Nataka niache Ualimu nikasomee Udaktari

Nataka niache Ualimu nikasomee Udaktari

Toka zaman UDAKTARI upo damuni na mpaka sasa. UALIMU niliingia tu Kwa sababu ya kukimbilia mkopo. Napenda. Huku napata msahara mimi binafsi naridhika nao, lakini bado. Pia nikiwa hospital nikiwaona madokta na nguo zao zile huwa najiona kama nami ningekuwa pale
Huko wanaosemea udakitari walikuwa hawapewi mikono?
 
je kama ukiwa na hela yako ukasepa zako ata bila ruhusa itakuwaje mm pia nasumbuliwa na hilo nimesoma pcm nkapata div two mwaka 2010 nkasoma ualimu lkn napenda kuwa engineer sasa sielewi wengi wananiogopesha japo nilipanga mwaka huu nisepe zangu niliomba chuo mwaka jana nkapata lkn ruhusa awataki kunipa kabisa nishaurini kwa simu namba 0783962022
 
Duh! By the time unamaliza kusomea udaktari mvi nazo zitakuwa zimeanza kukutoka. Udaktari inabidi uanze kusoma wakati kichwa kiko empty. Haujui cha bili ya umeme wala hela ya matumizi. Ukiwa na mawazo ya pesa kichwani ka udaktari lazima waku Disco!
 
ESPIRIT

Ahan, bahati mbaya ulichukia biology na kusoma pcm , sijui labda uanze na diploma kama inawezekana kutumia cheti cha form 4 kama ulipass vizuri chem & biology....

Kila la kheri...
 
Toka zaman UDAKTARI upo damuni na mpaka sasa. UALIMU niliingia tu Kwa sababu ya kukimbilia mkopo. Napenda. Huku napata msahara mimi binafsi naridhika nao, lakini bado. Pia nikiwa hospital nikiwaona madokta na nguo zao zile huwa najiona kama nami ningekuwa pale
Mkuu mbona hata u-daktari siku zote kuna mkopo?Au hukulijua hilo?
 
Mimi ni Mwalim wa sekondari nafundisha sayansi. Fom4 nina div.2 nilimaliza mwaka 2005. Advanced level nilosoma PCM ntapata div 2.Chuo nikasoma BSc ed. Nataka nikasomee UDAKTARI, Napenda sana, naombeni ushauri wadau.
Karibu
 
Changamkia fulsa nakushauri uombe scholarship ukasome engineering ya amafuta na gas level ya masters kama matokeo yako yako vizuri mbona walimu wenzako wa sayansi pcm wamejajiriwa TPDC kwenye field ya mafuta na gas ambayo bado haijawa na wataalam wa kutosha ukirudi unaweza kubadili maisha yako.
 
Nahic unataka kuacha ualimu labda tu kwa kuwa maslahi madogo ila udaktar ukifuata maslahi tu kama huna passion hata kumaliza tu miaka 5 itakuwa ni shida kwako.
 
What I try to focus between those two fields is that teaching field is escaped by many people because the income isn't sustainable. Medical field is done in a very complicated environment but the income is sustainable.

Income wise diploma in medical field is more valuable than degree in teaching field!!I think this is due to a large number of employees compare to that of medical field.

MY TAKE if you withstand to change a field please do it immediately for your own life effectiveness. Am a teacher but the aged one I can't dare to change am too late.....
 
Udaktari hausomwi bila uthibitisho wa kuwa na msingi mzuri wa Biology. Afadhali ungekuwa ulisoma CBG ukakosa Physics ungeweza kufikiriwa. Hata hivyo kwa kuwa siku hizi kuna vyuo vinavyolenga biashara zaidi unaweza kupata nafasi ya kusoma udaktari na ukafaulu with distinction!
 
Nenda chuo binafsi kinachotoa kozi ya CLINICAL MEDICINE omba nafasi ya kujiunga..

Kwanini Uende Chuo Private?
... Ni kwa sababu ukiomba kwa chuo cha government au ukiomba direct kupitia NACTE kupata ni ngumu kwani hauko eligible kwa sababu umemaliza O-Level kitambo sana.

Baada ya Kusoma Clinical Medicine utakua Clinical Officer (Afisa Tabibu)

Kisha utafanya kazi miaka 2, utaomba nafasi ya Kusoma kwa DMO wako then utaenda Chuo kikuu Miaka Mitano na Kusoma Degree ya udaktari wa binaadamu (Doctor of Medicine)

Karibu Mjomba
Ni lazma afanye kazi miaka miwili ?mkuu
 
Mtoa mada vipi wazo lako ulilifanyia kazi? Ikiwa ulilifanyia kazi umefikia wapi

SUKAH
 
Back
Top Bottom