Naumia kumuona mtoto wangu

Naumia kumuona mtoto wangu

Jamani, ninawashukuru kwa ushauri wenu. Nawaombea mlionitukana pia. Mimi ni binadamu na kuna kuteleza. Ila ninawashukuru sana watu wote mliotoa ushauri kwamba niachane na kudai mtoto. Asanteni sana na hakika mimi na mke wangu tunafurahia kulea watoto tuliobarikiwa na Mungu. Asanteni.
Kati ya watoto wako watatu ...wawili umetombewa....subir,baba zao waje kudai watoto wao
 
Naona katosa kujibu hilo swali.....

Nadhani swala linalohusu toba wengi hawalielewi. It means mtu unaweka uwazi mbele ya mtu yeyote uliemkosea akiwemo na mke wangu. Sasa katika kujibu swali lako, ndio mke wangu anajua na alinisamehe. Hata hizi jitihada ninazotaka nizifanye anajua maana nimemshirikisha.
 
Dah!? haya sasa,..... Mentor vipi, huna risasi ya ziada?

Ah nishashauriwa kutumia bomu!

Nadhani swala linalohusu toba wengi hawalielewi. It means mtu unaweka uwazi mbele ya mtu yeyote uliemkosea akiwemo na mke wangu. Sasa katika kujibu swali lako, ndio mke wangu anajua na alinisamehe. Hata hizi jitihada ninazotaka nizifanye anajua maana nimemshirikisha.

Good, step two: kapime wanao DNA kwanza.
 
Mpaka sasa hujaokoka kwa kuwa kuna dhambi umeificha, usijiite mlokole kabisa kama unataka kuwa mlokole SEMA HAYA MBELE YA WAHUSIKA NA KWELI ITAKUWEKA HURU. Haya yanayokuumiza ni dhambi na yule motto bila kujua ukweli yupi baba yake ni adhabu tosha kwako. Jiweke huru kama bado unataka kuwa mpendwa la acha hilo jina ni unafiki mbele za Mungu.
 
Ndo maana nataka niweke kila kitu wazi, hapa hujaamini kwamba nimeokoka? Mbona nimemweleza hata mke wangu na kumuomba msamaha? Hata yeye ameniunga mkono kwamba anataka akae na mtoto amlee.
 
Mkuu, mi nakuunga mkono. Japo ya kale yamepita, ila huko nyuma kuna mtoto wako. Kwa mtu yeyote mwelewa, atakusamehe tu. Kwanza, kama jamaa anasali, uende kwa Mchungaji wake ukapate ushauri, usiende mahakamani maana hapo kesi yenu itakuzwa na magazeti ya udaku. Nenda kapate ushauri kwa mchangaji wako, pia na kanisa anakosali huyo bwana. Wachungaji watamweleza kwanza kabla ya yeye kukubali kuonana na wewe. Pia sikiliza ushauri wa huyo mwanamke anaokupa na kama anakubali basi endelea na jitihada hizo.
 
Nadhani swala linalohusu toba wengi hawalielewi. It means mtu unaweka uwazi mbele ya mtu yeyote uliemkosea akiwemo na mke wangu. Sasa katika kujibu swali lako, ndio mke wangu anajua na alinisamehe. Hata hizi jitihada ninazotaka nizifanye anajua maana nimemshirikisha.

Okay ni vema, ila ndo unaenda kumvunjia huyo mwanamke ndoa yake.....
 
Ngumu kumesa hii kitu
Kabla hujafanya uamuzi wa kwenda kudai mtoto, kaa chini utafakari madhara yatakayojitokeza baada ya wewe kutoa hiyo siri ya mtoto
 
Ubaya wenu ni mlifanya kwa kupanga kabisa! Haikutokea bahati mbaya. Natumaini wakati mnapanga ulijua kabisa mtoto atabaki kwa mama yake (atatunzwa na mume mwenzio). Iweje leo utake kumdai? Huoni ni kukiuka mipango yenu? Usidhani kwa kufanya hivyo ni huyo mchepuko wako tu ndo ataathirika, hakika hata wewe na familia yako hutobaki salama. Maumivu utayompa huyo mume mwenzio hatawaacha salama. Kaa kimya tulia, meza maumivu ya kumuona mwanao anamuita mwenzio baba maana ndo malipo ya kosa mlilolifanya tena kwa kudhamiria.
 
Unahakika gani kama watoto unaowalea ni wako?

Ila nyie ndo mnasababisha lara 1 aseme ndoa ni taasisi iliyojaa unafiki kuliko zote duniani.

Sijui nikutukane tusi gani aisee ili uumie! Hata konokono hawezi fikiri u.jinga kama huu ulofanya
 
Ndugu zanguni wana JF, natumaini nyote ni wazima wa afya!

Juzi, nilikua na maongezi ya muda mrefu na mfanyakazi mwenzangu. Katika maongezi, nikagundua kwamba yeye, kama nilivyo mimi, anaumia sana. Aliponieleza shida yake, nilimwambia wazi kwamba nami nateseka na mawazo kama wewe. Hivyo nikashindwa kumpa ushauri maana tatizo lake linafanana na langu. Mawazo yenu yatasaidia nijue la kufanya, na yeye akiyasoma atapata uamuzi afanye nini.

Mimi, kabla sijaokoka nilikua na mahusiano na mke wa mtu. Nilibahatika kuzaa nae mtoto wa kike. Mme wake yupo ila huyu mwanamke tulipendana sana ila hatukubahatika kuoana. Alipoolewa, na hata mimi baada ya kuoa, mahusiano yetu yaliendelea tena vibaya sana. Mwaka juzi mwanzoni tulishauriana tuache maana tulikua tunatenda dhambi ila tuliamua kuwa na mtoto awe ukumbusho wetu. Na kweli tukabahatika kumpata mtoto huyu wa kike.

Kwa huyu bwana, kama ilivyo kwangu, huyu nimtoto wa kike pekee. Ninao watoto wakiume 3. Yeye anao watoto wa kiume wawili na alivyoona huyu amwezaliwa, alimweleza mke wake kwamba wanatosha. Anampenda sana mtoto huyu wa kike.

Sasa mi naumia sana. Siku moja nikiwa na mke na watoto wangu supermarket mmoja ya hapa, niliwaona wao pia wakiwa katika heka heka ya shopping wakiwa na mtoto wangu. Niliumia sana. Sasa nataka nifanye harakati nimchukue mtoto wangu. Nifanyeje jamani nisaidie.

Mfanyakazi mwenzangu yeye alimpa binti wakati anasoma na bila kujua, binti alikua mchumba wa mtu. Alipoolewa aliolewa na ujauzito wa jamaa. Yeye alipata mtoto wa kiume na mme wa huyo mwanamke hajui lolote kwamba analea mtoto wa mwenzake. Na yeye anataka afanye harakati amchukue mtoto wake.

Najutia dhambi niliyoifanya na nimbaya sana. Lakini mtoto wangu namtaka nawaombeni msaada. Nimejutia dhambi hivyo naomba ushauri tu na sio matusi.

nakutakia kila la kheri nenda kadai huyo mtoto halafu uone aibu ya uzinzi
 
Du! please kama ushatubu hiyo dhambi yako yatosha. Lakini halahala ucjemuaribia dada wa watu ndoa yake maana ataachwa kimoja ila ingawa na wewe ndoa yako itasuwasuwa kidogo lakini kama mwanaume bado utakuwa na uwezo wa kumshawishi mkeo abaki maana umeamua kumueleza ukweli.

mliahidiana kuzaa katoto cha ukumbusho c azae halafu akupe, endelea tu kukachapo aiseeeee, mshahara wa dhambi ni mauti tena ya kukusudia!
 
Jamani, ninawashukuru kwa ushauri wenu. Nawaombea mlionitukana pia. Mimi ni binadamu na kuna kuteleza. Ila ninawashukuru sana watu wote mliotoa ushauri kwamba niachane na kudai mtoto. Asanteni sana na hakika mimi na mke wangu tunafurahia kulea watoto tuliobarikiwa na Mungu. Asanteni.
Pole na Hongera kwa kukubali, wengine tulishakubali na yameisha.Ni vigumu kudai mtoto kwenye nyumba ya mtu, Kaka usijaribu. we endelea na maisha yako sahau kuhusu huyo mtoto.
 
Wewe ni mbinafsi na unastahili kupigwa risasi kichwani.
 
Ndo maana nataka niweke kila kitu wazi, hapa hujaamini kwamba nimeokoka? Mbona nimemweleza hata mke wangu na kumuomba msamaha? Hata yeye ameniunga mkono kwamba anataka akae na mtoto amlee.
OK. Umemueleza mkeo na amekubali na kukusamehe, lakini kwa nini usiongee na huyo mwanamke ulie zaa nae pia umsikilize anasemaje, kama na yeye anaweza kumueleza mumewe hilo swala mwambie aliweke wazi na kama akisema hawezi kuliweka wazi na kukupa huyo mototo umsikilize na achana na hilo wazo la kudai motto. Makubaliano yenu mwanake azae na abaki na motto kwa nini unageuka? Acha kumvunjia mwenzio nyumba yake, matokeo yanaweza kuwa mabaya ukajuta milele yote, huyo mama wa watu akiachwa na kuamua kujitoa uhai wake baadae motto aje aambiwe chanzo cha kifo cha mama ake unategemea amani kutoka kwa huyo mototo? ACHA UBINAFSI.
 
mimi nakushauli hilo jambo ukaliacha tu, litakuletea mazingira magumu sana hapo baadaye
 
we naona unataka kuleta balaa kwenye ndoa ya mwenzio
 
Back
Top Bottom