Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,650
- 16,731
OkkTukiwa bado tunatafakari mabadiliko ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya tano, hali inaonekana sio shwali ndani ya chama hicho.
Nasema hali sio shwari, kwani kila mtu amekuwa na hofu kubwa, hasa wale wadadisi ndani ya chama. Inavyoonekana kwamba sasa hivi JPM ameamua kuwafunga midomo CCM na yeyote atakayeibuka kusema kitu ambacho ni tofauti na fikra za mwenyekiti wa chama na Musiba et al, basi akumbuke kwamba, nafasi yake ndani ya chama itakuwa ni finyu sana.
Serikali zote, tangu ile ya kwanza, zimekuwa zikiwaona vijana kuwa ndio hazina ya chama na wamekuwa wakisaidia kuongeza ushawishi kwa vijana wenzao ambao hawako karibu na chama. Hatua hii imesababisha kujenga chama kwa kutumia imani ya vijana ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura wote Tanzania.
- Kuwavuruga vijana
Ndio maana, leo utaowaona akina George Kahama, Malechela, Mkuchika, Lukuvi ambao miaka ya 80 walikuwa vijana wakiendelea kuhudumu serikalini toka serikali moja kwenda nyingine na wamekuwa wakiheshimiwa hadi hivi leo.
Leo hii kuwavuruga Nape, Mwigulu, Makamba nk, ambao ni miongoni mwa vijana wenye ushawishi CCM, sio kitu kizuri na kinaweza kuharibu afya ya chama.
Tangu serikali ya tano ianze kutawala, wazee wamekuwa hawana chao. Hawana ushawishi tena na kila wakijaribu kusema kitu, basi wanaambiwa wanawashwa washwa. Tumeona baadhi wakipewa onyo na mwenyekiti kuwa wakae kimya. Huu sio ustaarabu kabisa ndani ya chama kwani historia inawanyonya awamu ya tano.
- Kuwavuruga wazee
Hivi majuzi, tumeona bwana anayejiita Musiba akiendelea kuwadharirisha wazee wa chama kwa kuwakashifu hali iliyosababisha wazee hao kutoka hadharani na tamko ambalo limesababisha mjadala mkubwa miongoni mwa watanzania.
Ikumbukwe kwamba, mwaka 2015 kwenye sakata la kura za maoni CCM, hakuna aliyejua kwamba JPM atapenya kwani mchuano ulikuwa mkali sana. Bila wazee wa CCM, basi JPM asingepenya hata nafasi tano..leo hii huenda Membe, Makamba, ama wale akina mama wa Zanzibar ana Lowasa, mmoja wao angekuwa rais.
- Kuwavuruga watanzania
Maisha ya watanzania yamebadilika sana tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani. Njia kuu za uchumi zimeharibiwa na fedha zote zimeenda kwenye mikondo ya serikali, ambayo kwa mbwembwe zinaishia kununua ndege, madaraja nk, vitu ambavyo havijengi kabisa social capital. Tujifunze kwa Nigeria.. imeendelea sana lakini gap la maskini na tajiri ni kubwa sana hali inayosababisha wanigeria wengi kukosa imani na nchi yao na wengine kukimbia nchi.
Kuna ukabila sana serikali hii ya awamu ya tano. Ukiangalia safu za wakubwa, wengi wao wanatoka kanda ya ziwa, na wengi ni watu wa karibu sana na Rais ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa ni dhaifu katika kushughulikia maslahi ya watanzania na wamebaki kuimba mapambio kwa JPM.. kusifia kusiko na mwisho.
- Kuleta ukabila
Kwa sababu hizi nne, ninaona muelekeo wa CCM sasa huenda ukawa mbaya kwani CCM wanajulikana jinsi wanavyozika vichwa vyao ardhini na pale wanapokugeuka hutaamini kwamba ndio wao
Marijani Kyomo
Maruku, Kagera
Ndugu anza kwanza kurekebisha 'r' na 'l' kwenye hizi hisia zako...Tukiwa bado tunatafakari mabadiliko ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya tano, hali inaonekana sio shwali ndani ya chama hicho.

Na hao wote wanaojifanya watabiri ama kuibua utabiri wao uchwara kipindi hiki cha ccm kujivua gamba, ni haohao wachumia tumbo ama marafiki zao wanufaika.Kipindi hiki tutapata wapiga ramli wengi kweli.
Hii ni theory tu. Ukweli ni kwamba ccm changa iko kwenye wakati mgumu.Kampeni za 2020 kwa asilimia kubwa zilifanywa na Mh Rais Samia.
2015 CCM ilisaka kura za kina mama kupitia Samia na ilizipata.
Magufuli na Samia wanetekeleza ilani ya CCM kwa kiwango cha hali ya juu.
ni uzuzu kufikiri CCM inaweza kuanguka 2025.
