Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
12,073
Reaction score
16,638
Habari za Jumapili wakubwa?

Leo natangaza rasmi kuachana na pombe, maana nimeshindwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala. Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.

Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani, sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyoni bia zitanitambua, nilivyofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha alafu nikashushia na mzinga wa konyagi ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya.

Sasa wakati wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhani nae alikua tungi, mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashindana nae kukata mauno, ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.

So kwa utashi wangu, nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu, nimeamua kuacha pombe rasmi.
 
hahahaaaaa,sasa wewe ulijuaje wakati unasema ulilewa,ulisimuliwa vituko ulivyofanya au uliangalia cd ya harusi?
 
Punguza sikushauri kuacha kabisaa,maana unaweza angukia ulevi mwingine kama kuvuta shisha.
 
Nimecheka sana aisee hahahahahaha lol! Umenikumbusha harusi moja nilialikwa na jamaa zangu pale Diamond Jubilee. Sasa katika harusi ile vinywaji vyote ikiwemo kilevi vilikuwa ni self service pumzi yako, na baadhi wakakamia kutaka kuonyeshana nani ana pumzi ya kunywa kilevi. Pombe za kawaida za nchini na nchi za nje na pombe kali za kila aina. Jamaa yangu mmoja kaamua kufakamia pombe kali mara yuko na whisky mara kahamia kwenye nyagi na dancing floor anazuka mara kwa mara na hiyo cheza yake baada ya kukamata masanga mie sina mbavu.

Ghafla bin vu jamaa anadai anasikia joto kupita kiasi hivyo anaenda nje kupata upepo kasha atarudi. Baada ya muda hatumuoni tukaenda kumtafuta huku na kule hatimaye tukamkuta kavua shati, kavua viatu na soksi kaingia chini ya uvungu wa gari maana mwanga wa mataa ulikuwa unamsumbua sana hivyo akatafuta giza giza uvunguni mwa gari.

Tukamtoa baada ya muda akaanza kutapika mpaka tukaogopa anaweza kufa maana ilikuwa si kutapika kwa kawaida. Ikabidi tumrudishe home, lakini alikuwa na bahati sana tulimuona vinginevyo kama mwenye gari asingemuoa basi siku ile angekutana na umauti wake pale uvunguni mwa gari. Chezea Pombe weye hasa ukizikamia.

Habari za jumapili wakubwa?
Leo natangaza rasmi kuachana na pombe,maana nimeshndwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala.
Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.
Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani,sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyon bia zitanitambua,nilivofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha afu nikashushia na mzinga wa konyagi..ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya,sasa wkt wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhan nae alikua tungi,mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashndana nae kukata mauno,ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani.kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.
So kwa utashi wangu,nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu,nimeamua kuacha pombe rasmi.
 
Miluacha pombe huwa hatangazi, inatakiwa maamuzi ya nafsi na kimyakimya. Nenda katoe lock!!!
 
we unazan kuacha ingekua rahisi kiivo dunia siingekua haina walevi kabisa

umepumzika kwa masaa tu,jioni jion lazima ukazimue moja
 
Habari za jumapili wakubwa?
Leo natangaza rasmi kuachana na pombe,maana nimeshndwa kuitawala na badala yake yenyewe ndio inanitawala.
Kumekua na matukio mengi ya hovyo ambayo nimekua nikiyafanya pindi nikiwa nimelewa ila hili nililolifanya jana imenibidi tu niache pombe.
Jana nilikua na mwaliko kwenye harusi flani,sasa na kwa vile saivi usawa mgumu nikajisemea moyon bia zitanitambua,nilivofika ukumbini nikatandika ukawa za kutosha afu nikashushia na mzinga wa konyagi..ebana after two hours nikawa niko tilalila mbaya,sasa wkt wa kucheza mziki ulivyowadia kuna mrembo mmoja nadhan nae alikua tungi,mtoto ana wezere ya kufa mtu ndo tukawa tunashndana nae kukata mauno,ukumbi mzima wakawa wanatushangilia kwa jinsi tulivyokua tunaruka kwanja yani.kwangu mimi hili ni jambo la aibu sana.
So kwa utashi wangu,nikiwa na akili timamu na pasipokushauriwa na mtu,nimeamua kuacha pombe rasmi.
Mkuu Kwa Mara moja si mbaya ila kama ndiyo tabia yako,hiyo ni mbaya sana,ila pia utakuwa umejiweka kando na mahaba ya wahudumu Wa bar na vyumba vya wageni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom