Wakati umefika kwa wa Tanzania ku engage na kuchambua siasa kwa uhuru pasipo kuwategemea sana wanaharakati na wapinzani kwani kila mmoja ana agenda zake binafsi anazozificha nyuma ya pazia la MAPINDUZI/MABADILIKO.
Mfano: Maria Sarungi, Cyprian, Hilda, Tito, Mbowe, Kigogo, Ansbert Ngurumo ni wanufaika wa Mabilioni kutoka Ford foundation n.k.
Hii inaitwa PAID ACTIVISM.
Paod activism ina entail uwezo wa kununua mashabiki na wapambe ili kupata jukwaa kubwa la wasikilizaji watakaokuza biashara yao ya harakati. Mwisho wa siku, wanaandaa ripoti kuonyesha wadhamini ushiriki wenu na idadi ya wafuasi na namna walivyofanikiwa kuwafikia.
Ndiyo maana, Maria Sarungi, Mbishi, Cyprian, walijikuta na wafuasi wengi kama uyoga ghafla kwanzia mwaka 2020 na kuendelea.
Maria Space ni zao la ufadhili wa Ford licha ya kuwa hajawahi kuwatambua kwenye kurasa zake za kijamii!
Swali linakuja, anaficha udhamini ili iweje na kwa manufaa ya nani?
Nani anaweza kupokea kiwango kikubwa cha fedha namna hiyo kupitia A/C za TZ bila CCM/serikali kuruhusu?
Wakishapewa kibali cha kupokea fedha za kuwezesha harakati na serikali ya CCM, unadhani hawapewi masharti?? Masharti ambayo yakikiukwa fedha zao zitazuiwa??
Kama CCM wakiamua ku match hela wanazopokea na kuwanunua au kuwatumia kusambaza propaganda zao kijanja nyuma ya camera mtajua?
Mf propaganda za Baba wa Taifa #Dear Nyerere na Benjamin Mkapa aka Anko Ben kama Maria anavyomwita.
Nyerere aliongea maneno mazuri bila kuyaishi na aliteka na kupoteza raia waliomkosoa. Pia alizuia vitabu fikirishi Mf Animal Farm. Alitawala TZ kwa miaka 25 na alikuwa besti wa madikteta kama vile Mao na Nicolae Ceausescu dikteta wa Romania aliyehukumiwa kifo na wananchi wake mwenyewe!
Mange Kimambi, Double agent, ambaye sifa yake kubwa ni kampeni za umbea, drama/maigizo na kukosa msimamo. Ndivyo alivyojipatia umaarufu wake.
Alikua CCM, tena aligombea ubunge wa Kinondoni kupitia chama chake pendwa mwaka 2015 akashindwa kura za maoni.
Mange alionekana kumkosoa vikali Magufuli na kujifanya ameachana na CCM hadi pale JPM alipoondoka.
Samia alipoingia, Mange akaja hadharani kujitangaza kama "Chawa wa Mama Samia" na akaenda kumlaki aliposafiri kikazi kwenda Marekani.
Hata hivyo alibadili mwelekeo ghafla tangu mwaka 2024, bila kutangaza wasmi msimamo wake mpaka 2025 Juni.
Mange Kimambi pia aliweka wazi kuwa Abduli mtoto wa Samia anafahamu hadi anwani yake ya anapoishi na alijaribu kumhonga akakataa ilihali kulikuwa na mgogoro kati ya Mange na benki ya CRDB ambao uwazi wake hatuujui.
Mange huyo huyo, kupitia kirasa zake za Instagram, amekuwa akianika ufisadi wa Abduli na serikali ya Samia LAKINI, ushahidi mwingi alioutoa unaonyesha nyaraka za miaka michache iliyopota. Mf nyaraka za Access bank nk
Si kwamba ushahidi una mashaka, swali langu ni, Je, kwanini alisubiri miaka kabla ya kuja kuwaanika? Tena baada ya mgogoro kati yake na CRDB bank?
Je, ni kweli kwamba wa Tanzania tulihitaji Mange aje kuanika usbahidi wa ufisadi wa kina Abduli na Samia kwa sisi kujua kuwa kuna UFISADI mkubwa unaendelea?? Hatukujua siku zote kuwa nchi yetu imegubikwa na rushwa??
Je, Mange akilipwa na CCM nyuma ya pazia kupotosha umma, tutajuaje?
Alipokuja kutuambia kuhusu JWTZ kuwa upande wetu tukakuta ni UWONGO, Si afadhadhali angetuacha tutathmini hali wenyewe na kujihami kwa akili zetu kuliko kumsikiliza yeye kama MPIGA RAMLI??
Je, Kwanini Mnamo June 2025 Club huouse, chumba cha "SAUTI YA WATANZANIA" Waliandaa theme MAALUM ya "TUNAM SUPPORT DADA WA TAIFA, MANGE KIMAMBI, ANA SILAHA ZA MAANGAMIZI" wakati ule ule ambao Mange Kimambi ali declare kuingia kwenye harakati 💯% na kuomba support ya subscription ya App yake ili kumwezesha kiuchumi?? Huu ni MKAKATI wa kum promote mhuni ambaye pia ni DOUBLE AGENT au BAHATI MBAYA?
Ni kwanini App yake, ukiiangalia, haina umbea wala taarifa yoyote ya maana tangu mwaka 2021/2? Yaani Siasa hapo ni kisingizio tu, hakukuwa na jipya kwa miaka kadhaa hapo katikati. Waliolipia app yake kum support bila kumtathmini wataelewa hili.
Conclusion: Wa Tanzania tuwe makini sana, Wana harakati wanaolipwa wanasaidia kufichua maovu lakini pia msaada wao unaishia pale utashi wao unapoishia hasa kama SIO WAKWELI wala WAWAZI kama hawa wa kwetu! Lazima tuwahoji na kjwakosoa kina Maria Sarungi, Mange Kimambi na wanaharaki wote ILI tuweze KWENDA SAWA!! WAMEJIAJIRI KUKOSOA WATU NA WAO WAWE TAYARI KUHOJIWA NA KUKOSOLEWA, HAWATAKI, WASOGEE PEMBENI WAINGIE WATU WASAFI NA WENYE NGOZI YA KUPOKEA NA KUHESHIMU MAWAZO HURU‼️ Leo ukimkosoa Maria Sarungi kwenye ukurasa wake wa X au Instagram hata kwa nia njema unapigwa block! 🚫
Yaani, hataki kukosolewa wakati analipwa na Ford kukosoa CCM?? Huyu sasa anatofauti gani na mwanasiasa dikteta??
Wanapoficha taarifa za udhamini wao PAID ACTIVISM, ina ashiria ukosefu wa Integrity kitu ambacho CCM pia hawana.
KAMA TUNATAKA KUWAHOJI CCM, TUWAHOJI NA WANAHARAKATI WANAPOKOSEA! SIO WATIMILIFU! LA SIVYO TUNAUZIWA UTAPELI NA MAPINDUZI TUTAENDELEA KUYASIKIA KWA WENZETU KAMA NEPAL‼️
I rest my case.