Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

Hongera kwa uwamuzi na jitahidi sana kuepukana na vishawishi vya kurudia ambayo sio kazi rahisi lakini ukifanikiwa utaona tofauti kubwa katima maisha yako
 
Nyau wewe usichanganye kama unakunywa bia usiweke kiroba. kula ushibe kwanza sikushauri ule kiroba
 
Uamuzi sahihi , Mimi niliacha Pombe Tarehe 01. January 1986 kwa uchungu mkubwa baada ya kulewa na kubebwa kurudishwa nyumbani ktk Christmass ya 1985. Nilitafakari sana hiyo Hali na ilipofika 31 desember nikafikia 'UAMUZI' kwamba nitavishinda vishawishi Vyote isipokua Kifo ! Hivyo ninaamini hata wewe Wawezeshaji kufanikiwa kama Mimi kwani hadi leo sijanywa Tena pombe .
 
MUNGU akakuwezeshe. KAZI sana kuacha pombe kwa juhudi zako MWENYEWE, bila msaada wa MUNGU. Shetani wa TBL kishashusha bei ya SafAri LARGER na Kilimanjaro Premium LARGE. Jini Serengeti nalo limeshushwa bei. Heineken na Windhoek nazo ni 2500/-
bar gan windhoek ni 2500
 
Habari za Jumapili wakubwa?

Leo natangaza rasmi kuachana na pombe, maana nimeshindwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala. Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.

Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani, sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyoni bia zitanitambua, nilivyofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha alafu nikashushia na mzinga wa konyagi ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya.

Sasa wakati wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhani nae alikua tungi, mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashindana nae kukata mauno, ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.

So kwa utashi wangu, nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu, nimeamua kuacha pombe rasmi.
Sasa mkuu kama ulishangiliwa kwa kucheza na huyo dada mbona fresh. Sherehe ni furaha, mi nilijua ulianzisha ugomvi. Endelea tu mkuu.
 
Nilisha jaribu kuacha pombe kama mara 2 mara ya kwanza nilikaa kama miez 7 nikarudia kwa kasi badae nikaacha kwa kama mwaka nikarudia tena kwa kasi kubwa ila baada ya kupata majanga ya ajali ya gari yani nilipiga tungi nikawaambia washkaji naenda moshi kumsalimia mama wakaniambia hyo safari ulipanga nikawaambia hamna nimeamua tu sasa hv..aisee nikaamsha gari saa 4 usiku huo mzinga niliokula sikuamini kama nilitoka...leo 5yrs sijagusa pombe ila kanisani sikosi misa ya kwanza kuomba pombe ipite mbali na mm maana nimepoteza fedha nyingi sana kwa mambo niliyoyafanya wkt nikiwa nimelewa staki kurudi kwenye hayo ma addiction
Kwa huu ujasir kajioongeze na bia 2
 
iache tu kabisa huiwezi

usije kuwa mwenzako, katoka atokako kafika traffic lights za Namanga kashuka kwenye gari kasogea pembeni kususu, kamaliza kususu kasimamisha Taxi na kuondoka, kasahau kama alikuwa anaendesha
 
Habari za Jumapili wakubwa?

Leo natangaza rasmi kuachana na pombe, maana nimeshindwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala. Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.

Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani, sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyoni bia zitanitambua, nilivyofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha alafu nikashushia na mzinga wa konyagi ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya.

Sasa wakati wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhani nae alikua tungi, mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashindana nae kukata mauno, ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.

So kwa utashi wangu, nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu, nimeamua kuacha pombe rasmi.
umenishtua....nikajua labda ulivua nguo hadharani hapo kwenye sherehe !!! kumbe ni kukata miuno tu... nenda kanywe soup utoe hangover halafu kesho nitafute nikuongeze bapa lingine
 
Mkuu na wale mende waliokuwamo kwenye sherehe walikuacha ivi ivi kweli au hilo unaliweka kama siri yako ya ww kuachana na kinywaji!
 
Habari za Jumapili wakubwa?

Leo natangaza rasmi kuachana na pombe, maana nimeshindwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala. Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.

Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani, sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyoni bia zitanitambua, nilivyofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha alafu nikashushia na mzinga wa konyagi ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya.

Sasa wakati wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhani nae alikua tungi, mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashindana nae kukata mauno, ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.

So kwa utashi wangu, nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu, nimeamua kuacha pombe rasmi.
Mrejesho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom