Nataka kuoa ila masharti magumu

charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
436
128
Nina umri usiozidi 31, nina watoto 4 kila mmoja na mama yake, wa kwanza nilimpata nikiwa sekondari, wa pili nikiwa chuoni, wa tatu nikiwa internship na wa nne nikiwa chuoni tena. Wawili kati ya hao wadada wameshaolewa, natamani sana kuoa sasa. Nilipowaendea hao wawili waliobaki kila mtu kwa nafasi yake walikubali ombi langu ila hakuna anayetaka kuletewa mtoto wa nje. Nimeshindwa nifanyaje kwasababu siwezi kuwa mbali na wanangu, hivi sasa nimeshawachukua wawili wapo boarding school na hao waliobaki natarajia kuwachukua ASAP. Wanajamvi natamani sana kuoa lakini mambo ndo hivo yalivyo. Nifanye je?
 
anamaanisha ww hauko kwenye market vizuri sana. una tabia ya kuwa na mahusiano ya kizembe ( 4 kids 4 women, kila mahali unapoenda huogopi ukimwi) na ukishapata mtoto unachapa lapa! tafuta mjane (wapo wana miaka 30 tu ndoa zimekatishwa na Mungu!). otherwise, kwa msichana aliejitunza lazma anategemea watoto wengine kama kumi hivi kwa kipindi cha ndoa (kama hamtaachana mara baada ya kuzaa na mkeo huyo!). huweiz kurudia kosa lile lile mara 4, hata kama hujajifunza walau ungekuwa bored na kukosea!

unamaanisha nini???
 
hawataki kuletewa watoto wa nje maana inaonekana wewe ni kiwembe so unaweza kuwajazia timu toka out.....Badirika kwanza then ndio uchukue hiyo hatua. watoto 4 kila mmoja na mama yao sio poa.
 
watoto wanne nje ya ndoa na bado hujaoa? hii kali.
man, nafikiri haupo serious, situation kama hizi zinatokea haswa ukizingatia situation niliyokua nayo ya ustudent. sasa mimi m2mzima nataka kusttle
 
hawataki kuletewa watoto wa nje maana inaonekana wewe ni kiwembe so unaweza kuwajazia timu toka out.....Badirika kwanza then ndio uchukue hiyo hatua. watoto 4 kila mmoja na mama yao sio poa.
nataka ufahamu mimi si kiwembe, ningelikua kiwembe tungezungumza mengine saa hii. pilinilishabadilika kwani mtoto wa mwisho ana miaka mitatu. sina nia ya watoto wengi ila kwa mwanamke akipendezwa nami nitaridhia kumpa wawili. najua sio poa niliyofanya lakini siwezi kuwatupa wanangu
 
Nenda kijijini kwenu wazee watakutafutia mke mwenye huo uwezo wa kulea.
asante lakini umekosea. nia ninayo, uwezo ninao. kwanini nitafutiwe? kwanini kwenda kutafuta kijijini ilihali mjini wapo? sidhani jambo la kulea hapa lina umuhimu kwasababu watoto ni wakubwa
 
Kaka we kondomu ulikuwa huzioni au? Mitoto mi4 unataka umpelekee msichana mbichi huoni aibu au? Zaa tu nje manake ndio utaratibu wako wa maisha.
 
anamaanisha ww hauko kwenye market vizuri sana. una tabia ya kuwa na mahusiano ya kizembe ( 4 kids 4 women, kila mahali unapoenda huogopi ukimwi) na ukishapata mtoto unachapa lapa! tafuta mjane (wapo wana miaka 30 tu ndoa zimekatishwa na Mungu!). otherwise, kwa msichana aliejitunza lazma anategemea watoto wengine kama kumi hivi kwa kipindi cha ndoa (kama hamtaachana mara baada ya kuzaa na mkeo huyo!). huweiz kurudia kosa lile lile mara 4, hata kama hujajifunza walau ungekuwa bored na kukosea!

hapa mkuu umekosea. kama ni swala la market nadhani niko wa bei ya juu maana nimeshaproove nina uwezo wa kiume. mahusiano nhayakua ya kizembe ukizingatia situation niliyokua nayo. isitoshe ningelijua hao wanawake wangelipata ujauzito nisingefanya hicho kitendo kwa wakati huo lakini sikujua, hesabu zao walifanya kimakosa. pia sina nia ya kusaka girlfriend bali WIFE so jambo la kuachana ondoa shaka
 
smtimes kuna makosa huwa tunayafanya ujanani bdae yanatucost sn. See how unahangaika? From now control urself kakangu wasije wakawa 5 6 tabu ikaongezeka. Unaweza ukaendelea kumwomba Mungu akupe mke atakaewapenda hao wanao ipasavyo. Punguzu ngono zembe 2lia one day utampata tu
 
Hahaha..
Wewe fanya kazi ya kulea wanao wanne aisee,
u will be so busy with them to even remember marrying!
Kweli hii yako kali!
 
kaka, tatizo lako ni kubwa kuliko nilivyofikiria! kama ni malaria hii ni 10,000 sio 2! hadi chuo hujajua ukikutana kimwili na mwanamke bila kinga atabeba mimba? na sio jukumu lako, ni hesabu 'zao'! Aisee, ngumu kumesa! market ya mwanaume sio kuvaa mashati mazuri na kuwa na bank balance kaka! ni pamoja na uwajibikaji! wa kwanza alikuwa hajui mahesabu, wa pili naye kadhalika! wala hukugundua ungeweza kuenda tuition ukagundua na ww jinsi ya kufanya mahesabu, ukarudia tena! inabidi sasa upate mhandisi kabisa! na mdogo ana miaka 3, unadhani utakayeoa anajua mahesabu manake 3 yrs ago hukujua mahesabu? wasi wasi wangu mkuu ni huu ulowekaji wako na maradhi haya ya sasa. inabidi ujifunze sio mahesabu tu, bali calculus pia! nina wasiwasi hujajifunza kutokana na makosa, na niamini, mwanamke mwenye akili zake timamu atakupiga interviwe hadi ukasirike. nakuandaa tu kukutana na challenges.

Back
Top Bottom