Nataka kuacha kazi .

Nataka kuacha kazi .

Nahisi nikiacha kazi nitapata msukumo wa kujua Cha kufanya
Kazini napoteza muda tu kiukwel
Nina mpango wa kufungua kampuni,nishaandaa Hadi momerandum,nahangaikia kuisajil tu
Then nijitose,huenda nikikosa hata hiyo 220k nitapata akil Zaid na hasira ya kufanya vizuri zaid
ACHA KAZI.
 
Teh teh teh wangejua nimepigika hadi najichukia,naichukia hata kazi yangu
Laiti ningalijua nisingeajiriwa serikalin,nilikuwa private Kwa mwaka mmoja ,walipotangaza ajira kiherehere nikajitosa,kumbe naingia pori la miiba
Halafu plot zenyewe ni potential sema hamna wanunuzi,kimoja Cha makazi nilichojenga,kingine nilipanga kujenga mjengo wa kustaafia sema naona dream zi ebadilika na upepo,na Cha mwisho ni industrial plot hiki,nilipanga nipate mwekezaj tuingie partinership sema disko limeingia mmasai.
Ukiacha Kazi Ndo Utauza Mbunye Vizuri.


ACHA KAZI

ACHA KAZI

ACHA KAZI

ACHA KAZI

ACHA KAZI
 
No kabla bodi hawajaanza nikata nilikuwa napokea kiasi kinachokidhi matumizi ya nyumbani,walipoanza kunikata ndipo tatizo lilianza,manake nililetewa Deni la tshs mil 18 Kwa miaka 4 niliyokuwa chuo kwani nilipata mkopo 100%.
Ulisoma kozi gani miaka 4?
 
Yaani hata muda wa kujibu watu hapa ungekuwa unautumia kufanya mambo mengine lakini umekaa kujibu kila MTU ili umridhishe.


JIUE KWANZA HALAFU NDO UACHE KAZI
 
Pole sana, hayo n mapito. Napenda kukushauri yafuatayo:
1. Usiache kazi kwa sasa kwan huna njia mbadala, ya kupata kipato.
2. Ishi ktk uwezo wako; watoto somesha shule za kawaida kwa sasa. Panga nyumba ya uwezo wako sasa
3. Nenda Ustawi wa jamii. Mtapata ufumbuzi wewe na mzazi mwenzio ktk malezi ya watoto.

NB: pesa iliyo mfukoni mwako, ndo yako.
 
Habari za asubuhi wana jukwaa.

Mie ni mtumishi wa umma na niliajiriwa mwaka 2013.Nina watoto wawili wa kiume,Nina viwanja vitatu ambapo kimoja nimejenga nyumba iliyoishia kwenye linta.

Toka aingie mkulu maisha yamekuwa magumu Sana,si furahii kazi yangu hata kidogo naenda tu kazini kuonekana nipo.Na siyo kuwa ni mpiga madili Wala,zamani tulikuwa tunapata hata viextra duty vinatuboost mwezi unaisha,ila saivi Nina mwaka wa tatu siijui posho.Tulikuwa tunaenda kazini hadi jmos angalau tupate chochote tulishe family.

Nimejaribu kuuza kiwanja kimoja at least nimalizie nyumba nihamie,manake Kodi inanitesa Sana huku nilikopanga ila nimekosa mteja.wanangu wanasoma mmoja baby class na mwingine class one.Bado mfanyakazi kumlipa hapo hujasaidia ndugu wanao ona nalipwa mamilioni ilihali mwisho wa mwezi napokea laki mbili na ishirini(220,000) ambayo haikidhi mahitaj yote.

Am a single parent kwahiyo mimi ndiyo baba na mama kwa wanangu.Baba yao tuliachana akaoa,na alitaka wachukua watoto ila sikuwa tayari kuacha wanangu wa under 7 years walelewe na mama wa kambo,hivyo kawasusa hatoi hata Senti tano kwaajili yao,so am their only hope.

Naona napoteza muda,nimeshafikiria hata kujirusha ghorofan ili nitoweke duniani ila nikiwafikiria wanangu roho inauma naona sitawatendea haki.So nimewaza nikaona si bora niache kazi,niuze Kila nilichonacho ingawa wateja wanakuwa tabu,nihame mji,nende sehemu nyingine nikaanze upya.Nimewaza pia kufanya nite business at least watoto wale na nipate Kodi ya nyumba,sema dhamira inakataa.

Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.

Naombeni ushauri wadau nifanyeje?je niache kazi?then niende wapi ama nifanye Nini baada ya kuacha kazi,Ningekuwa Sina watoto ningeshaondoka kitambo,tatizo mustakabali wa maisha ya wanangu utakuwaje,nikiwaza Hilo nachoka,naishia kumwaga machozi kama mtoto.
Pole sana dada mimi nakushauri usiache kazi, mambo magumu sio wewe tu tuko wengi mimi ni mmoja wapo ukiacha kama huna kitu kingine cha kufanya yaani unategemea kuanza itakupa shida na watoto, haya mambo ni ya muda tu yataisha nashauri uvumilie tu., miaka 5 sio mingi.
 
Kwanza kabisa nakupa ongera kwa maamuzi ambayo unayafikiria kuyafanya ni sahihi kabisa kwa wakati huu.
Kesho yetu inajengwa na leo.Tatizo wengi wetu tupo ndani ya comfort zone hivyo mawazo ya kuacha kazi tunaona ni magumu na hayawezekani kitu ambacho si kweli,kila kitu/jambo linaanzia kwenye mind and then unalifanyia implementations.
Financial freedom is only for those whose dare to step out of comfort zone.Not so easy to step out of comfort zone, really scaring and disturbing the mind. But once you step out of that zone,you will be free.
IMG_2644.JPG
.Nakushauri hakuna wakati mwengine sahihi wa ku act maamuzi yako kama sasa.Maamuzi ya kuacha kazi ni moja ya maamuzi magumu yanayohitaji ujasiri na ujiamini zaidi lakini unapoelekea katika maamuzi hayo lazima uwe na tahadhari ili usiyumbe yumbe katika safari yako.Sitokuambia kuwa don’t take risks ila nitakuambia how to minimize risks.

1)Ishi kulingana na kipato chako ikiwezekana punguza matumizi yasiyo ya lazima.
Ukiwa Unajiandaa na safari ya kuacha kazi hili ni moja ya suala muhimu sana.Jaribu kubana matumizi yasiyo na umuhimu.Wanawake wengi mnakuwa na matumizi mengi ambayo hayana ulazima sana ukiyaacha hautaathirika.Hii inafaida kwani zile pesa ambazo ulikuwa unatumia kwa matumizi haya zinabaki hivyo Utaweza kuwa na extra money in your pocket.

2)Buy assets and not liabilities.
Hadi sasa huwa najiuliza kwanini somo linalohusiana na pesa halifundishwi katika shule zetu.Kwanini lisiwekwe katika mtaala wetu wa elimu.
Katika post yako nilichojifunza kuwa wakati unachukuwa mkopo haukujuwa nini cha kufanya pindi umepata mkopo,hivyo uliishia kununua liabilities ambazo sasa zinakutesa.Pesa nyingi uliishia kununua viwanja na kufanya matumizi yasiyo na ulazima ukiwa na mategemeo kuwa viwanja utaviuza kwa bei nzuri,kitu ambacho sio kweli.
We learn through the mistakes we make.Hilo liwe funzo kwako katika safari hii ya ujasiriamali.Huku usinunue vitu ambavyo haviingizi pesa labda viwe kama rewards from your assets.

3)Mind preparation.
Hii ndo ilitakiwa iwe namba moja.Jiandae kiakili na kisaikolijia zaidi katika safari hii ndefu lakini yenye amani na tumaini huko mbele.Watu wengi watakushangaa,watakuzarau,watakucheka,kama hapa jukwaani lakini usikubali kuyumbishwa na hizo kelele za nje.

4)Uza liabilities ili upate mtaji wa kuanza ujasiriamali.
Tafuta broker wa viwanja hapo Dar ili wakuuzie viwanja.Offer them kiasi kizuri cha pesa pindi wakifanikiwa kukuuzia hivyo viwanja vyako.
Wateja wapo ila tatizo unaweza kuwafikia huko walipo?
Jibu hauwezi kuwafikia hivyo tafuta wakala nzuri wa viwanja mpe ahadi nzuri ya malipo kama atafanikiwa kuuza hivyo viwanja.I assure you.Vinauzika.Lakini pia kama una liabilities zingine ambazo hazina faida ila hasara mi nakushauri uza ili upate acces Money.

5)Tafuta mentor aliyefanikiwa na soma vitabu vya ujasiriamali.
By standing on the shoulder of the Giants.Waliofika juu hajafika wenyewe kwa juhudi zao never,walishikwa mkono na waliotangulia kabla yao ambao walianza safari hii mapema sana.
Angalia ni biashara gani ambayo unaona inakufaa and then tafuta mtu/watu sahihi wa ku share nao mawazo yako lakini pia watakupa ups n down ya biashara hiyo.Take note.Sio kila mtu anafaa.
Lakini soma sana vitabu vya ujasiriamali hii itakusaidia kukuongezea maarifa na knowledge zaidi.the richest man in the Babylon .
NOTE.Meli inakuwa salama zaidi inapokuwa nchi kavu.Tatizo haijatengenezwa kukaa nchi kavu.
 
Kwanza pole usiache kazi mapipo tu.upo mkoa gani nikushauri biashara ya kufanya uku ukiwa unafanya kazi
 
Usitegemee kipato cha serikali unakufa masikini.uza uwanja mmoja fungua biashara.niambie upo mkoa gani ntakuambia ufanye biashara.usifikirie kufa kisa maisha mungu akutie moyo wa ujasiri
 
Nahisi nikiacha kazi nitapata msukumo wa kujua Cha kufanya
Kazini napoteza muda tu kiukwel
Nina mpango wa kufungua kampuni,nishaandaa Hadi momerandum,nahangaikia kuisajil tu
Then nijitose,huenda nikikosa hata hiyo 220k nitapata akil Zaid na hasira ya kufanya vizuri zaid
Kampuni gani dada? Ujenzi? Kama ndio basi inabidi upate ofisi, water bowser , gari n.k
Naona washauri wengi wanakushauri juu ya kuwapeleka watoto shule za kawaida, lakini hili bado hujakubaliana nalo, hata sisi tulisoma kayumba na wengine waliosoma huko wote tulikutana chuoni,
Peleka watoto kayumba ila hakikisha jioni unasimamia nini wamesoma n.k,
Kuhusu mkopo wa bodi hata sisi wengine tunadaiwa kiasi hicho hicho 18m hivyo no way out lazima bodi wakate chao
Usiache kazi dada, hebu jaribu kuonana na baba watoto ana kwa ana huenda mambo yatabadilika maana maongezi ya simu hayana nguvu kubwa,
Mueleze hali halisi ikibidi watoto awachukue au aende na mmoja kukupunguzia mzigo
 
Umesema unakiwanja Fanya hivi kisaminishe benki wakupe mkopo harafu usirufishe mkopo hata wakija kupiga bei hicho kiwanja huna haja nacho
Hahahaha, mkuu pitia tena thread maana mtoa maada ana mikopo miwili, bodi na huo mwingine
 
usiache kazi, utadhalilika zaidi nashauri uendelee na kaihuku ukitengeneza namna nyingine kama kujiajiri nk ni ngumu sana kupata kazi ya serikali, kazi za watu binafsi watu wanadhalilika zaidi kuliko za serikali
Kujiajiri wapi? Jaribu kuingia hoteli nyingine zinauza vyakula viporo; vyakula haviishi wanalaza. Biashara yenye unafuu labda baa angalau kila chupa unayofungua kuna vishilingi umejiongezea
 
Kujiajiri wapi? Jaribu kuingia hoteli nyingine zinauza vyakula viporo; vyakula haviishi wanalaza. Biashara yenye unafuu labda baa angalau kila chupa unayofungua kuna vishilingi umejiongezea
sikumsupport aache kazi aende akajiajiri, kulingana na risk kama hizo, piahata kama i kwenye ajira akute anajaribu nje ya box! ila umeandika kwa specific evidence, mkuu utakuwa una hotel au baa naomba kazi mm sina kazi
 
sikumsupport aache kazi aende akajiajiri, kulingana na risk kama hizo, piahata kama i kwenye ajira akute anajaribu nje ya box! ila umeandika kwa specific evidence, mkuu utakuwa una hotel au baa naomba kazi mm sina kazi
Napataga chakula cha mchana; kwa uzoefu wangu ndani ya wiki moja nimelishwa viporo hotel nne tofauti; nakula leo nagundua ni kiporo nahamie ingine nalishwa kipo hadi sasa nakula nyama choma au nashindia karanga. Hali si hali na afya yangu hainiruhusu kila chips ambazo kwa kiasi fulani ni fresh kuliko vyakula vya kwenye sufuria
 
Back
Top Bottom