Nateseka na ndoto

Delegate

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
331
201
Naombeni msaada.

Usiku nikilala natembelewa na watu nisiowajua,yaani kila siku kuna watu wanakuja chumbani kwangu halafu tunakaa na kuongea,wakiondoka tu na mimi naamka mara nyingi inakuwa mida ya saa tisa usiku,nikiangalia milango yote imefungwa najaribu kuangalia kama kuna mtu pale ndani lakini hakuna kitu,naombeni msaada jamani hili jambo linanisumbua sana
 
Kuomba sana na kubadirisha muda wa kulala,tafuta kitu cha kufanya usiku cha kufurahisha ,kuupooza akili yako
 
Kama wewe ni mkristo kamuone mchungaji/padri, kama ni muslim kamuone sheikh na kama ni mpagani kamuone mganga. Zaidi ya hapo sina cha kukuambia.
 
yahh ni dalili ya kua na mapepo na minguvu ya giza,sali kabla ya kulala,ukiwa karibu na mungu hakuna kiumbe /kisichokua kiumbe kibaya kitakachoweza kukukaribia
 
Pole mkuu. jitahidi uwe unasali kabla ya kulala na ukiweza fungua zile redio za dini kwa sauti ndogo ukeshe nazo.
 
Pole sana kwa hili, kazana kuomba hata kama watakuwa wameondoka, inuka na piga maombi usali. kama wewe ni mkristo basi kumbuka kuweka biblia chini ya pillow yako.
 
Kula pombe ndo ulale hao ni wachawi wanakuletea offer ya kuingia kwenye contract ya kuloga so Hang'over na uchawi haviendani watakupotezea.Nipo serious kaka.
 
Delegate: hujatuambia mnaongea nini na hao wanao kutembelea?
na hao watu ni wa Haina gani (ke/Me), na wanakuja kwa taswira ya ubaya au uzuri?
ukijibu ili utawapa wadau uwanja mpana wa kukusaidia! pia wewe unaintaract na watu wa Haina gani?
katika Swahili neno "KUTEMBELEWA" some time inabeba -ve connotation, wewe yako ni ipi?
pole sana!
 
Delegate: hujatuambia mnaongea nini na hao wanao kutembelea?
na hao watu ni wa Haina gani (ke/Me), na wanakuja kwa taswira ya ubaya au uzuri?
ukijibu ili utawapa wadau uwanja mpana wa kukusaidia! pia wewe unaintaract na watu wa Haina gani?
katika Swahili neno "KUTEMBELEWA" some time inabeba -ve connotation, wewe yako ni ipi?
pole sana!

Mkuu umeuliza mambo muhimu'mimi ni mwanaume wa 39yrs'mimi ni single na mara nyingi sana nalala peke yangu'wanaokuja nashindwa kujua kama ni wanaume au wanawake lakini kuna kipindi wanakuja wawili'watatu au mmoja'
Mkuu kuna wakati nawaza labda ni baadhi ya wanawake ninaokutana nao mara kwa mara'ninaamini hawatanidhuru lakini hili jambo linaninyima usingizi'ila nikilala na demu hawaji kabisa
 
Pole mkuu. jitahidi uwe unasali kabla ya kulala na ukiweza fungua zile redio za dini kwa sauti ndogo ukeshe nazo.

Hazitakusaidia redia hizo, hata kama ukilalia Biblia usiku, kwani wanafuata roho yako sio radio wala Biblia ila, ukimpokea Kristo hautaweza kulala kwa hofu. Kwani kulala na radio au Biblia ni kumchezea Mungu, ni sawa na kwenda BAA ukakutana na mrembo kumbe ni jini alafu ukapiga kelele ya kumuomba Mungu akisaidie, hawezi kukusaidia kwani mawazo yako awali yalikuwa ni dhambi.
 
Nenda kwa mzee wa upako ubungo kibangu ,hata kama ww ni muslim au tafuta mlokole wanayatimua faster!
 
Piga magoti muombe Mungu kwa IMANI akufunulie. Akusaidie kupambanua mambo hayo, kumbuka kutubu dhambi zako. Ukiwa na IMANI hakuna lisilowezekana kwa Mungu.
 
Jiombee kwa imani yako, wakemee na ujitenge nao. Funga kwa siku hata 2 na uweke alarm uamke saa nane na kusali. Wakija wakikukuta unasali wataishia zao
 
Au mafreemason wanakutembelea. Sa tisa ndio mida yao. Sali kabla ya kulala. Ukistuka usiku sali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom