Nataka kuahirisha kuoa Oktoba Mwaka huu

Granted Faith

Member
Jul 4, 2021
57
292
Wadau nisaidie kimawazo na Ushauri Mwaka huu Mwez October ni harusi yangu ila Gafla imetokea sitaki kusikia kitu kuhusu ndoa kabisa. Inshort sitaki kuoa Mwaka huu hata mwanamke nayetaka kumuoa sitaki hata kumuona nimetokea kumchukia Namuona hadi ni kero kwangu

Taratibu zote za harusi tayari ila nataka kuahirisha kufunga ndoa mwaka huu nifanyaje ili hii harusi isifungwe mwaka huu nimechanganyikiwa

1625727787067.png
 
Title imenishtua kidogo. Nimesoma kwa haraka haraka eti "Kuharisha" kumbe ilipaswa kuwa kuahirisha

Screenshot_20210707-115144.jpg


On a serious note: unafikiri ni kwa nini hali hiyo imekutokea? Kuna tukio la kutisha limetokea maishani mwako (mf. kufiwa na mtu wa karibu, kufukuzwa kazi...) au huko nyuma uliwahi kuumizwa sana na wanawake kiasi kwamba unafikiri hata huyu atakufanyia hivyo hivyo kama waliotangulia? Au kuna watu hawataki hiyo ndoa yako na huyo binti?

Tafuta chanzo cha hisia hizi na itakusaidia sana huko mbeleni. Ni hayo tu kwa sasa
 
Tatizo lako lilianzia pale ulipowatangazia hata wale uliowaaminisha kuwa utawaoa na haikuwa hivyo.

Kwa nini mnatangaza sana uchumba kuliko ndoa?
Kikulacho kinguoni mwako.

Ktk vitu ambavyo havishauriwi kuvichelewesha ni vitatu
1. Ndoa
2. Kuzika
3. Kusilimu

Hivi vitu huwa vina fitna nyingi ndani yake.
Tafadhali usihairishe km huyo mke mtarajiwa hajakukosea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom