Nataka kuacha kazi .

Nataka kuacha kazi .

Habari za asubuhi wana jukwaa.

Mie ni mtumishi wa umma na niliajiriwa mwaka 2013.Nina watoto wawili wa kiume,Nina viwanja vitatu ambapo kimoja nimejenga nyumba iliyoishia kwenye linta.

Toka aingie mkulu maisha yamekuwa magumu Sana,si furahii kazi yangu hata kidogo naenda tu kazini kuonekana nipo.Na siyo kuwa ni mpiga madili Wala,zamani tulikuwa tunapata hata viextra duty vinatuboost mwezi unaisha,ila saivi Nina mwaka wa tatu siijui posho.Tulikuwa tunaenda kazini hadi jmos angalau tupate chochote tulishe family.

Nimejaribu kuuza kiwanja kimoja at least nimalizie nyumba nihamie,manake Kodi inanitesa Sana huku nilikopanga ila nimekosa mteja.wanangu wanasoma mmoja baby class na mwingine class one.Bado mfanyakazi kumlipa hapo hujasaidia ndugu wanao ona nalipwa mamilioni ilihali mwisho wa mwezi napokea laki mbili na ishirini(220,000) ambayo haikidhi mahitaj yote.

Am a single parent kwahiyo mimi ndiyo baba na mama kwa wanangu.Baba yao tuliachana akaoa,na alitaka wachukua watoto ila sikuwa tayari kuacha wanangu wa under 7 years walelewe na mama wa kambo,hivyo kawasusa hatoi hata Senti tano kwaajili yao,so am their only hope.

Naona napoteza muda,nimeshafikiria hata kujirusha ghorofan ili nitoweke duniani ila nikiwafikiria wanangu roho inauma naona sitawatendea haki.So nimewaza nikaona si bora niache kazi,niuze Kila nilichonacho ingawa wateja wanakuwa tabu,nihame mji,nende sehemu nyingine nikaanze upya.Nimewaza pia kufanya nite business at least watoto wale na nipate Kodi ya nyumba,sema dhamira inakataa.

Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.

Naombeni ushauri wadau nifanyeje?je niache kazi?then niende wapi ama nifanye Nini baada ya kuacha kazi,Ningekuwa Sina watoto ningeshaondoka kitambo,tatizo mustakabali wa maisha ya wanangu utakuwaje,nikiwaza Hilo nachoka,naishia kumwaga machozi kama mtoto.
Pole sana, Usikate tamaa hata kidogo hii hali inapita ,mawazo ya kujiua sio solution kabisa jaribu kutafuta watu wakupe ushauri wa kiroho, Mimi nakushauri mpe Yesu maisha yako yeye atakupa neema ya kipekee sana, Usiwaze tena kujiua kabisa ni dhambi lakini pia ukifa kwa njia hiyo lazima jehanamu inakungoja. Issue ya viwanja ni vizuri ukasema viko wapi na ukubwa gani.
Nakuombea Mungu akupitishe salama,
Hajalishi giza nene namna gani asubuhi yako inakuja.
Mwisho jitahidi kusamehe yote na wewe utasamehewa.
 
Sorry kama ntakuudhi lkn huu ndiyo ukweli:
Unaonekana mjuaji sana, una tamaa ya mambo makubwa, una hasira na hushauriki! Bilashaka ndiyomaana mzazi mwenzio mlishindwana.
Rekebisha kwanza hayo mapungufu yako then utaona maisha yako yatakavyobadilika.
Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
 
Je,uliwahi kuwa na kampuni?,baki na kazi yako huku unatafuta fursa nyingine,....anza kuishi Low profile,usiendelee kujilazimisha kuishi maisha ambayo yanakula kipato chako.
Sio wewe tu unaekutana na hizo changamoto ni wengi sana!
USHAURI WANGU;
1.USiache kazi,utakuja juta sana,vile vitabu vya acha kazi ufanye biashara havi apply katika mazingira yetu tulio nayo.. it's very hard to get new job nowadays
2.Hama unapoishi,nenda pembezoni kidogo ya mji palipo na usafiri,kapange vyumba vichache
3.Ondoa watoto hizo shule za garama,mimi wa kwangu alikua anasoma hizo shule za private ada mlima nilimuondoa nikampeleka za serikali,saa hizi nalipa pesa tu ya tuition kwa mwezi elfu kumi,ila sijalipa mwezi wa tatu sasa na bado anasoma
4.Katika mtu mmoja aliefanikiwa kibiashara kuna watu 1000 waliofeli,so jitafakari na usiache kazi
5.Sikiliza moyo wako and Listen to people but take your own decisions
Hapo kwenye kufungua kampuni inampasa awe makini zaidi...ajifunze kwanza kwa kina kuhusiana na kile anachotaka kukifanya ndipo aingie.
 
Kuna faida kuonekana wafanya kazi serikalini ilhali kuna wakati walala njaa na watoto?Sina sifa za kukopesheka,yani naona nilipoteza muda hata kuhangaika na shule Kama matokeo yake ndio haya.
Usiache kazi kama huna mbadala wake wa uhakika, ukiacha kazi ndio utajua kuwa kazi ilikuwa inakusaidia
Pengine unaishi maisha ya juu kuliko kipato, tafuta nyumba ya bei rahisi, watoto wapeleke shule za serikali kama wapo private
Laki 2.2 unaweza ku survive nayo tu hadi mambo yatakapokuwa mazuri

Mimi nina ndugu yangu kasota Chuo Kikuu na hana kazi ya kumuingizia hiyo laki 2.2 tangia mwaka 2013, una afadhali kuliko watu wengi ndugu
 
M nakushauri usiache kazi nikuhakikishie hata hapa dar lak mbili hyo unayoipata unaeza kuishi wakat ukiangalia namna ya kufanya ila ukisema kuacha kaz mama yangu wakat huna kitu kilochosimam utapata shda sana kikubwa ishi kulingana na uwezo wako usiishi kwa kuangalia watu watakuonaje
 
We siyo dalali wa viwanja kweli!!? Maana unashauriwa mambo ya maana unang'ang'ania tu kuuza viwanja!!!!!
Jamani shtukeni, hili ni tagazo la viwanja.
Kila lakheri.
Doh hahahah
Mara useme udalali was viwanja,Mara sishauriki,Mara mjuaji,sijui jamaa nilishindwana naye,btw yeye si hoja ya mada yangu,Nina miaka sijawah kula hata Senti yake so he is not an issue here inshort haexist he was just a sperm donor
Hapa natafuta mbinu ya kusurvive na wanangu
Isitoshe it's not a sin kudream big kama ndoto zako ndogo poleee
Sorry to burst your bubble dude
 
Usiache kazi kama huna mbadala wake wa uhakika, ukiacha kazi ndio utajua kuwa kazi ilikuwa inakusaidia
Pengine unaishi maisha ya juu kuliko kipato, tafuta nyumba ya bei rahisi, watoto wapeleke shule za serikali kama wapo private
Laki 2.2 unaweza ku survive nayo tu hadi mambo yatakapokuwa mazuri

Mimi nina ndugu yangu kasota Chuo Kikuu na hana kazi ya kumuingizia hiyo laki 2.2 tangia mwaka 2013, una afadhali kuliko watu wengi ndugu
Ok shukrani anyway
 
Pole sana, Usikate tamaa hata kidogo hii hali inapita ,mawazo ya kujiua sio solution kabisa jaribu kutafuta watu wakupe ushauri wa kiroho, Mimi nakushauri mpe Yesu maisha yako yeye atakupa neema ya kipekee sana, Usiwaze tena kujiua kabisa ni dhambi lakini pia ukifa kwa njia hiyo lazima jehanamu inakungoja. Issue ya viwanja ni vizuri ukasema viko wapi na ukubwa gani.
Nakuombea Mungu akupitishe salama,
Hajalishi giza nene namna gani asubuhi yako inakuja.
Mwisho jitahidi kusamehe yote na wewe utasamehewa.
Shukran,ila siwez sema viko wapi manake nishaambiwa nafanya udalali
Ntazingatia ushauri wako wa kiroho
 
Mtumishi wa Umma ndugu usijiue, shukuru kwa kila jambo. Endelea kupambana kutafuta mteja wa kiwanja umalizie nyumba hata kama utamalizia chumba kimoja.
Pia watoto wapeleke elimu bwerere huku unaendelea kujipanga, haya maisha hayajawahi kuwa rahisi.
Mwisho kabisa tafuta mwenza itapunguza uzito wa mawazo.
Shukran ila sihitaji mwenza kwasasa
Sitaki kuongeza mzigo wa majukumu ya watoto ilhal hawa wawil bado sijakaa sawa
 
Kama ni kazi ya serikali punguza mda na siku za kwenda kazini utafute shughuri zingine hata ya kuhudumia kuku
 
Ni ya serikali
Tatizo nilikuwa najaribu kufanya hivyo,sema mkuu wa idara mnoko kila leo akawa ananisema kwenye vikao na kutishia kuniripot so nikaacha
Kama ni kazi ya serikali punguza mda na siku za kwenda kazini utafute shughuri zingine hata ya kuhudumia kuku
 
Ubishi, Ubishi, Ubishi, Ujuaji + tamaa
Hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia.
We kajiuze tu maana uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo!
 
Ubishi, Ubishi, Ubishi, Ujuaji + tamaa
Hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia.
Sawa nimekubali but mbona umekomalia thread yangu?hakuna thread zingine ukoment?
Isitoshe sijataka univumilie wala sijafungua thread ya mwanaume kunivumilia
Kama nakukera tafuta nyuzi zingine hate msiba wa Mzee Mengi ukachangie,huyu mbishi mwache huwezi mfanya utakavyo wewe kwani yeye ni raia huru mwenye Uhuru wa kufungua uzi humu muhimu tu asivunje kanuni
 
Back
Top Bottom