baharia 1
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 3,016
- 4,404
Usibembelee Ndugu Washenzi na Wachawi, Kuna Muda Damu Inakuwa Sumu Epuka Kuilamba!
Wakuu, leo nataka tushushane pumzi na tuambizane ukweli mchungu unaochoma hadi mifupa, maana tumekuwa wajinga wa kutupa kisa tu neno udugu wa damu.
Acheni upumbav wa kufikiri kila mtu mwenye DNA moja na wewe anakuwazia mema, ukweli wa maisha ni kwamba udugu hautoi leseni ya kulealea washenzi, wanafiki, washirikina, na wachawi kwenye maisha yako.
Kuna ndugu kiasili wana roho za kwanini na roho za kwanini hazina dawa, wanakuja kwako wanalia shida kumbe wanakuja kukuchungulia mianya yako ya mafanikio, na ukweli uliopo ni kwamba ukimpa mtu msaada badala ya kuutumia kujikwamua, anautumia kwenda kwa waganga wa kienyeji kusafisha nyota yake na kutafuta ushirikina wa kukurudisha wewe nyuma ili mlingane umaskini.
Hapa nyumbani kwetu kuna mfano hai na wa kweli unaouma sana moyoni, mzee wangu alikuwa na roho ya kipekee sana, akawa anajinyima na kuleta watoto wawili wa ndugu zake kutoka huko kijijini waje hapa nyumbani ili kuwasaidia, akawasomesha, akawalisha, akawasitiri uchi wao, na kuwafanya kama watoto wake wa kuwazaa akiamini anajenga familia na kusaidia damu yake.
Ukweli mchungu ni kwamba wale watoto wawili baada ya kufanikiwa na kupata mianya ya maisha mjini, leo hii ndio wamekuwa maadui namba moja wa familia yetu, wamekuwa washenzi wa kutupwa, wanafiki wakubwa, na mbaya zaidi wamebobea kwenye mambo ya ushirikina na uchawi wakihangaika usiku na mchana kwenda kwa waganga ili tu kuona mzee wangu anafilisika na sisi watoto wake wa damu tunafeli maisha.
Huu ni ujumbe mzito kwa kila mtu anayejifanya mwokozi wa ukoo, ukitaka kuishi kwa amani na kulinda akili yako, kata misaada kwa ndugu washenzi mara moja na ufunge milango yako usiku wa manane bila kugeuka nyuma.
Huwezi kamwe kubadili vinasaba vya msaliti au mshirikina kwa kutumia fadhila na upendo, na ni bora uonekane una roho mbaya na mchoyo mbele ya ukoo mzima ukiwa na amani na mafanikio yako, kuliko kuwa mwema anayelelea wachawi huku unajipalilia mkaa wa moto wa kukuteketeza wewe na kesho yako.
V NIMEMALIZA