Nataka kwenda kuchora Tatoo

Nataka kwenda kuchora Tatoo

Watu wa dini na wahafidhina wanapingana na hayo mambo...jamii unayoishi ni watu wa dini/wahafidhina? Unajali jinsi jamii inayokuzunguka inavyokuona?
Kama majibu ni hapana basi nenda
 
Mambo ya Walawi 19:28
"Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana".
Mama mchungaji Mimi sitaki ushauri mama,nimeomba nielekezwe,hivi mpaka Leo inamaana Mimi sijui zuri na baya?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni muislam nakushauri usichore kwani ni laana ya wazi amelaaniwa yule mwenye kijichora tatoo na mchoraji
 
Fundi huyu hapa

22c2a84f9a8fef3f76bd22209c4f5f19.jpg


sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Hizi tattoo aisee Mh! kuna watu wameanza kuweka mpaka usoni! Na wengine miili yao imejaa tattoo kila sehemu ya miili yao hata kupoteza ile rangi ya miili yao, lakini kuna baadhi zinapendeza mno hasa kwa warembo zilizowekwa kwa utalaamu mkubwa.
Kwangu itakua ni ya kwanza Mkuu na ndio itakua ni ya mwisho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bongo hamna artist wa tatu, kama unabisha kachore ndo utajuta kuchafua ngozi yako na hicho utakachokichora hautatamani hata kukiangalia. Kuna jamaa mmoja yuko kenya na pia hua anakuja bongo kwa appointment ni artist mzuri na pia gharama zake ziko juu lakini akikuchora tatoo utatamani kila mtu aione. Good tattoo is not cheap, cheap tattoo is not good.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya hebu ni connect nae basi nione kama naweza kutumia kijimshahara kangu kuchora kimstari tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaki ushauri nataka mnipe Location ya mafundi tatoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mjini location zipo nyingi saana.... Raha ya tattoo uwe na Ngozi angavu kama imefubaa ni shida.

nenda kipawa pale parish pale pale beneath kuna saloon wanaita Soul tattoo salon.


Kuna tena hawa jamaa wanaitwa Pollo tattoo wapo bamaga.. ni maarufu saana.
 
Chora mama, tena chora tu tattoo za kutosha. Allah ametupa utashi, lakini ukiutumia utashi huo bila yeye mwisho ndio kama hivi.

Wenye location please help her, ndipo dunia ilipofikia sasa, what can we do!!
 
mi pia mpenzi wa tatuu nilitamani niwachore mabinti zangu "geniveros"ila daah naogopa kwa Mungu tuuuu kwenda na kidhibiti mwilini

wale wanaochora usoni wamevurugwa wale
Unaogopa dhambi ya Tatoo tu kwa Mungu!? mnanichekesha sana ila kuzini mnazini,pombe mnakunywa,matusi mnatukana,uongo mna nena ila Tatoo tu ndo dhambi ya kuogopewa kwa Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila kitu cha kuinga vingine potezea...

Ukisha jichora tatto na akili zako za kawaida huwa zinaondoka, angalia asilimia kubwa ya raia wa kawaida huko mtaani walio chora tatto uangalie jinsi walivyo..
Haya asante! Acha akili zinitoke kama ndevu za zito K

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom