Nataka kuacha kazi .

Nataka kuacha kazi .

Hayo ni mapito tu,Maisha yetu yalivyo ni kama uonavyo season za vipindi vya majira katika mandhari zetu kama kuna kipindi cha joto,Masika,vumilia maisha ndivyo yalivyo,Na pia kama unauwezo jaribu kutafuta mume uolewe huenda mawazo yakakupungikia
Mie nahangaika na maisha wanambia habari za kutafuta mume kweli?bahati mbaya wanaume naowapata wanakuwa hawana msaada Zaid wananiona fursa
 
Pole sana, Usifikirie kuacha kazi kabla hujafahamu utaenda kufanya nn cha kukupatia kipato hata biashara nazo haziendi sawa kipindi hiki, heri uendelee kushikilia hapo ulipo..
 
Uza vyote ulivyonavyo nenda machimboni mfano Chunya,Mererani au Geita fungua mgahawa au biashara ndogo ndogo trust me utatoboa.
Kabla ya kwenda huko nakushauri waache watoto kwa ndugu japo mwezi mmoja mambo yakikaa sawa unaweza kuwachukua na kwenda kuishi nao.
Nina experience na kitu nilichokushauri.
Afterall, POLE SANA.
 
Hayo unayotaka kufanya ningekuunga mkono kama usingekuwa na watoto. Ila na hao watoto mwenzangu vumilia tafuta hata kabiashara. Huko kazini unakoenda waweza kuwa unawauzia vitafunwa au tafuta shughuli nyingine ya kukuingizia kipato kwa mfano waweza kujifunza kushona n.k
 
Habari za asubuhi wana jukwaa.

Mie ni mtumishi wa umma na niliajiriwa mwaka 2013.Nina watoto wawili wa kiume,Nina viwanja vitatu ambapo kimoja nimejenga nyumba iliyoishia kwenye linta.

Toka aingie mkulu maisha yamekuwa magumu Sana,si furahii kazi yangu hata kidogo naenda tu kazini kuonekana nipo.Na siyo kuwa ni mpiga madili Wala,zamani tulikuwa tunapata hata viextra duty vinatuboost mwezi unaisha,ila saivi Nina mwaka wa tatu siijui posho.Tulikuwa tunaenda kazini hadi jmos angalau tupate chochote tulishe family.

Nimejaribu kuuza kiwanja kimoja at least nimalizie nyumba nihamie,manake Kodi inanitesa Sana huku nilikopanga ila nimekosa mteja.wanangu wanasoma mmoja baby class na mwingine class one.Bado mfanyakazi kumlipa hapo hujasaidia ndugu wanao ona nalipwa mamilioni ilihali mwisho wa mwezi napokea laki mbili na ishirini(220,000) ambayo haikidhi mahitaj yote.

Am a single parent kwahiyo mimi ndiyo baba na mama kwa wanangu.Baba yao tuliachana akaoa,na alitaka wachukua watoto ila sikuwa tayari kuacha wanangu wa under 7 years walelewe na mama wa kambo,hivyo kawasusa hatoi hata Senti tano kwaajili yao,so am their only hope.

Naona napoteza muda,nimeshafikiria hata kujirusha ghorofan ili nitoweke duniani ila nikiwafikiria wanangu roho inauma naona sitawatendea haki.So nimewaza nikaona si bora niache kazi,niuze Kila nilichonacho ingawa wateja wanakuwa tabu,nihame mji,nende sehemu nyingine nikaanze upya.Nimewaza pia kufanya nite business at least watoto wale na nipate Kodi ya nyumba,sema dhamira inakataa.

Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.

Naombeni ushauri wadau nifanyeje?je niache kazi?then niende wapi ama nifanye Nini baada ya kuacha kazi,Ningekuwa Sina watoto ningeshaondoka kitambo,tatizo mustakabali wa maisha ya wanangu utakuwaje,nikiwaza Hilo nachoka,naishia kumwaga machozi kama mtoto.
Pole Sana dada ila husiache kazi kama huna other viable options, mtafute huyo Baba watoto wako awe anakusaidia Ada ya shule , mpe akaunti namba ya shule
 
Utakaposhinda majaribu uliyonayo sasa ndipo utakapokuwa imara zaidi! Hauna alternative nyingine baada ya kuacha kazi nakushauri uendelee huku ukijitahidi kubana matumizi kwa iendane na kipato ulichonacho
 
Una tatizo kubwa la kisaikolojia kuliko la kikazi. Tsh 220K kwa mwezi kweli ni kipato kidogo lakini hakika nakuambia zaidi ya watanzania 85% hawana uhakika na kipato hicho mwisho wa mwezi, lakina hawajakata tamaa na hawajui watafarijika lini.

Tiba ya tatizo lako, kwanya ni:
- Kukubali kulea wanao, mtoe kabisa akilini mzazi mwenzio, pili jaribu kuangalia ni wapi unaweza kupunguza matumizi yako yanayoweza kuepukika, tatu unachokiona ni tatizo kwa sasa ni masuala ya muda tu na soon yataisha kwa kuwa ni upepo tu wa kisiasa hivyo usikutoe relini.

Kwa kuwa stage ya maisha uliyopo kama mtumishi wa umma wa kawaida siyo mbaya sana.
Kwenye hiyo 220k,toa 100k Kila mwezi ya ada za watoto,inabaki,120k,hujanunua chakula,maji na matumizi mengineyo ya nyumbani,hapo hakuna hata nguo mpya kumbuka

Jamaa nilishamtoa akilini manake nilimsihi Sana anisaidie,akawa anasema atatuma ila akawa hatoi,so nikaacha kumwomba
Hali ni ngumu sana,bado Kodi ya nyumba,inakatisha tamaa kwakwel
 
Mie nahangaika na maisha wanambia habari za kutafuta mume kweli?bahati mbaya wanaume naowapata wanakuwa hawana msaada Zaid wananiona fursa
Nitafute nikushauri
.Mini ni mhanga Kama wewe.Najua ulikopa Bank ukitegemea kurenew mikopo na ulitegemea mishahara kupanda.Nicheki 0787938347
 
Kuna faida kuonekana wafanya kazi serikalini ilhali kuna wakati walala njaa na watoto?Sina sifa za kukopesheka,yani naona nilipoteza muda hata kuhangaika na shule Kama matokeo yake ndio haya.
Hebu hao watoto wapeleke kwa baba yao kwanza. Umaskini jeuri hauna mwisho mzuri. Unapowang'ang'ania eti unamwogopa mwanamke mwenzio ulishawahi kuwaza unaweza kudedi wakati wowote na hao watoto wakalelewa na huyuhuyo mama wa kambo??

Kwanini wanawake hamuaminiani namna hii? Kwanini hampendani?

Pole kwa wanayokusibu ila nakushauri usiache kazi kabla hujapata mbadala wa kukuingizia kipato.

BTW hujapata buzi la kukupunguza nyege? Nyege zikizidi huleta hasira na mawazo ya kijinga kabisa. Ndo maana unawaza hata kujiua au kufanya biashara za usiku

Swali la kizushi: Nini kilifanya ndoa yako ivunjike?
 
Kwenye hiyo 220k,toa 100k Kila mwezi ya ada za watoto,inabaki,120k,hujanunua chakula,maji na matumizi mengineyo ya nyumbani,hapo hakuna hata nguo mpya kumbuka
Jamaa nilishamtoa akilini manake nilimsihi Sana anisaidie,akawa anasema atatuma ila akawa hatoi,so nikaacha kumwomba
Hali ni ngumu sana,bado Kodi ya nyumba,inakatisha tamaa kwakwel
Vipi ukihamia hata chumba kimoja karibu na kazini ukapunguza matumizi ya nauli na nguo ukawa unanunua hata kila baada ya miezi 3 bila kujali watu watasemaje maana ofisi zetu tunazijua ?

Kumbuka wewe ndio unajua uko katika hali gani, usilazimishe kujionesha kwa public mambo mazuri wakati unaumia maana utaharibikiwa zaidi.

Finally utakuja kugundua hakuna anaejali sana kuhusu unaishi vipi na hata kama yupo anaweza kuwa ana matatizo makubwa kuliko wewe.
 
Nakushauri usiache kazi. Kabla hujajua cha kufanya.
Nakushauri siku ya jmosi nenda masokoo makukuu nunua nguo ambazo unaona ni nzuri na zinaenda na wakati. Jaribu kutumia CM yako hiyohiyo kuuzia watu Pamoja na Kazini kwako.
Ukijituma kwa hivyo angalau itakusaidia kidogo. Usikate tamaa
 
Pole Sana dada ila husiache kazi kama huna other viable options, mtafute huyo Baba watoto wako awe anakusaidia Ada ya shule , mpe akaunti namba ya shule
Nishampatia kitambo anakujibu atalipa ila hatoi na hajawahi toa hata mia yake
Juzi hapa walipofunga shule nikamtumia akaunti ya shule akasema atalipa,ila hadi leo wanangu wana wiki ya pili shuleni hajalipa,ilibid nikalipe tu mwenyewe
 
Back
Top Bottom