Nunua chip zote TIGO,VODA,ZANTEL,ZAIN kila moja ina faida yake
........What???Ndugu mfano mimi huwa natembelea sana kanda ya ziwa haswa maeneo ya madini kule , maeneo yale mara nyingi sana zain ndio haisumbui au kuleta tatizo lolote ukiwa na report au ukitaka kuwasiliana ni hapo hapo ukiwa na simu pamoja na laptop yako mitandao mengine yote huwa inaleta utata muda mwingi haipatikani labda uwe karibu na minara karibu nayo
hizo line nyingi tuseme labda kwa sababu ya promotion na urahisi wa gharama za mawasiliano kama zantel kupigiana ingawa sasa hivi kampuni zote zinaviwango vyake vya mawasiliano vya chini mfano kwa sasa zain kuanzia saa 4 usiku unaweza kuongea na simu za nje kwa gharama ya tshs 5 kwa dk huo ndio mtandao wa kwanza kwa tz kufanya hivyo ingawa zantel walikuwa na huduma hiyo ingawa kujiunga ulitakiwa kulipa kiasi cha alfu 20
Wadau, mimi ni mteja wa Zain tangu mwaka 2004. Niliponunua simu nilipewa sim card ya Voda kama offer ikiwa na shilingi 1,000/- na baada ya mwezi mmoja nilihamia Tigo (Mobitel wakati huo) baada y kuona kuwa Vodacoma wako ghali sana. Mwaka 2004 nilipoteza simu na hivyo niliponunua simu nyingine nikaamua kuhamia Celtel baada ya kuona mahali nilipokuwa mandao wa Mobitel unasumbua.
Baada ya Celtel kubadilisha jina na kujiita Zain, walituandikia wateja kwa sms kuwa wanakuja na mfumo mpya wa bonasi badala ya ule wa zamani kwa ajili ya wateja wao waaminifu (loyal customers). Baada ya kuingizwa kwenye hilo daraja la loyal customer kuanzia Novemba, Zain wakaja na mfumo mpya wa bonasi za kulazimisha ambazo ndo zinanifanya kutaka kuhamia mtandao mwingine. Kwanza walianza kutuandikia wateja sms kuwa ongeza 40,000/- kabla ya tarehe fulani upate bonasi ya shilingi 12,000/-! Kwa kweli mfumo huo unanikera na juzi nimepokea sms nyingine ati niongeze shs 40,000/- kabla ya tarehe 26 Dec ili nipate bonus! Ilinudhi sana maana nilidhani ni sms ya muhimu. Zamani Celtel ukiongeza airtime kwa muda fualni unatumiwa sms kuwa umepewabunus ya shilingi kadhaa na si kushawishiana kutumia ili upate bonus kama sasa.
Mfumo wa sasawa kupata bonus na hasa kunitumia sms ati niongeze shs kadhaa kabla ya tarehe fulani ili nipate bonus umekuwa kero kwangu maana sioni sababu ya kunishawishi kuongeza matumizi ati nipate bonus.
Wana JF nimeazimia kuachana na Zain, Je, nihamie mtandao gani ambao ni bora zaidi?
Yaani unahama Zain- kisa Bonasi?
A u serious?[/QUOTE]
Mzalendo, hukunielewa, kinachonikera ni kuwa msg inaingia na ninapoisoma wananiambia niongeze 40,000/- kabla ya tarehe 26 Des. ili nipewe bonus. Msgs hizo huingia mara kwa mara kiasi kwamba inakuwa ni kero.
Kanakansungu amenielewa vizuri, laiti Zain wangetupa wateja option ama ya kupokea au kukataa msg zao za promotion kama ilivyo kwenye e-mail ambapo kuna option ya kuzipiga spam msg address zote ambazo hutaki kupokea mail zao.
Ni jambo la kawaida kwa makampuni ya simu kuwatumia wateja wake sms kama hizo unazotumiwa hata huku Ulaya lakini kuna option ya kuzistopisha kama hutaki kusumbuliwa, am not sure if this thing exists with Zain. Naamini pia ukiwapigia simu Customer service wa Zain na kuwajulisha kero yako ya hizo sms wataweka mambo sawa, binafsi sioni kama ni tatizo kubwa kiasi cha kukuhamisha mtandao.
In general gharama za simu za mkononi bongo ni ndogo kama utapiga simu kwa watu walioko kwenye mtandao wako ie Zain to Zain au Tigo to Tigo, ukicross kwenye mtandao mwingine gharama ni almost double! inakula kichizi ndio maana its very common kwa Bongo kumkuta mtu anatembea na simu tatu!Simu ya lines mbili itakufaa sana.
Asante Kanakansungu mwela, wewe umenipata vizuri.
Plz dont make me angry!!! Bado hujahamia tigo? Unasubiri nini? Hata mawaziri siku hizi (ofcoz na mafisadi) wanatumia tigo, so wahi haraka msela tigo mtandao wa wajanja, why pay more while u can pay less for the same service???? kuwa macho baba, zain waizi!!!
Plz dont make me angry!!! Bado hujahamia tigo? Unasubiri nini? Hata mawaziri siku hizi (ofcoz na mafisadi) wanatumia tigo, so wahi haraka msela tigo mtandao wa wajanja, why pay more while u can pay less for the same service???? kuwa macho baba, zain waizi!!!
Nishajipatia TiGO mkuu, yaani ni bomba kweli hata ukipiga kwenye mtandao mwingine bado ni nafuu. Hata hivyo bado nina laini ya Zain, uchumi ukiruhusu itabidi ninunue hata simuya promotion ya Zain maana jamaa zangu wengi wananipata kupitia Zain.