Mchanganuo wa Kuanzisha TRADING COMPANY

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,497
5,533
Habari za wakati huu;

Ni matumaini yangu kwamba unendelea salama na shughuli zako za ujenzi wa Taifa.

Leo nimeleta Mjada kuhusu aina ya Biashara inayohusisha zaidi na Ununuaji na Uuzaji wa bidhaa na huduma.Biashara hii ambayo ni biashara maarufu zaidi ulimwenguni huwa inahusisha mnunuzi kununua bidhaa na kuziuza kwa kuongeza kiasi kidogo cha commission kama faida.

Trading Business ni aina ya biashara ambayo mtu yoyote anaweza kuianza kwa kiwango chochote ch mtaji kwani aina hii ya biashara haina vizuizi vigumu vya kuingia sokoni(Barrier to Market entry) kama vile teknolji,mtaji, au utaalamu wa kipekee.Hivyo basi mara nyingi utaona hata ukienda Kariakoo utaona kuna machinga anatandika mzigo wake chini,kuna mawinga wako madukani,kuna wamiliki wa maduka,kuna madalali wa mizigo ya jumla na kuna wanaopiga picha na kuweka mtandaoni na kuuza bila kuwa na mzigo kabisa.

Jambo la kuzingatia unapotaka kuanzisha aina hii ya biashara na kuhakikisha unachagua soko lako,aina ya biashara au bidhaa na namna ambavyo utajitofautisha na wengine.Ukweza kufanya hayo kwa umakini basi unachotakiwakufanya ni kuingia sokoni kwa kujiamini.

Unapochagua aina ya bidhaa hakikisha unaelewa bidhaa husika na unaweza kumshawishi mtu kuhusu bidhaa husika.

Karibuni tujadili kwa pamoja namna ambavyo mtu anaweza kuanzisha,kusimamia na kuendesha aina hii ya biashara pamoja na fursa na changamoto zilizopo
 
Back
Top Bottom