Kipande nilichokiwekea rangi nyekundu kinaonesha wazi, mambo hayajaisha na kuna mtego umewekwa. Unless mleta mada awe kachakachuwa maana anaonesha si mtu wa kuaminika.
Ni mtazamo objectively na si ushabiki:
Hoa jamaa watatu ni nouma hata Jah Kaya anawajua, ukianzia na:John Mnyika, Tundu Lissu, Joshua Nassari...every person at CHADEMA;
YOU ARE THE STRONGEST EVER...
Ninavyoona either mleta habari hajaiweka habari kama ilivyotolewa na spika au spika mwenyewe amechanganya mambo.
Kama kweli Spika amesema kamati "ilishindwa kuwahoji" wahutuhumiwa alikuwa anamaanisha nini?
Alikuwa anamaanisha kuwa kamati iliwaita lakini hawakujitokeza kuhojiwa au kamati haikuwaita kabisa kuwahoji?
Kama kamati iliwaita kuwahoji lakini wakakataa, basi ingeweza kufanya uamuzi wao on that basis.
Lakini kama kamati ilifanya maamuzi kabla ya kuwapa watuhumiwa nafasi ya kusikilizwa basi hiyo ripoti yao ni batili.
Lakini kilichonishangaza sana ni madai ya Spika kusema kusema kuwa watuhumiwa hawatachukuliwa hatua mpaka kwanza wahojiwe.
Kwa maana nyingine adhabu yao tayari imeshaandaliwa, kinachosubiriwa na wao tuu kuhojiwa ili waadhibiwe fasta.
Ndivyo nilivyoelewa.
Mambo mengine haibu tpu! Hawa wazee na mvi zao watoaje hukumu bila kuhoji watuhumiwa? Hizi kamati na tume viini macho tu! Shame on them!
sasa walihukumuje bila kuwahoji watuhumiwa?
Utawasikia magamba wakiongozwa na JK kuwa nchi hii inaongozwa na utawala wa sheria....Sheria in my A.S.S
Iweje utawala wa sheria huku kamati ya Bunge inatoa hukumu bila kumsikilza mtuhumiwa? SISIEMU wanaita huu utawala wa sheria..lol.
Mungu ni mwema sana!
Mh.Haasani Ngwilizi, mchana huu amewasilisha bungeni ripoti yake ya uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea bungeni wakati mh.Mnyika alipowasilisha hoja yake.Ripoti hiyo imewatia hatiani mh.Mnyika,Nassari na mh.Tundu Lissu.Ripoti hiyo pia inaonyesha waheshimiwa hao walikiuka kanuni na hivyo walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu.Ripoti hiyo imeonyesha kuwa kiti kilitenda haki na hata mh.Waziri wa maji hakukiuka kanuni yoyote alipochangia hoja ya mh.Mnyika kama alivyodai mh.Tundu Lissu.
Hata hivyo,mh.Spika amesema kuwa wahusika hawataweza kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu kwa sasa kwasababu kamati ya mh.Ngwilizi haikuwahoji wahusika kupata maelezo yao.Mh spika alidai kamati hiyo ilishindwa kuwahoji na hivyo mpaka watakapohojiwa ndio adhabu itatolewa kwa wahusika.
Swali,je ni kweli kamati ya mh.Ngwilizi ilishindwa kuwahoji au wanajua wangeumbuka?
Inawezekana hatua ya katibu mkuu wa CHADEMA,mh.Dr.Slaa, kuwataka wabunge hao wasikubali kuhojiwa ndio sababu?Mbona hakutaja sababu hiyo?
Kulikuwa na umuhimu gani wa kuisoma ripoti hiyo bungeni huku ikiwa haijakamilika?
Tafakari!