Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Wadada wa sasa Kwani kuwa baba wa mtoto mmoja ni tatizo....!???
 
Kama kwel kazaliwa ndan ya muhusiano..hyo mtu achana nae kabisa, hiyo kitu ni mbaya sana kutoka nje ya mahusiano wakati hanyimwi kitu kwako...ili mradi tu wew hujamkosea kitu,hutakua na dhambi..mungu amekuonesha kwamba huyo cyo mtu mwema, so ukilazimisha kua nae yatakayokuku usimwambie mungu.
 
FIRST
1. Kakucheat mpaka kapata mtoto
2. Anakataa wakati ni kweli( Wazazi wako sio wajinga maana hawana sababu ya kuongopa)

Kubwa kuliko yote ni kukutishia kukuacha, yani hili ndio baya na ndio ambalo unatakiwa kuliangalia zaidi kuliko hata Swala la kutokuwa muwazi.

Jamaa hakupendi, anakuchukulia poa maana angekuwa na busara na upendo asingekutishia kukuacha wakati yeye ndio mkosaji. Hapo hamna mume dada yangu

SECOND
1. Umewadharau wazazi wako na kutowaamini
2. Mtu anakutushia kukuacha halafu na wewe unajaa upepo unapanic

Kawaombe msamaha wazazi wako kwa ulichowafanyia, wanakupenda mpaka wakakusaidia kufanya uchunguzi ambao wewe ulitakiwa ufanye au utambue sababu ni mtu wako.

Mwisho kabisa acha Kuwa kama kipofu, Kupenda gani huko ambako unaona red flag waziwazi halafu unang'ang'ania tu kuendelea na mahusiano kisa kakuahidi ndoa!! Ndoa haina maana kama unaolewa na mtu ambaye hajali hisia zako kiasi cha kukutishia kukuacha kwa kosa lake mwenyewe. Atakuendesha sana huyo

MWISHO
Mimi nina mtoto nje ya mahusiano yangu Lakini huyo jamaa yako sikushauri aisee sababu hana busara,ishu sio mtoto bali ni jinsi gani kama mwanaume anayekupenda ambavyo anatakiwa kulishughulikia hilo swala.be careful.

Kazi Kwako
I am out
 
Asante sana.Barikiwa.
 
Binafsi napenda saaaana ukweli katika maisha yangu but nauthamini saaana mchango wa uongo katika maisha yangu.
Nampa pole huyo unayemwita mwenza kwa kumkana mwanae kisa mwanamke. Me nina mtoto nimezaa kabla ya kuoa but piga ua na ugalagaze siwezi kumkana mwanangu.
 
Unaogopa nini kulea mtoto ambae sio wako dunia imechenj kina madonna wanakuja Africa kutafuta watoto mwambie mpenzio awe huru akutambulishe mwanae na umpende.

Mi wanangu wawili wanalelewa na wazazi wa kambo na hawajapata shida yoyote naitwa kwenye shida tu na mim nimeapa ningepata aliezalishwa nsingeangalia kigezo cha mtoto watoto ni malaika hawana makosa
 
Alizaa kabla yako au baada yako? Unaishi nae nyumba moja au mna ukaribu yaan kukutana mara kwa mara?
My capture ....kuzaa sio tatizo but kutokuwa mkwel ndio tatizo though it depends sometimes inawezekana alidanganya kulinda penzi lenu au kukuepusha na bp na mengine

Pili unaonekana hauko serious nae au hujui tofaut ya urafik na ndoa ulijisahau ukahis bado mtakuwa marafik na kusahau ndoa inataka follow up ya maana as long mnajua wanawake muwengi
Ushauri wangu

Tatu we unaonekana unajua kutenda miujiza...how come you let your parents know your privacy before you? Kuna mengine siri za ndan hata wakijua haina faida kwao hayo ufe nayo wewe sio wao

Ushauri wangu....if you love him na uwe na uhakika kama nae anakupenda unless otherwise atakudanganya

Talk to him ajue unajua then mjue what next
Pili jifunze kujua what marriage wants especially for girls
Tatu jifunze kuwa na privacy sana sana kwa ndugu kwani wao hawajui thaman ya moyo wako zaid yako
 
Baada ya kumcomfront kuhusu kuwa na mtoto kwa nini atishie kukuacha???????anaona kuwa you need this relationship more that he does.

Kwa nini alipoona umejua hakukiri?? maana kukuficha at the beginning pengine alikuwa anatafuta wakati muafaka..lakini baada ya kuona umejua angekubali tu

Msimamo wako wa kutotaka kuingia katika ndoa na mtu mwenye mtoto sio mzuri..ila kuingia katika ndoa na mwanamme wa namna hii ndo mbaya kabisa.

Show him that you are not desperate dada!!! mwambie tena hii ishu na akitaka kutishia kukuacha muulize "do you see me crying?"

Na kwa nini unaacha watu wengine wakufanyie kazi yako mwenyewe ya ugunduziiii? unajua sana kupenda eeeh?
 
Dada unaonekanika una roho mbaya kwel...kwan kama mpezio alipata mtoto kabla ya mahusiano yenu tatizo liko wap..maana ake hajakusalit..alafu mtoto ni zawad mungu anakuzawadia!

Huyo atakua kavurugwa 2 hivi kumkuta kijana ana mtoto kuna ubaya gani mtoto ni baraka istoshe huyo dada inaonekana ina kisununu balaa anaweza mpa mwanao mateso
 
Kwnza pole sana, mimi mwenyewe mpaka hivi ninavyo andika Haya mahusiano yangu ni kama sijui kama yanaweza kuendelea, ila nimemwachia Mungu, naomba nikushauri kufuatilia jambo hilo na kama ukikuta ni kweli, fanya maamuzi kwa kuzingatia mazuri na mabaya ila kuishi na mtu ambaye ana mtoto na mbaya zaidi hakukwambia inauma sana

Mtoto ni baraka istoshe huyo mtoto n mapenzi yenu anahusikaje
 
Pole wazazi hujaaamini ila jf ndio utaamini?
 
Samahani lakini, ila wewe ni wa ajabu, mpaka wazazi wako wafanye ushushushu wewe uko wapi? Wakakuambia lakini bado hukuweza kufuatilia! Ungekuwa karibu na mimi ningekuvuta kofi la hatari!

Nimetafuta sehemu ya kulike hii comment yako nimekosaa,,elewa nime i like
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom