Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

Natangaza rasmi kuacha kunywa pombe

Pombe hatuachi Mkuu... uwa tunapumzika baada ya tukio la aibu. Hiyo hangover ikikata after 3 days utarejea tu.

Cha msingi kama mipombe iko mingi usichanganye na Nyagi.... nyagi mara nyingi pigia kwako.
 
Kiongozi vijana hawajakuvunjia yai kweli!?

Hivi siku zote hujui Castle light zilitengenezwa kwa ajili ya vichwa vya panzi kama wewe?
 
Acha tu hakuna namna [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hangover hiyo, umeamka nazo nenda kupata supu na chapati 2 na maji chupa kubwa ya kilimanjaro. Pumzika supu ishuke halafu kuanzia hapo mfuate kiongozi wa ibada wa eneo lako na umweleze azma yako ili ujenge network ya marafiki wapya wanaomcha Mungu.

Ukishindwa hapo, hakuna namna utarudia tu

Mimi sijaamua kuacha japo mama kanilisha mavitu fulani yanayonifanya nikinywa pombe nipate kichefuchefu sana hata bia moja napata tabu sana lakini bado nakomaa. Nakunywa mbili halafu natapika ile mbaya lakini bado nimo
 
Pombe mbaya sana, familia inawezashindia dagaa na maharage wiki nzima alimradi ww ukapate pesa ya kulewea.
 
Haya yote ni sababu ya Magufuli, mwaka huu wengi wameacha kunywa.
Siku nyingine utakuja hapa useme una acha kula mchana kuepuka kisukari.
 
huwezi acha kirahisi ivo, kesho kutwa njoo na story ulivua nguo, wanao achaga hawasemi ukisema ni kama umejipa laana, utarudi tu
 
Nadhiri ya kuacha pombe huwa haitangazi popote pale iwe kwa maandishi amamaneno, huwez kuacha pombe sababu ya tukio lolote baya lilikukuta ama lililomkuta mwenzako lililosababishwa na pombe. Mwisho huwezi kuacha pombe iti kisa huna pesa, unajidanganya!!!!!!
 
Hangover hiyo, umeamka nazo nenda kupata supu na chapati 2 na maji chupa kubwa ya kilimanjaro. Pumzika supu ishuke halafu kuanzia hapo mfuate kiongozi wa ibada wa eneo lako na umweleze azma yako ili ujenge network ya marafiki wapya wanaomcha Mungu.

Ukishindwa hapo, hakuna namna utarudia tu

Mimi sijaamua kuacha japo mama kanilisha mavitu fulani yanayonifanya nikinywa pombe nipate kichefuchefu sana hata bia moja napata tabu sana lakini bado nakomaa. Nakunywa mbili halafu natapika ile mbaya lakini bado nimo
Duh.. hiyo noma. Midawa gani hiyo??
 
Mara nyingi ukiamka na hangover au hasara ya ulevi wa jana, cha kwanza kukujia kichwani ni wazo la kuacha pombe. Nakushauri fanya maamuzi hayo baada ya week moja mbele. Ukiwa very sober!
 
usiache mkuu, serikali itakosa mapato-au hujui kodi kubwa inatokana na Bia nchi hii??
 
Hongera. Am sure umefanya uamuzi wa maana sana maishani. Umeushinda utumwa mkubwa kuliko utumwa wote maishani.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kumbe ndo ww jamaa !!!! usiache kabisa maana sio kwa miuno ile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom