"Natural Justice" yawabeba Mnyika,Lissu na Nassari

"Natural Justice" yawabeba Mnyika,Lissu na Nassari

Kamati yenyewe imeshindwa kutenda haki kwa ku"absolve" kiti cha spika wakati kila mtu aliyetazama TV aliona jinsi gani spika au naibu spika walivyovunja kanuni. Utaratibu huu wa 'to make the guilty innocent and the innocent guilty' utatuletea matatizo Tanzania.

Pia hawajawaona wabunge wengine wa ccm walioongea lugha chafu bungeni? Kama dr. kitumbua alimsema Lissu maneno machafu na kudhalilisha au ndo kuku kanya akinya bata kaharisha?
 
Tanzania nchi yangu iliyokuwa ikitambulika kama kisiwa cha Amani. Magamba mnatupeleka wapi? Hv kweli mna uchungu kweli na sisi watanzania wenzenu,
 
Duh!!!

Daima mwenye akili ndogo kuongoza mwenye akili kubwa ni taaabu kweli kweli! Hivi kulikuwa na haraka gani ya kusoma hiyo taarifa wakati kamati haijafanya kazi??? Nilicho kuwa nafahamu ni kwamba, kulikuwa na tuhuma za uvunjwaji wa taratibu za bunge, kazi kubwa ilikuwa ni kuhoji watuhumiwa. Sasa iweje kamati ilishindwa kuhoji watuhumiwa, halafu itoke na majibu kwamba watuhumiwa walikuwa na makosa!!!!???

LIKE FATHER LIKE SONS!!!!

hii awamu ya nne mambo yake yanaenda kizuzu zaidi sheria zipo wanashindwa kuzisimamia na kubaki kukilalamikia chama kimoja tu ambacho ni makini ktk kufanya mambo yake. Badala ya kushindana nao kwa hoja wamekuwa wakitumia nyadhifa zao ktk kuwakandamiza na ktk kuyafanya hayo wao ndo udhaifu wao unazidi kuonekana tizama nchi ilivyo sasa uwezikuamini kama kuna rais
 
Ngwilizi 100 ndio nusu ya ufahamu wa T.Lissu,jeuri ya kuwahoji wanaitoa wapi?

Pia wanahanya kwani wanajua umakini wao na ujuaji wa sheria hawataweza kushindana nao. Ushauri wa bure kwa magamba if you can't fight them join them na siyo kung'ang'ani jiwe kuwa mkate
 
Kesi ya nyani kapelekewa ngedere unategemea nini?
 
Mh.Haasani Ngwilizi, mchana huu amewasilisha bungeni ripoti yake ya uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea bungeni wakati mh.Mnyika alipowasilisha hoja yake.Ripoti hiyo imewatia hatiani mh.Mnyika,Nassari na mh.Tundu Lissu.Ripoti hiyo pia inaonyesha waheshimiwa hao walikiuka kanuni na hivyo walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu.Ripoti hiyo imeonyesha kuwa kiti kilitenda haki na hata mh.Waziri wa maji hakukiuka kanuni yoyote alipochangia hoja ya mh.Mnyika kama alivyodai mh.Tundu Lissu.

Hata hivyo,mh.Spika amesema kuwa wahusika hawataweza kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu kwa sasa kwasababu kamati ya mh.Ngwilizi haikuwahoji wahusika kupata maelezo yao.Mh spika alidai kamati hiyo ilishindwa kuwahoji na hivyo mpaka watakapohojiwa ndio adhabu itatolewa kwa wahusika.

Swali,je ni kweli kamati ya mh.Ngwilizi ilishindwa kuwahoji au wanajua wangeumbuka?

Inawezekana hatua ya katibu mkuu wa CHADEMA,mh.Dr.Slaa, kuwataka wabunge hao wasikubali kuhojiwa ndio sababu?Mbona hakutaja sababu hiyo?

Kulikuwa na umuhimu gani wa kuisoma ripoti hiyo bungeni huku ikiwa haijakamilika?

Tafakari!

Taarifa za kiintelijensia zilizonifikia zinadai kuwa kutohojiwa kwa wabunge hao kulipangwa na kuratibiwa na Lukuvi pamoja na spka ili adhabu isitolewe kwa mda huu ambao watu wengi wanafuatilia sana sakata hili,cha kujiuliza kamati inapoamua kuwasilisha ripoti inakuwa imekamilisha kukusanya taarifa zote na kama walikuwa hawajawahoji ni dhahili kamati ilikuwa haijakamilisha uchunguzi wake kwanini iamue kuwasilisha ripoti nusu badala ya kuomba kuongezewa mda? Je,wakihojiwa kamati inaaminije kuwa yale waloyapata yanatosha kuwatia hatiani hata kama watakuwa na sababu zinazoonesha kuwa udhaifu umetokea sehemu nyingine? Nadhani kamati zinazoundwa hazipewi hadidu za rejea bali wanapewa kazi ya ku-compile tu data zipo tayari hakuna kingine!
 
