Nataka kuacha kazi .

Pole mpenzi, hauko peke yako watu wengi ama wanapitia, walishapitia au watapitia hali hiyo hasa watumishi wa umma, ila usikate tamaa.

USIACHE KAZI

220k unayoona ni ndogo wakati huu ukiacha utatamani hata ukaibe uipate,

Fanya yafuatayo
1.Usiwe mvivu pika mandazi kwa mtaji wa buku kumi uwezo wa kupata faida ya elfu tano ukaiacha watoto wakala upo
2.Usiringe, wasomi wengi tunaringa yani kuna maisha flani tunaitaga ya wasiowasomi, unaishi maisha ya juu bila kuangalia kipato chako
3.Ishi kawaida, nguo za gharama achana nazo, nywele etc.

Unaweza kufanya yafuatayo
Tengeneza unga wa lishe mtaji ni kama 30k
Pika mandazi mtaji 10k
Tengeneza karanga za mayai mtaji kama 20k

Yani sometimes mtumishi ukifa njaa naweza sema umependa naongea kwa experience mimi nimefanya kazi ambazo hazina hata heshima unasota na watu ambao hawajasoma ila ukija kwangu wanangu wanakula vizuri wanavaa vizuri kutokana na kujishughulisha ila ukiwa sister du eti siwezi pika mandazi ndo mwisho wa siku lazima uwende soko la usiku mana hela rahisi now day's haipo.
 
Aisee, nilikuwa sijasoma uzi wote, nimefika hapa naona tatizo ndio lipo

Mtu unalipwa 220k, unalipia watoto ada ya 100k kila mwezi, una mfanyakazi wa ndani unamlipa labda 30k, unaishi nyumba yenye vyumba viwili labda 100k, unalipia umeme labda 20k, maji labda 10k, chakula kwa kujibana ni 80k, nauli ni 40k, Jumla ni 370k
Ana matumizi zaidi ya mshahara wake ya zaidi ya 150k kwa mwezi

Hapo kwa haraka haraka ni kufanya hivi
Watoto wapeleke shule za Serikali, au hata kijijini kwa bibi waende za kijijini huko, umesave almost 80k, nyumba ondoka tafuta single room hapo ume save kama 50k, beki tatu ondoa, umesave 30k, chakula chako mwenyewe kama kazini mnakula hata 60k inatosha, so umesave 20k
Negative balance inaondoka...

Mtumishi wa Umma
 
Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.

Hii paragraph hii. Basi mkuu Mungu akusaidie, hayo yote ni mapito.
 
#Hata usiku uwe mrefu vipi lazima kupambazuke

Utakiwi kukata tamaa
Mfikirie mama aliyeishia la saba aliyeachwa na watoto watano akipata hiyo 220k atafurahije!!
 
Wanawake wanajifanyaga kupenda sana watoto kama silaha ya kupigia wanaume,sasa usihangaike nao wakikomalia watoto waachie usihangaike nao japo mm huwa nawaonea huruma watoto,yaani upuuzi wa mwanamke unaenda kuwaadhibu
Mtu anajifanya hana haja na huyo mzazi mwenzie lakini anamlaumu,huyu kachangangikiwa
 
Umesema unakiwanja Fanya hivi kisaminishe benki wakupe mkopo harafu usirufishe mkopo hata wakija kupiga bei hicho kiwanja huna haja nacho
 
Sijamlaumu Kwa lolote Wala sihitaj kumwadhibu Kwa lolote,atajijua na Mungu wake
mie nilieleza situation ya mzaz mwenzangu ili kuwaweka wachangiaji aware wasijeuliza baba wa watoto yukwapi ama anachangia nini
Uzi huu ni maalumu kwaajil yangu,wanangu na changamoto za kazi ninazopitia, that's the main point.
 
Sina Kijiji cha kupeleka wanangu kwani walonilea walishafariki
Walobak wote wananiangalia mie ambao ndo warithi wa walezi wangu,nyumba nzima walishapangisha hata chumba nilichokuwa naishi mimi walishapangisha
Wamebak watoto za walez wangu marehemu na ndio warithi ,wakagawana vyumba na kuvipangisha vyote wanapokea Kodi Kila mmoja,mie nililelewa tu pale baada ya wazaz wangu kufariki.
 
NINA BONGE LA USHAURI NA HAKIKA UKIUZINGATIA UTA_WIN SOON NA UTAFURAHI,
ILA JIBU HILI SWALI KWANZA,

NI SABABU IPI IMEKUACHANISHA NA MUMEO WATOTO WAKIWA WADOGO KIASI HICHO??
 
Hayo ni mapito tu,Maisha yetu yalivyo ni kama uonavyo season za vipindi vya majira katika mandhari zetu kama kuna kipindi cha joto,Masika,vumilia maisha ndivyo yalivyo,Na pia kama unauwezo jaribu kutafuta mume uolewe huenda mawazo yakakupungikia
KWA WANAUME VIJANA NA WENYE UMRI WA MAKAMO,

NI WACHACHE SANA WENYE UTAYARI WA KUJIBEBEA MKE MWENYE WATOTO WADOGO KUANZIA WAWILI NA KUENDELEA.

SANASANA WATAANZA KU_DOUBT,
"NI KWA NINI KAACHANA NA MUMEWE?!?!
LABDA ANAWEZA KUWA NA MATATIZO FULANI YASIYOVUMILIKA HUYU!!!"

KISHA WANASEPA,
LABDA APATE MZEE ASIYEJALI SANA.
 
Suala la kuacha kazi, ni moyo wako binafsi na kile unachokiamini, hapa yatakuja maoni mengi lakini yanaweza yakawa nje ya moyo wako unachoamini.
 
A
Amesoma nini
 
HIYO AYA MWISHO HIYO INA MADINI KUNTU SANA-
SISI AMBAO HATUTAKI KUGOMBANAGOMBANA HUWA TUNAKUVUTIA KASI TU-
UKIZIDISHA JEURI TUNAFANYA MAAMUZI YA BUSARA,
KISHA TUNAANGALIA USTAARABU MWINGINE.
 
MKUU,

WEWE VUMILIA UMALIZE HUO MKOPO KWANZA,
MAANA'KE HUO ND'O UNAOKUFANYA UPANIKI,
MALIZA MKOPO TU-
SOON UTAANZA KUTANGAZA SHEREHE ZA BIRTHDAY ZA WANAO NA KUFANYIA UKUMBINI KWA GHARAMA KUBWA SANA!!!
 
Kama unataka msaada wa kweli njoo pm
 
Ukiona mtu anakuitia fursa isiyoeleweka ujue we ndo fursa..,hv hiki kipindi wachimbaji wanavyolalamika kweli uache kazi we mshahara permanent uende cheza kamari migodini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…