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini Sana siasa za Tanzania. Naweza nikasema tangu mwaka 2000.
Tangu wakati huo CCM haijawahi fiwa na mwenyekiti wake . Na hata taifa halijawahi kupoteza Rais.
Mwaka 1995 nikiwa bado Niko shule lakini historia inaonesha kulikuwa na mnyukano mkubwa Sana ndani Cha Chama kwenye uchaguzi wa Urais. Mkapa na Kikwete walichuana vilivyo.
Mwaka 2005 mchuano ulikuwepo lakini haukuwa mkubwa Sana.
Mwaka 2015 mchuano ulikuwa mkubwa mno na Makundi yalikuwa na nguvu Sana kitu ambacho kiliwafanya Wagombea kutembeza rushwa nje nje.
Mwaka huu Hayati JPM aliibuka kidedea kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni vita kati ya Lowasa na Membe. Lakini wengine wanaamini ulikuwa ni mpango wa Mungu JPM kuongoza hili taifa.
2015 ndio mwaka ambao upinzani ulikuwa na nguvu Sana na huo mwaka CCM walimtumia hayati JPM kama daraja la kushinda uchaguzi.
"Mabango karibu yote yalikuwa *Chagua Magufuli mchapakazi, makali, mfuatiliaji, n.k". Hii yote ilikuwa ni kujibu mapungufu aliyokuwa nayo Kikwete kama vile ufisadi, dhaifu na mpenda safari Mara kwa mara.
Magufuli alipoingia madarakani alifanya kazi yake kadili ya uwezo wake wote.
Bahati mbaya ameondoka kabla ya 2025. Na hiyo 2025 iko karibu Sana. Wakati huu wananchi wengi wanataka utawala wa radha nyingine tofauti na ya hayati JPM. Hii Ndio kawaida ya watu kutaka kubadili radha ya mtawala kwa maana hakuna mkamilifu.
Hapa ndipo hoja yangu ilipo
Samia ameingia wakati ngumu Sana.
Kwanza, kumalizia Kazi alizo ziacha JPM.
Pili, kuwatuliza watu waliokuwa kwenye mbinyo wa JPM ili nao wapumue .
Tatu, kujitengenezea njia ilu 2025 apate turufu ya kugombea tena.
Nne, kuepuka mitego ya watu wanataka madaraka maana JPM alikuwa ameshawajua na hivyo walikuwa hawampi shida.
Tano kusimamia ustawi wa nchi. Ikiwemo usalama, uchumi, na huduma kwa jamii n.k.
Sita, kuendelea kuwafuta machozi na kuwa fariji walio kuwa Wana mpenda Hayati JPM. Ikiwemo familia yake, wateule wake, watu wa kanda ya Ziwa hususani wasukuma. Bila kuonesha chuki ama toka kwake Moja kwa Moja ama kwa wateule wake ama wafuasi wake.
Haya yote yanamkuta mda ambao alikuwa hajajianda
Samia akishindwa kufanya hayo yote ni wazi kwamba atapoteza kiti mapema Sana lambda akichuke kwa nguvu. Na huo Ndio mwanzo wa kifo Cha CCM.
Hadi Sasa utasikia mengi Sana hasa toka kwa waliokuwa na chuki na JPM walimsifia Sana Samia ili tu kuwabagaza waliokuwa wateule na wapenzi wa Hayati JPM. Hii ni hatari kwa usitawi wa Chama. Hii ni hatari maana hadi Sasa hakuna jambo ambalo unaweza sema Samia amewafanyia hao wapinzaniwa Hayati JPM.
Samia anakazi kubwa tumuombee. Maana wanao msifia wengi sio wanachama wa CCM lakini lengo lao ni kuwaweka njia panda Wana CCM waliojengwa na Hayati JPM . Mwaka 2025 ndipo utawaona Hawa waliokatishwa Tamaa ndani ya CCM wakikimbilia upinzani.
Samia chama kiko mikononi kwako. Kife ama kipone.
Pole kwa Msiba Mzito Rais Samia.
Hongera kwa kuwa Rais wetu
CCM haiwezi kutolewa na chama pinzani, kuna factors mbili kubwa zinaweza kuitoa ccm na ikawa mwisho wake, 1) mpasuko ndan ya chama atleast iwe zaidi ya 2015 (sasa shida ya hapa wapinzani mpaka leo hakuna chma cha kurusha kadi kwao incase ccm itapasuka maaana ikipasuka lazima upinzani wachezewe ndumba alafu wajimalize wenyewe)
2) hii ndo kubwa na ya uhakika, wananchi wenyewe waamue kufanya vurugu hapa ccm itatoka ila kwa coverage ccm ilionayo na imani iliorudisha kwa wnanachi hmm miaka 60 tena