Nateseka na ndoto

muombe sana mungu atakusaidia.pia nenda kanisani kwa mchungaji akuombee.kwa ushauri zaidi ni kanisa gani uende nipm nitakuelekeza,
 
Ndoto zako hata hukumbuki mnaongei nini. Anza kwa ktumia B Complex ili uweze kukumbuka mnacho ongea na baada ya kuweza kukumbuka ndoto zako nenda ukawaone shrinks hapo Muhimbili. Hilo ni tatizo dogo sana. Lisikutoe jasho.
 
weka maji ya baraka,biblia,na sali kabla hujalala
siajasahau hata mfupa wa kitimotooooooooooozzzz
ni dawa ya kutimua majini..kama ww ni ati mislamu swali funua aya za mtume acha qurani wazi pale uliposoma
 
Ee bwana Mungu,wasaidie wale wote wanaopata mateso aina zote wawapo usingizini,na uwaepushie kero hizo! Amin.
 
Kama wewe ni Mkristo sali kabla ya kulala na soma fungu lolote katika Biblia. Pia kumbuka kulala na Biblia karibu hasa Kitandani itakusaidia sana. Yaani kitendo tu cha Kuamini neno la Mungu kwa kulisoma, kuomba na kulala karibu nacho ni hatua kubwa sana kiimani na itakusaidia.

Sisi kama Wakristo tumepewa mamlaka kuomba lolote tulitakalo kwa Mungu naye amehaidi kutupatia kile tumwombacho. Naomba usiwe na mawazo mengi sana sijui mpaka uombewe na fulani ndiyo upone, kwanza hilo ni upungufu wa Imani kwako. Ni kwanini mtu fulani ndiyo akuombee wkt Mungu wako amekupa uhuru wa Kusoma neno lake na Kufanya maombi? ingekuwa habari ya Kanisani, sawa lazima huyo Mchungaji angeomba kwa niaba yako. Tafadhali simama kwa miguu yako na Mwite Mungu naye atakuitikia. Kumbuka kutubu kwanza na kumshukuru Mungu kwa ulinzi na mibaraka yake kwako, then mwambie Mungu akulinde naye atakupa ulinzi wake kwa njia ya Malaika zake na Roho Mtakatifu.

Ndugu yangu ninachokuambia ni hakika;
kuna kijana mmoja wkt nasoma A-level shule fulani; alikuwa na kawaida ya kuota ndoto za ajabu hadi akafikia hatua ya kuhama hata chumba lkn vyote hivyo havikumsaidia, kwani ndiyo alizidi kuota na kushindwa kupata Usingizi kabisa na hatimaye alikuwa na hofu sana hata wkt wa Mchana. Nilimwambia kwamba, ondoa hofu then amini kwamba Yesu anaweza yote. Nikamwambia akasome Biblia(hakuwa na Biblia, hivyo alienda kuazima) na kusali, then alale na ile Biblia karibu. Hakuweza kuona tatizo tena mpaka leo ni mtu mkubwa tu anafundisha DIT.

Mungu na akutie nguvu na kukulinda dhidi ya hayo matatizo yanayokusumbua. AMINI NA MUNGU ATAKUSHINDIA.
 
Pole sana kwa hili, kazana kuomba hata kama watakuwa wameondoka, inuka na piga maombi usali. kama wewe ni mkristo basi kumbuka kuweka biblia chini ya pillow yako.
Mkuu biblia sio hirizi, kuweka tu mchagoni haisaidii, chini ya pillow atachana karatasi bure tu, atafute mtu makini anayemjua Mungu afanye maombi hapo home kwake, kwisha kazi. Ishu ndogo sana hiyo.
 
kulala peke yako nako sio vzuri. Chukua ndito moja au ile inakuja kuja hapo oa! Tatizo nadhan litaisha. C umesema ukiingiza ndito wazee wa kaz hawaji?
 
Kitu kama hii maana yake ni tatizo,na tatizo huwezi kulielezea ki-summary summary,jaribu kuelezea kiundani zaidi ili solution utakayopata hapa iwe deeper than the problem,JF huwezi kukosa solution,trust me on this one.
 
