Naumia kumuona mtoto wangu

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Ndugu zanguni wana JF, natumaini nyote ni wazima wa afya!

Juzi, nilikua na maongezi ya muda mrefu na mfanyakazi mwenzangu. Katika maongezi, nikagundua kwamba yeye, kama nilivyo mimi, anaumia sana. Aliponieleza shida yake, nilimwambia wazi kwamba nami nateseka na mawazo kama wewe.

Hivyo nikashindwa kumpa ushauri maana tatizo lake linafanana na langu. Mawazo yenu yatasaidia nijue la kufanya, na yeye akiyasoma atapata uamuzi afanye nini.

Mimi, kabla sijaokoka nilikua na mahusiano na mke wa mtu. Nilibahatika kuzaa nae mtoto wa kike. Mme wake yupo ila huyu mwanamke tulipendana sana ila hatukubahatika kuoana. Alipoolewa, na hata mimi baada ya kuoa, mahusiano yetu yaliendelea tena vibaya sana.

Mwaka juzi mwanzoni tulishauriana tuache maana tulikua tunatenda dhambi ila tuliamua kuwa na mtoto awe ukumbusho wetu. Na kweli tukabahatika kumpata mtoto huyu wa kike.

Kwa huyu bwana, kama ilivyo kwangu, huyu nimtoto wa kike pekee. Ninao watoto wakiume 3. Yeye anao watoto wa kiume wawili na alivyoona huyu amwezaliwa, alimweleza mke wake kwamba wanatosha. Anampenda sana mtoto huyu wa kike.

Sasa mi naumia sana. Siku moja nikiwa na mke na watoto wangu supermarket mmoja ya hapa, niliwaona wao pia wakiwa katika heka heka ya shopping wakiwa na mtoto wangu. Niliumia sana. Sasa nataka nifanye harakati nimchukue mtoto wangu. Nifanyeje jamani nisaidie.

Mfanyakazi mwenzangu yeye alimpa binti wakati anasoma na bila kujua, binti alikua mchumba wa mtu.

Alipoolewa aliolewa na ujauzito wa jamaa. Yeye alipata mtoto wa kiume na mme wa huyo mwanamke hajui lolote kwamba analea mtoto wa mwenzake. Na yeye anataka afanye harakati amchukue mtoto wake.

Najutia dhambi niliyoifanya na nimbaya sana. Lakini mtoto wangu namtaka nawaombeni msaada. Nimejutia dhambi hivyo naomba ushauri tu na sio matusi.
 
Duh...apo inabid pia uwaze consequence zake zitakueje?...je mke wako na mume wa huyo dada watalichukuliaje ilo suala
 
Mi nakushauri tafuta wazee wenye hekima wakazungumze na huyo baba. Kama mnasali wote tumia hata wazee wa kanisa wenye hekima. Hata kama ungekuwa huumii bado ungetakiwa kuweka wazi hilo suala ili uwe huru....
 
Sema unataka kuvunja ndoa ya huyo mwanamke.. Akiwa mke wangu alafu nikagundua hilo namuacha huyo mwanamke ila nafanya jambo lingine la kuwafanya msinisahau.

Maana mnakua mmenipotezea vitu ambavyo siwezi kuvirecover,time and resources,naweza recover resources but not time,nguvu,upendo,usumbufu. Kwa kweli siwaachi hivi hivi.
 
Mi nakushauri tafuta wazee wenye hekima wakazungumze na huyo baba. Kama mnasali wote tumia hata wazee wa kanisa wenye hekima. Hata kama ungekuwa huumii bado ungetakiwa kuweka wazi hilo suala ili uwe huru....

Huyo mwanaume sidhani kama ataelewa maana wamezaa tayari huyo mwanamke akiwa kwenye ndoa.

Hata kama ni mimi siwezi kuelewa. Hata akija na wazee gani.
 
.....na akae kimya milele....mshayakoroga kwa kuchangia mambo yaliyopelekea uzao wa huyo mtoto. kwa sasa unatafuta mkoroganyo mwingine wa kutimbwilisha ndoa zote mbili....

Kaah...ila wapendwa nanyi kiboko, haya sie wa mataifa tufanyeje?
 
Kwa huyu bwana said:
huyu nimtoto wa kike pekee[/B]. Ninao watoto wakiume 3. Yeye anao watoto wa kiume wawili na alivyoona huyu amwezaliwa, alimweleza mke wake kwamba wanatosha. Anampenda sana mtoto huyu wa kike.
Sipati picha jamaa anavyokapenda anacheza nako kumbe mke wake anamchora tu na kujisemea kimoyomoyo"----- we lea tu mtoto wa mwaname mwenzio....dah wanawake bhana!
Anyway nakushauri nawe utafute mtu akufetulie mke wako naye azae wa kike!
 
Ndugu zanguni wana JF, natumaini nyote ni wazima wa afya!

Juzi, nilikua na maongezi ya muda mrefu na mfanyakazi mwenzangu. Katika maongezi, nikagundua kwamba yeye, kama nilivyo mimi, anaumia sana. Aliponieleza shida yake, nilimwambia wazi kwamba nami nateseka na mawazo kama wewe. Hivyo nikashindwa kumpa ushauri maana tatizo lake linafanana na langu. Mawazo yenu yatasaidia nijue la kufanya, na yeye akiyasoma atapata uamuzi afanye nini.

Mimi, kabla sijaokoka nilikua na mahusiano na mke wa mtu. Nilibahatika kuzaa nae mtoto wa kike. Mme wake yupo ila huyu mwanamke tulipendana sana ila hatukubahatika kuoana. Alipoolewa, na hata mimi baada ya kuoa, mahusiano yetu yaliendelea tena vibaya sana. Mwaka juzi mwanzoni tulishauriana tuache maana tulikua tunatenda dhambi ila tuliamua kuwa na mtoto awe ukumbusho wetu. Na kweli tukabahatika kumpata mtoto huyu wa kike.

Kwa huyu bwana, kama ilivyo kwangu, huyu nimtoto wa kike pekee. Ninao watoto wakiume 3. Yeye anao watoto wa kiume wawili na alivyoona huyu amwezaliwa, alimweleza mke wake kwamba wanatosha. Anampenda sana mtoto huyu wa kike.

Sasa mi naumia sana. Siku moja nikiwa na mke na watoto wangu supermarket mmoja ya hapa, niliwaona wao pia wakiwa katika heka heka ya shopping wakiwa na mtoto wangu. Niliumia sana. Sasa nataka nifanye harakati nimchukue mtoto wangu. Nifanyeje jamani nisaidie.

Mfanyakazi mwenzangu yeye alimpa binti wakati anasoma na bila kujua, binti alikua mchumba wa mtu. Alipoolewa aliolewa na ujauzito wa jamaa. Yeye alipata mtoto wa kiume na mme wa huyo mwanamke hajui lolote kwamba analea mtoto wa mwenzake. Na yeye anataka afanye harakati amchukue mtoto wake.

Najutia dhambi niliyoifanya na nimbaya sana. Lakini mtoto wangu namtaka nawaombeni msaada. Nimejutia dhambi hivyo naomba ushauri tu na sio matusi.

Kwanza una uhakika gani kwamba mtoto ni kwako kibiologia? Maana huyo mke wa mtu na wewe ni mwizi tu. Mlichepuka kufanya DNA? Au mnatumia ile DNA ya "macho"? Tayari ulishaharibu usitake kuharibu zaidi - mtoto sio wa kwako!
 
Jitahidi kuwa na roho ngumu, kubali watoto ulionao ndio wa kwako na huyo mwingine sio wako maana Baba anayeishi naye ndiye anaamini kuwa ni mwanae. Kwanza hata mtoto mwenyewe hana na hatakuwa na upendo wowote na wewe. Usijidanganye, tulia ishi kama wazee wetu walivoishi. Enzi zile utakuta mzee kazaa na jirani lkn inakuwa ni siri hadi kufa.
 
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana.Wewe mwenywe ilikubali ukiwa unajua kuwa hutokuja kupata umiliki wa huyo mtoto.Embu acheni huo ujinga aisee,nyie subirini adhabu zenu za pili maana adhabu ya kwanza ni hiyo karma a.k.a majuto,ya pili mtaikuta kwa Mungu baada ya kutenda dhambi.

Acheni hayo mawazo,live with it.Hilo unalo taka kulifanya sio suluhisho na wala halitoondoa dhambi uliyofanya sanasana utasababisha mateso kwa familia zenu na kuzidi kuwaumiza watoto wa pande zote mbili hadi huyo mtoto unaye mpigania
 
where silence can do better dont tell the truth kama wote wangekua wameokoka sawa utavunja ndoa za watu acha upumbafu jinsi unavo umia mwenzio ataumia mala mia just step into the shoes of ur fellow men
 
vtu vifuatavyo vitatokea jiandae
ndoa zote mbili kuingia mgogoroni
mkeo ni ngumu kumkubali mtoto
heshma kushuka
 
huyu nimtoto wa kike pekee. Ninao watoto wakiume 3.

.

mkuu hebu tuanzie hapo kwenye hayo maneno yako,
1.mtoto alie katika ndoa/familia ya mtu mwingine unamuita ndo mtoto wako wa kike pekee,je ushawahi kujiuliza utasababisha matatizo kiasi gani katika familia hiyo endapo baba wa hiyo familia atagundua mtoto siyo wake!!!?
2.Je ushajiuliza hao watoto watatu wakiume unaosema ni wako,endapo akitokea mtu na kudai ni wa kwake na mkeo akathibitisha hilo,wewe utachukua uamuzi gani!!!?

Ukinijibu nitarudi kwa ushauri
 
.....na akae kimya milele....mshayakoroga kwa kuchangia mambo yaliyopelekea uzao wa huyo mtoto. kwa sasa unatafuta mkoroganyo mwingine wa kutimbwilisha ndoa zote mbili....

Kaah...ila wapendwa nanyi kiboko, haya sie wa mataifa tufanyeje?

Ameandika kwamba alifanya hayo kabla hajaokoka. Maandishi hayo hujayaona au uneamua kuyafumbia macho makusudi?
 
Back
Top Bottom