Karibuni tena watoto wote katika kipindi mkipendacho, kipindi cha Mama na Mwana. Siku ya leo hakuna watoto waliotutembelea studio, ila nimewaandalia hadith nzuri sana ya Mwana na Bint Mfalme. Leo mtakuwa nami Uncle Bob XP, ila shangazi yenu Deborah Mwenda, hatokuwepo kwa sababu zisizo weza kuzuhilika.Haya basi na tuanze...Paukwaa... Pakawaaa...!Alitokeani... Naaam Twahib!Alitokea chanjagaa... kajenga nyumba kakaaa... Na kilango cha kupita... Mwanangu mwana wa Siti Vijino kama Chikichi!Hadithi... Hadithi...!Hadithi njoo.Hapo zamani za kale, paliondokea mtoto wa mfalme, alieishi nchi ya mbali sana, jina lake lilikuwa Stive D. Akakaa, akakaaa, akakaaaa, akakaaaaaaa weeeeeee, mwisho akahamia nchi za ughaibuni, akabadilisha na jina akajiita Stive Dii.Katika nchi ile aliyo hamia kulikuwa na Bint Mfalme aliyejulikana kwa jina la AshaD, Bint aliyekuwa mrembo jamali na mwenye kuvutia kwa kila hali, mwenye shingo ya upanga alikuwa aking'aa kama mbalamwezi.Basi siku moja akatoka kwenda kutembea, akakutana na mtoto wa Mfalme aliye hamia nchini mwao. Akamuuluza je waitwa nani wewe kijana jamali mwenye kuvutia kama kama jua la asubuhi. Yule mtoto wa mfalme akamwitikia kwa kumwambia, uko kwetu nilikuwa naitwa StiveD, ila kwenye nchi hii ya kuvutia, nimehamua kujiita StiveDii, ili nisijione mgeni na kuondoa upweke nilio nao.Basi Bint mfalme naye kwa kupendezeshwa na jina lile, na kwa kumuonea huruma na ili kumuondoa upweke, akaamrisha kuanzia siku ile naye asiitwe tena AshaD, bali aitwe AshaDii, ili afanane na mwana mfalme aliyekuja toka nchi ya mbali...! Kuanzia siku ile majina yao yakawa yanaishia na Dii, yaani StiveDii na Asha Dii...!Basi kwa leo tuishie hapo, Je Bint Mfalme na Mwana mfalme wataishia wapi?Hadith inaendelea na usikose wiki ijao...!Ni mimi uncle wenu, Uncle Bob XP, nikiwaageni, kwaherini, bai bai.