Mungu uongea na binadamu kupitia njia hizi hapa

Mungu uongea na binadamu kupitia njia hizi hapa

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
996
Maeneo ambayo Mungu anaweza Kuzungumza na wewe.

Mungu anaweza kuongea na binadamu kupitia ishara mbalimbali na unapoelewa basi unakuwa umesikia sauti ya Mungu.

1. Kupitia ndoto, Hii ni njia kubwa ambayo Mungu utumia kuongea na wanadamu,

Mungu anatumia ndoto kutoa ufunuo wa maisha ya wanadamu, ndoto sio jambo la kisayansi tu ni jambo la kiroho,

Kupitia bibilia Mungu alitumia ndoto kuongea na mitume na manabii kuweza kutabiri, kuonya na kujua ni mambo gani wafanye wakati huo.

hapa malaika wa bwana walitumia ndoto kuzungumza na Yusufu kuhusu kuzaliwa kwa bwana yesu.

Mathayo 1:20
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Mathayo 2:12
Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

2. Kupitia Akili(Mind) au Mawazo, Muda mwengine Mungu anaweza kuzungumza na wewe kupitia mawazo.

Mfano unaweza pata wazo mpigie fulani na kweli unapigia na kuongea naye unakuta anashida na anaitaji msaada wako wa kifedha au mawazo hii ni Mungu anaongea na wewe ili uweze kutoa msaada kwa mwengine.

3. Upitia watu, Mungu anaweza ongea na wewe kupitia watu wengine,

Mfano wewe ujioni huna kibaji fulani lakini kila mtu unayekutana naye anakuambia wewe una faa kuwa sehemu fulani mfano watu wanaweza kukuona kama kiongozi, mfanyabiashara, tajiri, nabii, mbunifu nk

Kile watu wanachosema mara kwa mara katika namna chanya hiyo ni Mungu anaongea na wewe kupitia kwa wengine anataka uchukue hatua kwenye hivyo vibaji watu wanavyoona kwenye maisha yako.

4. Kupitia changamoto, Muda mwengine Mungu anataka uone ukuu wake au uwepo wake kwenye maisha yako kupitia changamoto.

kuna nyakati Mungu anaweza kukupitisha kwenye changamoto ambazo akuna wa kukusaidia na unapata msaada kwa namna ambayo wewe mwenyewe unasema huyu ni Mungu tu ndiye aliyenisaidia .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom