Anataka kuanzisha biashara ya kuuza nafaka, anaomba ushauri

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,560
8,638
Ni muda tena.

Katika tafuta tafuta zake akaje kunicheki na kuniomba ushauri kuhusiana na duka kiujumla duka la vyakula kama muitavyo nafaka.

Maswali aliyouliza. Je, kuanzisha biashara ya kuuza unga, mchele, mafuta, maharage nk inahitaji awe na nini (Vibari gani kisheria)

Anamaanisha je anahitaji service levy, leseni ya biashara, TRA au kuona viongozi gani ili kufungua duka?

Nawasilisha, mimi sifahamu.
 
Hapo nenda tra ukapate namba yako ya mlipa kodi yaani TIN. Kisha nenda halimashauri na TIN yako upate leseni ambapo utawapa location ya biashara yako aina ya biashara watakupa leseni then unakwenda kutundika ofisini kwako kazi inaanza.

Hakuna mambo mengi sana.
 
Kama una pesa na tayali tafuta eneo ambalo lina msongamano mkubwa wa watu, kisha tafuta chumba anza biashara, kisha nenda TRA,

Zingatia kama umepanga flem ya zaid ya sh 80 eflu ule mkataba usiende nao kule kwenye makadilio ya kodi tafuta au tengeneza mkaba mwingine feki ambao kodi isome sh 30 eflu,

Ikiwa duka lako lipo sehemu mashuhuri kwenye mkataba andika sehem nyingine ambayo sio mashuhuri mfano kwa huku dar, sehemu kama tandika, vingunguti, mbagala, g-mboto au chanika hauwezi kupata flem chini ya laki na nusu kwenye barabala kuu kwa maana wale watu wa TRA na manispaaa wanajua hili, ukipeleka mkataba wakiangali wanajua umedanganya,na hauwezi kuwa na mtaji wa sh laki 8 ukapanga flem ya laki 2 kwa mwezi,



Maisha yetu yamekuwa duni kwa sababu ya kodi kandamizi na ukisema ulipe kodi kisheri ahutobi, ,

Ukiweka chakula na pombe kama k vant nk unatakiwa kuwa na leseni 2 au ya bidhaa mchanganyiko na pombe kali,
 
Back
Top Bottom