Nauza contacts za watu na majina yao

Nauza contacts za watu na majina yao

kwelakenya

Member
Joined
Jan 21, 2010
Posts
59
Reaction score
6
Wadau, kuna promotion/sampling ya kampuni moja tulifanya na tukakusanya majina pamoja na namba zao za simu.Kwa yule anaehitaji nimuuzie tuwasiliane.Ni contacts kama 3,000 za watu wa Dar.
 
Wadau, kuna promotion/sampling ya kampuni moja tulifanya na tukakusanya majina pamoja na namba zao za simu.Kwa yule anaehitaji nimuuzie tuwasiliane.Ni contacts kama 3,000 za watu wa Dar.

Fafanua kidogo, nikishanunua mimi nafanyia nini?
 
unauza kiasi gani?

Nina hakika gani kama hizo number za simu bado wanatumia?

Je ulikusanya sample ya watu wa aina gani?
 
Wadau, kuna promotion/sampling ya kampuni moja tulifanya na tukakusanya majina pamoja na namba zao za simu.Kwa yule anaehitaji nimuuzie tuwasiliane.Ni contacts kama 3,000 za watu wa Dar.

vague.
hawa wadau unaotaka kutuuzia namba zao wanajihusisha na nini?
 
Kwa hiyo wewe ni mwizi, unaiibia hiyo kampuni kinyume na utaratibu wao.
 
Ndo maana wakati flani watu huwa hawatoi ushirikiano kwenye studies mbalimbali kwa sababu ya watu wa namna yako, yaani contacts na jina la mtu unalifanyia biashara pasipo ridhaa yake
 
du, hii dunia kuna biashara, sasa mleta maada, hizo contact mtu ananunua ili afanyie nini hasa? Je afanyie biashara? au za kutongozea means atafute zenye majina ya ke/me aanze kupiga sound, make hivi hivi inakua ngumu
 
Labda anamaanisha kuwa kwa wale wanaohitaji contacts kwaajili ya kazi!!
 
Msimshangae na kuuliza huwa ni za nini! Huwa ni kwa ajili ya database ambayo kwa kampuni zinazojishughulisha na SMS marketing wanahitaji sana hizo number ndo msingi wenyewe wa hiyo biashara...kumbukeni kipindi cha kampeni mlikuwa mnatumiwa message za ajabu ajabu ndo mtindo wa kukusanya number zetu uliotumika,
 
Njaa mbaya wajameni...what the hell is this?
 
Aisee...At this information age you still thinking you can make such easy money. By the way clean people do not hide their profile and hence their information. Hizo unazotaka kuuza labda ni za watu wanaotafutwa na polisi.
Isaidie nchi yako ... peleka tu hizo information polisi.
 
Dunia haiishi vituko.
Jamaa kakaanga mbuyu kawaachia wenye meno watafune!
 
Kwa nini mtu asitumie telephone directory na anunue kwako?
 
Ha..ha..ha Kweli wabongo tunaelekea pazuri.Tatizo lako sasa ni kwenye kuzifanyia pricing hizo contacts,najua utakosea tu.
Give me a cut & i'll put a price tag to those numbers.
 
Back
Top Bottom