ila mwisho wake kila mmoja anaujua. Keep moving Don Nalimison
Ushauri mzuri sana usiyo wa kinafiki
 
Mkuu achana na masuala ya watawala.

Vinginevyo Kitengule haipo mbali kwa mara nyingine.

Na wakati huu utakua mwenye bahati sana kurudi salama.

Jikite kwenye mambo mengine kando na serikali

Hata hivyo, ukitaka kuendelea na hizi harakati, tumia angalau ID fake
 
IQ yako ipo ICU
Ndugu unapoenda duka la jumla, ukataka kununua bidhaa moja; muuzaji anapokwambia tunauza bidhaa kuanzia dozens, kilos etc.

Baada ya maelezo yake akakupa na price lists na namna ya kutoa order zako sio kukurupuka tu siku nyingine na kuwaibukia. Ina maana amekujibu kistaarabu ujinga wako.

Ila kuna watu ujinga unakuwa umewazidi mpaka wanashindwa kutafsiri majibu simple tu, wanayopewa. Wao washazoea kujibiwa ovyo ovyo muda wote ndio waelewe.
 
ICC WAPO KIKAZI KWELI.

Asante Sana Mahakama ya Kimataifa-ICC kwa mwongozo mlionipa baada ya kuwatumia malalamiko yangu juu ya Rais kuvunja KATIBA na Mateso niliyoyapata gerezani. Nafanyia marekebisho nakuwarejeshea Tena.@Don Nalimison.
View attachment 1650762View attachment 1650763
Mkuu,

Ninahisi kilichoandikwa kwenye mrejesho huo hujakielewa kwenye tafsiri ya kisheria na wewe ukakimbilia kutupia kwenye mitandao kwa furaha.

Kiufupi wamekulengesha kwenye tundu la maangamizi kama mtu alieamua kufanya safari ya kuelekea kwenye jua hawezi kurejea kamwe.

Tambua haya

1. Mamlaka ya mahakama ya ICC
2. Mamlaka ya nchi
3. Mtu anayelalamikiwa anatoka kwenye nchi iliyoridhia mamlaka ya mahakama ya ICC ndani ya nchi yake?
4. Mtu anayelalamika anatoka katika nchi mlalamikiwa na nchi hiyo imeridhia mamlaka ya mahakama ya ICC?
5. Aina ya kosa ama hali ya usalama wa mtu au watu, jamiii husika imetolewa taarifa na Katibu mkuu wa UN
6. Kiiwango na athari cha kosa kwenye jamii na ni kinyume cha sheria za nchi husika na za kimataifa
7. Kwamba hakuna uchunguzi wowote unaoendelea kuhusiana na malalamiko ya mlalamikaji ama hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na mwendesha mashitaka wa nchi husika pamoja na kuwa na taarifa ya kutendwa kosa hilo

Kama unafikiri umefaulu kumubagaza Mh Rais na taasisi zake umekula la chuya bila kulazimishwa au kulaghaiwa na mtu kwa kuwa KESI inarudi kwako na hutajinasua kwa vyovyote kwa kulingana na aina ya makosa unayotenda kila siku dhidi ya Jamhuri.
 
Back
Top Bottom