Nataka niache Ualimu nikasomee Udaktari

ESPIRIT

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
665
524
Mimi ni Mwalim wa Sekondari nafundisha sayansi.

Form 4 nina Div. 2 nilimaliza mwaka 2005, Advanced Level nilosoma PCM nikapata Div. 2 na Chuo nikasoma BSc ed.

Nataka nikasomee Udaktari na napenda sana,

Naombeni ushauri wadau.
 
Kama ulisoma biology O level vyuo vya nje unaweza kupata admission na ukapata elimu iliyo bora ambayo itakusaidia kukabiliana na mazingira.

Vyuo vya Tanzania bado vipo nyuma sana kimtizamo na kiutaratibu na hata syllabus za hapa kwetu bado ni za kale sana unachomsoma darasani hakikuti kazini.

Nakushauri tafuta vyuo vya india au Malaysia mambo yako yatakuwa poa.
 
Kitu gani atakachosomea kwenye AFYA hatakikuta kazini?!
 
Nenda chuo binafsi kinachotoa kozi ya CLINICAL MEDICINE omba nafasi ya kujiunga..

Kwanini Uende Chuo Private?
... Ni kwa sababu ukiomba kwa chuo cha government au ukiomba direct kupitia NACTE kupata ni ngumu kwani hauko eligible kwa sababu umemaliza O-Level kitambo sana.

Baada ya Kusoma Clinical Medicine utakua Clinical Officer (Afisa Tabibu)

Kisha utafanya kazi miaka 2, utaomba nafasi ya Kusoma kwa DMO wako then utaenda Chuo kikuu Miaka Mitano na Kusoma Degree ya udaktari wa binaadamu (Doctor of Medicine)

Karibu Mjomba
 
Kama tayari umeajiriwa kwa fani ya ualimu endelea nayo,ila kama bado hujaajiriwa bado una uchaguzi uende wapi,ualimu huwa hauachwi ovyo ovyo,ukipewa wanafunzi wafundishe kikamilifu,ukiacha bila mpango maalumu utajuta mbeleni.
 
Atajutia nini,ungeelezea
 
Unavutiwa na u-daktari au umechoshwa na ualimu?
Naomba unijibu mwalimu wa sayansi.
Toka zaman UDAKTARI upo damuni na mpaka sasa. UALIMU niliingia tu Kwa sababu ya kukimbilia mkopo. Napenda. Huku napata msahara mimi binafsi naridhika nao, lakini bado. Pia nikiwa hospital nikiwaona madokta na nguo zao zile huwa najiona kama nami ningekuwa pale
 
Nenda chuo binafsi kinachotoa kozi ya CLINICAL MEDICINE omba nafasi ya kujiunga..

Kwanini Uende Chuo Private?
... Ni kwa sababu ukiomba kwa chuo cha government au ukiomba direct kupitia NACTE kupata ni ngumu kwani hauko eligible kwa sababu umemaliza O-Level kitambo sana.

Baada ya Kusoma Clinical Medicine utakua Clinical Officer (Afisa Tabibu)

Kisha utafanya kazi miaka 2, utaomba nafasi ya Kusoma kwa DMO wako then utaenda Chuo kikuu Miaka Mitano na Kusoma Degree ya udaktari wa binaadamu (Doctor of Medicine)

Karibu Mjomba
Asante
 
Kama tayari umeajiriwa kwa fani ya ualimu endelea nayo,ila kama bado hujaajiriwa bado una uchaguzi uende wapi,ualimu huwa hauachwi ovyo ovyo,ukipewa wanafunzi wafundishe kikamilifu,ukiacha bila mpango maalumu utajuta mbeleni.
Look this man advice you in humble and in very technical approach. Kama hutozingatia alichosema damu yako na iwe juu yako.
Utapataje kupona usipoujali ushairi mkuu namna hii ambao kwanza umenenwa na watu wenye taaluma yao kwamba kwenye ualimu wala hujapotea njia. Hii hunifanya niamini kwamba kama hujui unakoenda huwezi kupotea. Tatizo wwe unapajua unapoenda ndo maana umepotea
 
wamekushauri vizuri!!! nenda clinical medicine ya miaka mitatu, kama uko kazin tayari umefikisha miaka miwili, omba kwenda kusoma, den badilisha course baada ya ruhusa, au chukua kamkopo sepa zako kasome, still unaweza timiza ur dream
 
Back
Top Bottom