Nataka kuanzisha biashara ya kuuza soda, naomba ushauri

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,331
14,259
Wapendwa sana wanaJF, habari za asubuhi...

Siku chache zijazo nimefikiria kuanzisha biashara ya kuuza soda za chupa na za kopo (take away) kwa bei ya jumla na rejareja.

Mwenye uzoefu na biashara hii naomba anijuze kuhusu mtaji, faida na changamoto za biashara hii. Aidha kama kuna maujanja mengine kuhusu biashara hii anijuze.

Nitashukuru kwa msaada wenu.
 
Tatizo mnakalia vitu vya mihemko na kushikilia vitu ambavyo havina maana yoyote katika maisha yenu sasa swala la soda za mirinda na pepsi zinawasaidia nini hasa katika kipindi hiki kigumu cha maisha?

Halafu mnalalamika viongozi hawawajibiki je kukalia habari za chupa za mirinda na pepsi zitawarekebisha viongozi wenu?

Msipoacha ujinga huu mtaburuzwa sana!!
 
Bro, nakushauri tu badili ID yako Che Guevara hakuwa lofa km wewe.Akili Yako inawaza mavi tu,watu tupo serious na maisha, Wewe unaleta maneno yako ya kujiharishia.Km huwezi kutoa mawazo ya kujenga ni bora kufyata mkia tu.
 
Tatizo mnakalia vitu vya mihemko na kushikilia vitu ambavyo havina maana yoyote katika maisha yenu sasa swala la soda za mirinda na pepsi zinawasaidia nini hasa katika kipindi hiki kigumu cha maisha?

Halafu mnalalamika viongozi hawawajibiki je kukalia habari za chupa za mirinda na pepsi zitawarekebisha viongozi wenu?

Msipoacha ujinga huu mtaburuzwa sana!!
Mkuu nini kimekusibu mwisho wa mwaka huu.
 
Tatizo mnakalia vitu vya mihemko na kushikilia vitu ambavyo havina maana yoyote katika maisha yenu sasa swala la soda za mirinda na pepsi zinawasaidia nini hasa katika kipindi hiki kigumu cha maisha?

Halafu mnalalamika viongozi hawawajibiki je kukalia habari za chupa za mirinda na pepsi zitawarekebisha viongozi wenu?

Msipoacha ujinga huu mtaburuzwa sana!!
Mkuu ivi unajua upo jukwaa gani???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu mtaji hasa wa jumla sifahamu Ila Mimi nilikua nauza soda rejareja na maji ukichukua kwa Mara ya kwanza utachukua kreti moja 20000/= this means soda na kreti lake, Kama unazo kreti zako ni vizuri zaidi au tafuta wale watu ambao wanauza kreti ili kupunguza gharama kwa hiyo unaweza kupiga hesabu hapo unataka uanze na kreti ngapi,kubadilisha kreti ni 9800 kwahiyo kwenye kreti moja ya soda wewe unapata faida sh 3000 kwa rejareja.ili kupata faida unatakiwa uwe sehemu yenye mzunguko wa watu hasahasa maeneo ya sokoni na usiweke soda peke yake weka na maji hata kampuni mbili tofauti kwa kuanzia na juice mfano apple punch na energy.na kuhusu jumla ulizia tu kwenye kampuni husika coca na Pepsi sio lazima uende ofisini mahari Yao yanapita barabarani kila siku ukiliona tu wewe waulize watakupa muongozo, maana unaletewa mzigo mpaka ofisini kwako Ila sijui wanataka uanze na kreti ngapi kwa jumla.
all the best
 
Biashara ni zaidi ya kununua kwa jumla ukauza rejareja. Utapeleka sokoni hukute hakuna wateja wa kutosha kukupa faida
 
Wapendwa sana wanaJF, habari za asubuhi...

Siku chache zijazo nimefikiria kuanzisha biashara ya kuuza soda za chupa na za kopo (take away) kwa bei ya jumla na rejareja.

Mwenye uzoefu na biashara hii naomba anijuze kuhusu mtaji, faida na changamoto za biashara hii. Aidha kama kuna maujanja mengine kuhusu biashara hii anijuze.

Nitashukuru kwa msaada wenu.
Wapendwa sana wanaJF, habari za asubuhi...

Siku chache zijazo nimefikiria kuanzisha biashara ya kuuza soda za chupa na za kopo (take away) kwa bei ya jumla na rejareja.

Mwenye uzoefu na biashara hii naomba anijuze kuhusu mtaji, faida na changamoto za biashara hii. Aidha kama kuna maujanja mengine kuhusu biashara hii anijuze.

Nitashukuru kwa msaada wenu.
Kwema mdau, biashara ya soda ni nzuri iwapo ukipata sehemu nzuri ya mzunguko wa watu na pia Mimi nitatoa gharama za rejareja kuhusu biashara iyo ya soda.

Ukinunua being jumla kwa wakala wa vinywaji Bei zake ni kama ifuatavyo

1. Pepsi - 20,000/= (kreti ikiwa na soda zake) ila kama una kreti yako utabadilisha/kununua kwa 9,800/=.

2. Cocacola- 20,000/= (kreti ikiwa na soda zake) ila kama una kreti yako utabadilisha/kununua kwa 9,800/=

3. Jambo soda, energy & juice 300ml -4,500/= per katoni

4. Jambo maji 1.5ltr - 4,000/= per katoni
WwwWw
5. Jambo Maji 500ml - 3,500/= per katoni

Faida zake ni:-

1. Pepsi (Ina chupa 24) - 2,200/= per kreti moja.

2. Coca-Cola (Ina chupa 24) - 2,200/= per kreti moja.

3.Jambo soda, energy & juice (zipo chupa 12 kwa Kila katoni) - 1,500/=

4. Jambo maji 1.5 lita (ina chupa 6) - 2,000/= kwa katoni moja.

5. Jambo maji 500ml (chupa 12) - 2,500/= kwa katoni.

NB:- hizo ni gharama za kununua vinywaji kwa Bei ya jumla toka kwa mawakala na ukauza kwa rejareja ila gharama hutofautiana mkoa kwa mkoa.

Na pia fremu gharama zake hutofautiana mkoa kwa mkoa ila ukiwa na kianzio cha laki 3 unafanya biashara vizuri tu chunguza Kwanza kabla hujaanza.
 
Hii biashara ni nzuri sana, kuna jamaa angu anafanya pale Chama mikocheni hakika anauza sana inakua nzuri ukiwa na vijana ata wawili unatafta wateja wa uhakika unakua unapigiwa simu ata katon moja unampelekea mpaka dukani kwake alafu wewe unawalipa vijana kwa jinsi mtakavyokua mmekubaliana, jamaa angu yy anawalipa kwa mwezi kikubwa uwe na Toroli kama litakua na tair za pikipiki itakua vizur zaidi, pia uwe na baskel ata mbili kwa ajili ya vijana kusambazia Mzigo hakika ukifanya hivo faida imo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom