Nauliza shujaa wa tiktok Habil Kabil yuko wapi?

Nauliza shujaa wa tiktok Habil Kabil yuko wapi?

Jee hiyo tabia ya CCM ya kutokutaka kutoa dola Kwa njia ya kidemokrasia ni halali?

Maandiko yako wakati wote huwa yanaonesha uhalali wa CCM kutumia kila njia kubaki madarakani.

Kubali Kuna watu wanaona njia inayotumiwa na CCM kubaki madarakani ni haramu.
Mimi sio CCM na wanaonijua vizuri Mimi nishafanya harakati za Field na sio haya mambo ya keyboard

Then Mimi ili unielewe usiweke HISIA .

Mimi hapa ni victim wa siasa za CCM na nimekuwa nikiwapinga Sana na sio mitandaoni Ila Field.

Zipo njia ambazo najua tukizitumia basi tutafanikiwa na sio Kama wanavyofanya Chadema , na Gen Z

Hizo harakati tumefanya kitambo mpaka tukawa dead body .

Nikiona watu wananiita CHAWA huwa nacheka kwakuwa hawajui nini nimewahi kufanya kuhusu NCHI yangu.

Sisi sio watu wa Ku-brag kuwa nimefanya hiki na kile Ila siasa tumeanza kutambo Sana .

Kuitoa CCM madarakani ni VITA hauwezi ukawa unataka kuitoa CCM madarakani mnakaa Tiktok mnajadili mambo yenu ya maandamano sijui hivi na vile na mkasema mtatoboa

Njia ambayo nilimpa Joel Nanauka nadhani ndo njia sahihi Sana ambayo wangeipata Chadema tungekuwa hatuna CCM

Ila dharau za kejeli na Kuita kila MTU chawa haifai.
 
Mimi sio CCM na wanaonijua vizuri Mimi nishafanya harakati za Field na sio haya mambo ya keyboard
Kwanza kusema ulikuwa field ni mambo ya kinadharia zaidi na hayana uhalisia. Unatumia jina bandia halafu unataka tukuamini wewe uliwahi kuwa kinyume na CCM?

Mambo ya keyboard unayadharau lakini wewe ni mmojawapo wa washinda kwenye hiyo keyboard. Na Kwa zama hizi mambo mengi huanzia mitandaoni.

Kama keyboard haina taathira (impact) kwa nini watawala wanahangaika kuwafungulia kesi kina Mange Kimambi na wenzake?

Unasema mambo ya keyboard wakati unaowatetea wanapambana hata na hii JF tunayoitumia hivi Sasa kujadiliana Mimi na wewe.
 
Sawa , je ni sahihi VIJANA kuandamana ?
 
Sawa , je ni sahihi VIJANA kuandamana ?
Kabisa... Maana siyo jambo baya kuandamana...

Kuna hoja kuwa walitaka kupindua Serikali... Sijui kama tunajua Serikali huwa inapinduliwaje.

Mwalimu Nyerere alinusurika kupinduliwa mara zaidi ya mbili lakini rasmi ni mwaka 1964 na mwaka 1982. Ulisikia ni watu wangapi waliuawa zaidi ya Tamim(Komandoo)?

CCM imeshusha sana viwango vya Mapinduzi na Uhaini ili tu kukidhi haja zao za kisiasa.
 
Mimi sio CCM na wanaonijua vizuri Mimi nishafanya harakati za Field na sio haya mambo ya keyboard

Then Mimi ili unielewe usiweke HISIA .

Mimi hapa ni victim wa siasa za CCM na nimekuwa nikiwapinga Sana na sio mitandaoni Ila Field.

Zipo njia ambazo najua tukizitumia basi tutafanikiwa na sio Kama wanavyofanya Chadema , na Gen Z

Hizo harakati tumefanya kitambo mpaka tukawa dead body .

Nikiona watu wananiita CHAWA huwa nacheka kwakuwa hawajui nini nimewahi kufanya kuhusu NCHI yangu.

Sisi sio watu wa Ku-brag kuwa nimefanya hiki na kile Ila siasa tumeanza kutambo Sana .

Kuitoa CCM madarakani ni VITA hauwezi ukawa unataka kuitoa CCM madarakani mnakaa Tiktok mnajadili mambo yenu ya maandamano sijui hivi na vile na mkasema mtatoboa

Njia ambayo nilimpa Joel Nanauka nadhani ndo njia sahihi Sana ambayo wangeipata Chadema tungekuwa hatuna CCM

Ila dharau za kejeli na Kuita kila MTU chawa haifai.
You are displaying your failure in the public.... Unadai wewe umepigana sana huko ''field''. Mbona hakuna matokeo? Gen Z na CHADEMA (chini ya Lissu, baada ya kuondoka yule msaliti) wamakiwasha muda mfupi sana na duniani yote imejua mpaka CCM imetikisika! Wewe ni ndiye failure mkubwa ambaye ulipoteza nguvu bila kuwa na matokeo yoyote!
 
Wakati umefika kwa wa Tanzania ku engage na kuchambua siasa kwa uhuru pasipo kuwategemea sana wanaharakati na wapinzani kwani kila mmoja ana agenda zake binafsi anazozificha nyuma ya pazia la MAPINDUZI/MABADILIKO.

Mfano:
Maria Sarungi, Cyprian, Hilda, Tito, Mbowe, Kigogo, Ansbert Ngurumo ni wanufaika wa Mabilioni kutoka Ford foundation n.k.

Hii inaitwa PAID ACTIVISM.

Paid activism ina entail uwezo wa kununua mashabiki na wapambe ili kupata jukwaa kubwa la wasikilizaji watakaokuza mradi wao wa harakati. Mwisho wa siku, wanaandaa ripoti kila mwaka kuonyesha wadhamini ushiriki wenu na idadi ya wafuasi na namna walivyofanikiwa kuwafikia.

Ndiyo maana, Maria Sarungi, Mbishi, Cyprian, walijikuta na wafuasi wengi kama uyoga ghafla kwanzia mwaka 2020 na kuendelea.
Maria Space ni zao la ufadhili wa Ford licha ya kuwa hajawahi kuwatambua kwenye kurasa zake za kijamii!

Swali linakuja, anaficha udhamini ili iweje na kwa manufaa gani na ya nani?

Nani anaweza kupokea kiwango kikubwa cha fedha namna hiyo kupitia A/C za TZ bila kibali cha CCM/serikali?

Wakishapewa kibali cha kupokea fedha za kuwezesha harakati na serikali ya CCM, unadhani hawapewi masharti?? Masharti ambayo yakikiukwa fedha zao zitazuiwa??

Kama CCM wakiamua ku match hela wanazopokea na kuwanunua au kuwatumia kusambaza propaganda zao kijanja nyuma ya camera mtajua?
Mf propaganda za Mafia Sarungi kuhusu Baba wa Taifa kupitia hashtag yake ya #Dear Nyerere na Benjamin Mkapa aka Anko Ben kama Maria anavyomwita.

Hotuba za Nyerere zina maneno mazuri sana ambayo yeye hakuyaishi. Aliteka na kupoteza sana raia waliomkosoa pamoja na kuwafungulia kesi za UHAINI. Mf Oscar Kambona na Bibi Titi Mohamed. Pia alipiga marufuku vitabu fikirishi Mf Animal Farm, vilivyoainisha mapungufu ya UJAMAA. Alitawala TZ kwa miaka 25 na alikuwa besti wa madikteta kama vile Mao wa China na Nicolae Ceausescu dikteta wa Romania aliyehukumiwa kifo na wananchi wake mwenyewe!

Mange Kimambi, Double agent, ambaye sifa yake kubwa ni kampeni za umbea, drama/maigizo na kukosa msimamo. Ndivyo alivyojipatia umaarufu wake.

Aligombea ubunge wa CCM jimbo la Kinondoni mwaka 2015 akashindwa kwenye kura za maoni.

Mange aliyempigia kampeni JPM na kumdhalilisha Lowassa kisiasa ili kumwongezea uhalali JPM alibadili mwelekeo baada ya JPM kuingia madadakani, akaanza kumkosoa vikali na kujifanya ameachana na CCM hadi pale JPM alipotangulia mbele za haki.

Samia alipoingia, Mange akawahi mapema hadharani kuja kujitangaza kama "Chawa wa Mama Samia" hata akaenda kumlaki alipokwenda Marekani kikazi.

Hata hivyo alibadili mwelekeo ghafla tangu mwaka 2024, bila kutangaza rasmi msimamo wake kwenye harakati za kisiasa mpaka ilipofika Juni 2025.

Mange Kimambi pia aliweka wazi kuwa Abduli mtoto wa Samia anafahamu hadi anwani yake ya anapoishi Marekani na alijaribu kumhonga akakataa ilihali kulikuwa na mgogoro kati ya Mange na benki ya CRDB ambao uwazi wake hatuujui.

Mange huyo huyo, kupitia kurasa zake za Instagram, amekuwa akianika ufisadi wa Abduli na serikali ya Samia LAKINI, mtakumbuka kuwa ushahidi mwingi alioutoa unaonyesha nyaraka za miaka michache iliyopota. Mf nyaraka za Access bank n.k.

Sitilii shaka ufisadi wa Samia na CCM hata kidogo! Swali langu ni, Je, kwanini alisubiri miaka yote kuanika haya? Nini kilibadilika hapo katikati? Je, Waligombana juu ya malipo? Tusishau ilivyotokea miezi michache baada ya mgogoro kati yake na CRDB bank!

Je, ni kweli kwamba wa Tanzania tunahitaji Mange aanike ushahidi mdogo alionao wa ufisadi wa kina Abduli ili tiweze kujua kuwa kuna UFISADI mkubwa unaendelea??
Yaani, Hatukujua siku zote hizi kuwa nchi yetu imegubikwa na rushwa tangu enzi za Mwinyi mpaka leo?
Ugumu wa maisha unapokithiri, deni la taifa linavyozidi kupanda, hatuelewi uhusiano uliopo kati yake na ufisadi wa hali ya juu mpaka "Dada yenu wa Taifa" aka Mange Kimambi alipwe na Ford na CCM Anti Samia faction, aje kuwachotea chakula kwenye sahani awalishe na kijiko??

Je, Mange akilipwa na CCM nyuma ya pazia kupotosha umma, tutajuaje tofauti kama hata tathmini hatumfanyii na anayedikriki kutoa maoni huru au kumkosoa Mange/Maria Sarungi anapewa jina la CHAWA?

Alipotuambia kuhusu JWTZ kuwa upande wetu na kutuagiza kuchoma vitu ili wapate sababu ya kuchukua nchi, tukatekeleza tukajifunza kuwa HAIKUWA KWELI, kwa gharama ya UHAI wa watu >10,000! Mbaya zaidi, hakuja kujieleza ni kwanini alitoa ujumbe wa aina hiyo, uliopotosha mpaka kugharimu maisha ya watu! Mf: kama na yeye alipotoshwa na ilikuwaje akapotoshwa n.k. ili wa TZ wanaotumia akili tuweze kumwelewa.

Ni afadhali angeacha tutathmini hali wenyewe na kujihami kwa akili zetu kuliko kumsikiliza yeye bila kuhoji taarifa zake kama MPIGA RAMLI??

Je, Kwanini Mnamo June 2025 Club huouse, chumba cha "SAUTI YA WATANZANIA" Waliandaa theme MAALUM ya "TUNAM SUPPORT DADA WA TAIFA, MANGE KIMAMBI, ANA SILAHA ZA MAANGAMIZI" wakati ule ule ambao Mange Kimambi ali declare kuingia rasmi kwenye harakati 💯% hadi Novemba baada ya uchaguzi, kisha kuomba support ya subscription ya App yake ili kumwezesha kiuchumi?? Huu ni MKAKATI wa kum promote mhuni ambaye pia ni DOUBLE AGENT au BAHATI MBAYA?

Ni kwanini App yake, haina umbea wala taarifa mpya za kutosha tangu mwaka 2021/2? Siasa hapo ni kisingizio tu, hakuna jipya kwa zaidi ya miaka 2. Waliofuata mkumbo wakailipia kum support watanielewa.

Conclusion: Tuwe makini sana na wanasiasa na wanaharakati pia.
Ni kweli wana harakati wanaolipwa wanasaidia kufichua maovu lakini pia msaada wao unaishia pale utashi wao unapoishia hasa kama SIO WAKWELI wala WAWAZI kama hawa wa kwetu! Lazima tuwahoji na kuwakosoa kina Maria Sarungi, Mange Kimambi na wanaharaki wote ILI tuweze KWENDA SAWA!!
KAMA WAMEJIAJIRI KUKOSOA WENGINE NA WAO WAWE TAYARI KUHOJIWA NA KUKOSOLEWA, HAWATAKI, WASOGEE PEMBENI WAINGIE WATU WASAFI NA WENYE UWEZO WA KUPOKEA NA KUHESHIMU MAWAZO HURU‼️
Leo ukimkosoa Maria Sarungi kwenye ukurasa wake wa X au Instagram hata kwa nia njema unapigwa block! 🚫
Yaani, hawataki kukosolewa wakati wanalipwa na Ford kukosoa CCM?? Wana tofauti gani na wanasiasa ma-dikteta??

Wanapoficha
taarifa za udhamini wao PAID ACTIVISM, wanakuwa na undeclared Conflict of interest! inayo ashiria ukosefu wa Integrity kitu ambacho CCM pia hawana.

ANAYETAKA KUIHOJI CCM/SERIKALI, AWE TAYARI KUHOJIWA PIA‼️

WANAHARAKATI NI WATU NA WANA MAPUNGUFU KAMA WENGINE! SIO WATIMILIFU!
Mwanaharakati asiyetaka kuhojiwa wala kukosolewa NI TAPELI! Lengo ni kujipa uhuru wa kutugeuka muda wowote! Ndiyo maana TZ ina historia ya kuwa na Matapeli wengi wa harakati Mf Polepole, Prof. Kabudi, Prof. Kitila Mkumbo, Wakili Madeleka na LIST itaendelea kukua kila kukicha!

TUKISHINDWA KUWAWAJIBISHA WANAHARAKATI WETU, MAPINDUZI TUTAENDELEA KUYASIKIA KWA WENZETU KAMA NEPAL‼️

I rest my case.
 
Baada ya wagalatia kujua kuwa ni Ustaadhi, wote wakala kushoto na kumgeuka
 
Ahaaa - kwahiyo mnataka watu wote tuwe na mawazo yanayofanana

Mimi niliongea hapa kuwa 29/10 vijana wasithubutu kuandamana kwakuwa wanaweza kupata madhara makubwa .

Watu wakasema sisi ni CHAWA.

Mkuu kupambana na CCM inahitaji mikakati ya siri na kujifua Sana na sio Kama ilivyo kule Tiktok.

Achievement iliyopatikana mpaka sasa ni VIFO Vya watu.

Ukiongea hivi unaitwa CHAWA
Bila shaka wewe siyo chawa ila ni mtu asiye na vision, mwenye upeo mdogo wa kuangalia mambo kwa kina. Vifo vilivyotokea vimefungua ukurasa mpya na Tanzania wakati wa uchaguzi haitakuwa tena kama ilivyokuwa. Mimi ni wale watu wanaongalia mambo kwa muda mrefu na siyo wewe unayetaka shortcut.
 
You are displaying your failure in the public.... Unadai wewe umepigana sana huko ''field''. Mbona hakuna matokeo? Gen Z na CHADEMA (chini ya Lissu, baada ya kuondoka yule msaliti) wamakiwasha muda mfupi sana na duniani yote imejua mpaka CCM imetikisika! Wewe ni ndiye failure mkubwa ambaye ulipoteza nguvu bila kuwa na matokeo yoyote!
Hakuna walichowasha wala hakuna achievement yoyote zaidi ya kuwasukumiza vijana wakauliwe Kama Kuku

Kwanza nyie keyboard sitaki hata kuwasikia hamjitambui

Angekuwa amekufa mwanao ungeongea huu upumbavu unaosifia hapa tumieni ufahamu wenu vzr acha mihemko na ubinfasi
 
Bila shaka wewe siyo chawa ila ni mtu asiye na vision, mwenye upeo mdogo wa kuangalia mambo kwa kina. Vifo vilivyotokea vimefungua ukurasa mpya na Tanzania wakati wa uchaguzi haitakuwa tena kama ilivyokuwa. Mimi ni wale watu wanaongalia mambo kwa muda mrefu na siyo wewe unayetaka shortcut.

Ndo maana tuna push movement mpya na Nanauka ili tuone .

Wewe hauwezi ukakaa huko unamtuma Kijana aandamamane ili auliwe haiwezekani.

Ukianzisha VITA pambana mwenyewe na sio kuwatumia vijana
 
Huyu jamaa alikuwa anapanda mbegu ya mapinduzi kwa vijana na alikuwa anawapa nguvu ya kujiamini dhidi ya watawala wezi wa rasilimari za inchi,kokote aliko tunamuitaji
🤣🤣🤣😂😂 Mna waziimu aise...
 
Ndo maana tuna push movement mpya na Nanauka ili tuone .

Wewe hauwezi ukakaa huko unamtuma Kijana aandamamane ili auliwe haiwezekani.

Ukianzisha VITA pambana mwenyewe na sio kuwatumia vijana
Mara hii umehamisha goli na kupiga ramli kuwa mimi natuma vijana? Hukujibu nililoli-challenge.
 
Hakuna walichowasha wala hakuna achievement yoyote zaidi ya kuwasukumiza vijana wakauliwe Kama Kuku

Kwanza nyie keyboard sitaki hata kuwasikia hamjitambui

Angekuwa amekufa mwanao ungeongea huu upumbavu unaosifia hapa tumieni ufahamu wenu vzr acha mihemko na ubinfasi
You claim to have fought for justice for many years until exhaustion set in. I asked you..... after all that time, what have you truly achieved, when others (Gen Z) have managed to shake the nation in a much shorter period? That is the crux of the argument.
 
Mara hii umehamisha goli na kupiga ramli kuwa mimi natuma vijana? Hukujibu nililoli-challenge.
Halafu CCM watu ajabu sana. Badala ya kutafuta suluhisho la tatizo wao huleta watu.

Sasa huyu yupo bize kumtajataja Nanauka kama vile wizara iliyopo haijawahi kuongozwa na Juliana shonza.

Keshasahu "project" Yao na kina Habib Mchange, Mtela mwampamba, Patrobas katambi na wengineo.

Tatizo siyo nani anaongoza wizara ya vijana bali mtizamo wa hao wanaoiongoza hiyo wizara.
 
Waliuawa "kama kuku" kama vile ni jambo dogo sana.

Jee waliowaua walikuwa na haki ya kuwaua?

Mimi movement yangu inasema hivi

"Don't play someone's game "

Kwahiyo haitoishia kwa raia mpaka katika security agency itafika

Kwahiyo haijalishi wewe ni Askari , mwnajeshi au Tiss n.k Ila usikubali Ku-play someone's game

CCM ikianzisha VITA vita waliionzisha waimalize bila kumtumia Kijana yoyote haijalishi yupo ktk security agency au wapi

Na GEN Z wasitumike kukipambania Chama Fulani

Anayetaka madaraka ajipambanie mwenyewe aingie front

Kama unavyoona Russia na Ukraine wanaoliwa ni wanajeshi wakati walioanzisha VITA ni wanasiasa.
 
Back
Top Bottom