Mapokezi ya wabunge wa upinzani Dar ni lini ili nilengeshe hapo safari yangu! Kichwa cha habari kimeniingiza chaka wakuu msaada tutani "Yawabeba Mnyika, Tundu na dogo janja"
 
ripoti imewaumbua vibaya haya waliokuwa na viherehere oohh sijui nguvu ya umma kiko waapiii:target:
 
Huo ni mtazamo wangu, ukipenda pokea ukipenda uwache, wala si kitu cha kubishana.

Sikujuwa kama siku hizi mnaletwa barua kutoka mbinguni. Una udugu na "babu" wa kikombe?

Bahati mbaya hapa huna wa kujiegemeza kwake kama kule kwingine.

Kamati iliyokwisha toa hukumu itawahoji ili iweje?
 
ripoti imewaumbua vibaya haya waliokuwa na viherehere oohh sijui nguvu ya umma kiko waapiii:target:

Na ndiyo maana walinywea kutoa maamuzi, wakijuwa kwamba nguvu ya umma itasimama na wapigania maslahi ya waTanganyika. Upo??
 
Kilichonifurahisha ni baada ya Ngwilizi alivyoaanza kusoma ile taarifa, Lissu akamuita Mnyika, baadae Mch. Msigwa, na jamaa walivyokaa wakielekeza macho mbele kwa umakini ilikuwa kama wansubiri golikipa ateme mpira wa penaliti ili wao wafunge goli. Nadhani huenda hukumu ilikuwa imeshaandaliwa, nikikumbuka maneno ya Anduje Ndugai. kama kuna siku Makinda amecheza basi alivyotumia kigezo cha natural justice na kusalimu amri basi yameisha vinginevyo naamini moto ambao ungewaka pale mtoto wa mkulima leo asingeahirisha bunge
 
Hapo wamewekewa bonge la mtego. Kalagabaho.

Ni very simple, wanapelekewa barua rasmi ya kuitwa kwenye kamati tajwa kama hawajafika wanakumbushwa kama hawajafika tena wanakuwa na makosa mengine zaidi ya hilo la fujo. Hapo walipowekwa hawachomoki, salama yao wakiitwa rasmi kwenye kamati waende.

Mheshimiwa zomba masaburi ya kichina kufikiri.
 
Spika na ****** wana akili kama za shetani and soon watakuwa wachawi kama Mwigulu
 
Magamba balaa, hapo yametumia pesa za walipa kodi kwa kakamati kasikojua cha kufanya. Ni heri wasinge soma hio report yao.
 
Hapo wamewekewa bonge la mtego. Kalagabaho.

Ni very simple, wanapelekewa barua rasmi ya kuitwa kwenye kamati tajwa kama hawajafika wanakumbushwa kama hawajafika tena wanakuwa na makosa mengine zaidi ya hilo la fujo. Hapo walipowekwa hawachomoki, salama yao wakiitwa rasmi kwenye kamati waende.

Kweli mkuu hili ni bonge la mtego si tu kwa wabunge watakaohojiwa bali hata kwa kamati yenyewe,kamati ingeomba kuongezewa mda ili iwahoji kwanza ndiyo wawasilishe lakini ripoti imewasilishwa tayari bungeni kabla hawajahojiwa wahusika,wataadhibiwa lakini zitakuwa tayari ni dalili mbaya kwa kamati ya maadili ya kutojua wajibu wake na kupoteza uhalali wake pia.
 
Kweli mkuu hili ni bonge la mtego si tu kwa wabunge watakaohojiwa bali hata kwa kamati yenyewe,kamati ingeomba kuongezewa mda ili iwahoji kwanza ndiyo wawasilishe lakini ripoti imewasilishwa tayari bungeni kabla hawajahojiwa wahusika,wataadhibiwa lakini zitakuwa tayari ni dalili mbaya kwa kamati ya maadili ya kutojua wajibu wake na kupoteza uhalali wake pia.

Hapana, hawajakosea. Bunge ni dynamic na si stagnant.
 
Back
Top Bottom