Kula pombe ndo ulale hao ni wachawi wanakuletea offer ya kuingia kwenye contract ya kuloga so Hang'over na uchawi haviendani watakupotezea.Nipo serious kaka.

hii ni kweli nimeiexperience kwa muda mrefu sasa.
 
Hakuna cha pole kwani ameumizwa?Inakubidi umtafute baba na mama yako kama wapo.alafu wao ndio uwaeleze.ukimaliza kwa wazazi ndio uangalie watakuambia ufanye nn.kama kw padri.shehe.au mganga.kama wote hawapo nenda kwenu.unaijua asili yako?Au unaishi kizungu?Kama unnaishi kizungu mjomba kazi unayo.waafrica tunamambo mengi sana.But don 4get dady and mumy its second god under tha sun.in god.................
 
Unachohitaji ni kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Mbona hao watu ni cha mtoto kwake!! Tembelea kanisa lillilo karibu nawe waeleze na watakufanyia maombi na kukueleza ufanye nini ili uwe na silaha. Kwa kifupi tubu dhambi zako uwe safi mbele za Mungu. Pia soma Waefeso 6:10 - 18 utazijua silaha zote unazohitaji kushinda vita hivyo. Hivyo ni vita vya kiroho. Hayo unayoyaona yametokea katika ulimwengu wa kiroho. Kuyashinda unatakiwa uwe imara kiroho. Kwa kifupi okoka na uwe na hizo silaha zote utakazozisoma katika Waefeso 6:10.
naombeni msaada
usiku nikilala natembelewa na watu nisiowajua,yaani kila siku kuna watu wanakuja chumbani kwangu halafu tunakaa na kuongea,wakiondoka tu na mimi naamka mara nyingi inakuwa mida ya saa tisa usiku,nikiangalia milango yote imefungwa najaribu kuangalia kama kuna mtu pale ndani lakini hakuna kitu,naombeni msaada jamani hili jambo linanisumbua sana
 
Kuweka biblia chini ya mto haisaidii kama wewe mwenyewe huna Yesu. Kama huna Yesu biblia inakuwa ni kitabu tu kama vitabu vingine. Cha msingi ni biblia iwe moyoni mwako na uishi kama neno la Mungu linavyoagiza.
Pole sana kwa hili, kazana kuomba hata kama watakuwa wameondoka, inuka na piga maombi usali. kama wewe ni mkristo basi kumbuka kuweka biblia chini ya pillow yako.
 
Delegate unayakaribisha haya yote kwa style yako ya maisha. Umesema wewe ni single na unlala na demu. Hao uanaolala nao si wazuri. Achana na hiyo tabia mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Watakimbia hao!! Ishi maisha ya kitakatifu. Yesu alituasa tuwe watakatifu maana yeye ni mtakatifu.
Mkuu umeuliza mambo muhimu'mimi ni mwanaume wa 39yrs'mimi ni single na mara nyingi sana nalala peke yangu'wanaokuja nashindwa kujua kama ni wanaume au wanawake lakini kuna kipindi wanakuja wawili'watatu au mmoja'
Mkuu kuna wakati nawaza labda ni baadhi ya wanawake ninaokutana nao mara kwa mara'ninaamini hawatanidhuru lakini hili jambo linaninyima usingizi'ila nikilala na demu hawaji kabisa
 
Ajiombee kwa imani yake ipi? Hakuna imani itamsaidia delegate isipokuwa Kristo Yesu. Delegate tubu dhambi zako zote na uvae silaha zote za Mungu nilizokutajia hapo juu. Utaniambia matokeo. Wakati mwingine kuombewa sio kitu kizuri kwani ukiachana na aliyekuombea unarudi kulekule. Jiombee mwenyewe. Tafuta kitabu cha Mgisa Mtebe kinaitwa Jifunze namna ya Kuomba. Kitakusaidia sana ukifuata utakayoyasoma. Kinauzwa elfu tano tu. Usikose kusoma Waefeso 6:10 -18.
Jiombee kwa imani yako, wakemee na ujitenge nao. Funga kwa siku hata 2 na uweke alarm uamke saa nane na kusali. Wakija wakikukuta unasali wataishia zao
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom