Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Kuna vitu vya kuficha lakini sio mtoto.......


Anayeficha mtoto aliyemzaa kabla ya kuoa/kuolewa ana roho ngumu sana....
 
Katika maisha haya kilichoko ndani ya uwezo wa mwanadamu ni kujibadili yeye mwenyewe na hakuna mwenye uweza wa kum-badili mtu mwingine. Msimamo uliojiwekea ni tanzi yako mwenyewe ukiiondoa utakuwa huru; ina maana ukiokota mtoto yatima barabarani hutamlea?

si zaidi sana akiwa ni damu ya umpendae? na je kama mungu hajakupa kizazi uko tayari kuasili mtoto gani huyo wa mumeo au mtoto baki? hebu acheni mawazo ya kishetani;

ukweli ndio huo wewe songa mbele na mtu wako na mtoto lea fresh tu kuliko kusubiri ukose wa kukuoa uwe unadandia waume za watu au utachagua ambao hawajazaa na wake zao? Inawezekana hata labda sio kakuficha ila huenda nayeye hana uhakika kama mtoto ni wakwake au anabambikiwa
 
Pole.

Watu wengi wanaogopa kuwa huru na kusema ukweli kuwa wana watoto.

Sijui kwanini!
 
aiseee babayangu rudi kwa wazazi wako uwapigie magoti uwaombe radhi
 
Huyo bwana a nakupenda sana, na bila Shaka unapaswa kumshukuru mungu kwa kukupea mwanaume anaekupenda Kama huyo ulienae sasa.

Tukirudi kwa point ya kwanini haku kwambia mapema kama aliwahi kupata mtoto, kuna mengi ambayo hupelekea sisi wanaume kuficha baadhi ya mambo Kama hayo.

1- pengine alisingiziwa mimba au hakuwa na uhakika wa mimba ambayo Leo ni mtoto.
2- jamaa anakupenda kiasi cha kuona kwamba angekuambia mahusiano yenu yange yumba ama kubomoka, kitu ambacho hakupenda kitokee kukukosa.
3- yawezekana weni mkali sana hivyo ilimuwia ngumu kuanza kukuelezea kwa kuhofia ukali wako.
4- pengine jamaa alitendwa na hakutaka kujihusisha kabisa hata na mtoto na baada ya muda akapata huruma kama mzazi.

Nakushauri kama mzowefu wa mambo ya mahusiano kwamba, iwapo unaamini kwamba jamaa hana matatizo yatakayo kupelekea kuvunjika kwa mapendo yenu, ni vema ukae na mpenzi wako mlizungumzie hili na maisha pamoja na mipango iendelee.

Onyo: usije Fanya maamuzi pasipo hekima, na ukaja jikuta unakwepa tundu na unadumbukia shimoni.

Amen.....
 
Hapo pa kuwa mkali na kutishia kukuacha hapajakaa vizuri meaning hiyo ni one side love we ndo unampenda sana, ila issue ya kumkuta na mtoto si tatizo kama unampenda, tena bora umemkuta je angekukuta ww ungemuacha? Mtoto ni innocent
 
Kwani ana mke?...kama hana bas tatizo lake libaki kuficha tu huyo mtoto. Vinginevyo dont set too many criteria for the one to marry you. Usitumie akili yako peke yake kuamua nani atakuoa...let situational context decide for you, wewe baki kuona merits or drawbacks za opportunity hiyo. Not a joke, many who set criteria end in vain and illusions. Defae defacto..latin words, if you choose criteria for marriage which are expirable, then be ready to end in frustrations thereafter...
 
Kwani ana mke?...kama hana bas tatizo lake libaki kuficha tu huyo mtoto. Vinginevyo dont set too many criteria for the one to marry you. Usitumie akili yako peke yake kuamua nani atakuoa...let situational context decide for you,

wewe baki kuona merits or drawbacks za opportunity hiyo. Not a joke, many who set criteria end in vain and illusions. Defae defacto..latin words, if you choose criteria for marriage which are expirable, then be ready to end in frustrations thereafter...
 
pole sana dada kwa mazito yaliyo kufika.
Binafsi naona mwanaume kuwa na mtoto sio kosa kabisa ingawa inavumilika zaid kama umemkuta na huyo mtoto....
lakin sio apate mtoto ndan ya mahusiano yenu... mbaya zaid kaficha na anakua mkal ukiuliza...

af na wewe bado unataka ndoa.....
em kaa chin ufikir tena, unamuuliza anatishia kukuacha... mbaya sana hii atafanya kosa lingine utashindwa kumuuliza. ili ulinde

mahusiano...
unajiingiza katika ndoa ya kitumwa na ndo zina vunjikaga mapema hiz.
 
kiukweli kwa mipango yako angekwambia ukweli angekukosa na lengo lake ni kukupata
 
Hata ukiamua kuolewa naye jua tu kuwa mko wawili. Hata iwe kuwa huyo mzazi mwenzie kaolewa lakini bado ni wazazi.
 
Mimi nakushauri endelea na mpenzi wako.ukitaka mpenzi ambaye hawezi kufanya makosa yeyote katika hii dunia huwezi kumpata bintii.
 
Ulipomuuliza akawa mkali kisha akatishia kukuacha. Fungua akili.

Hapa kwakweli na mi naona asepe tu!
Coz ilitakiwa awe mkweli tu,sasa mambo ya kutishia kukuacha !!?so anaona we hupindui hapo!?
No!!anaekupenda hawezi kutishia kukuacha,believe mi!!
 
my dear unanihukumu bure...wala sijasema nachukia huyo mtoto.Ila unapokua muwazi kwa mwenzanko af ye akakuficha inauma esp.ukizingatia huyo mtoto kazaliwa ndani ya mahusiano yetu.Kama mtu anaficha hili nadhani nexttym ataficha kinda zaidi ya hili

Ahaaa, kumbe kapatikana ndani ya mahusiano!

Sasa kutishia kukuacha manaake ana option,uwe nae ama usiwe nae yeye kwake ni sawa.
 
usimwamin mtu asilimia 100 kama haujafanya uchunguzi. lkn kaeni muongee kama yupo tayari kukuoa
 
Acha ujinga kukutishia kukuacha manaake uwepo au usiwepo yy kwake ni saw a.
 
FIRST
1. Kakucheat mpaka kapata mtoto
2. Anakataa wakati ni kweli( Wazazi wako sio wajinga maana hawana sababu ya kuongopa)

Kubwa kuliko yote ni kukutishia kukuacha, yani hili ndio baya na ndio ambalo unatakiwa kuliangalia zaidi kuliko hata Swala la kutokuwa muwazi.

Jamaa hakupendi, anakuchukulia poa maana angekuwa na busara na upendo asingekutishia kukuacha wakati yeye ndio mkosaji. Hapo hamna mume dada yangu

SECOND
1. Umewadharau wazazi wako na kutowaamini
2. Mtu anakutushia kukuacha halafu na wewe unajaa upepo unapanic

Kawaombe msamaha wazazi wako kwa ulichowafanyia, wanakupenda mpaka wakakusaidia kufanya uchunguzi ambao wewe ulitakiwa ufanye au utambue sababu ni mtu wako.

Mwisho kabisa acha Kuwa kama kipofu, Kupenda gani huko ambako unaona red flag waziwazi halafu unang'ang'ania tu kuendelea na mahusiano kisa kakuahidi ndoa!! Ndoa haina maana kama unaolewa na mtu ambaye hajali hisia zako kiasi cha kukutishia kukuacha kwa kosa lake mwenyewe. Atakuendesha sana huyo

MWISHO
Mimi nina mtoto nje ya mahusiano yangu Lakini huyo jamaa yako sikushauri aisee sababu hana busara,ishu sio mtoto bali ni jinsi gani kama mwanaume anayekupenda ambavyo anatakiwa kulishughulikia hilo swala.be careful.

Kazi Kwako
I am out

Umenikosha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom