Dumelang
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 3,267
- 5,854
Kuna makosa ulifanya maishani na ndio wanayofanya wengi wetu.Kiwanja ni mil 8,ila kiuhalisia Bei yake ni mil 15 hadi 12
Niko dsm hapa wanapojenga barabara ya njia 8, lifestyle nishabadil kitambo tatizo Kila leo afadhal ya jana
1. Ulichukua mkopo ukaweka kwenye liability. Wapo watu watasema hapa nyumba na viwanja ni asset. Ila niamini mimi vyote ulivyonavyo kwasasa ni liability maana havikuingizii chochote na vimebaki kuwa mzigo kwako kwakuwa havijakusaidia hata kutoka katika situation unayolia nayo sasa.
Sasa unataka kuacha kazi kwasababu unapokea 20k ambayo haitoshi, unakoenda unaweza tengeneza zaidi ya laki 2 kila mwezi ukaishi? Au ndio itakulazimu kwenda kwenye night busines?
Be serious mie mwenyewe nimekuwa mtumishi wa serikali na baada ya bodi nilikuwa nabaki na 180k. Na ni mwanaume, nionge, nile, nilipe kodi niendeshe maisha ya kila siku pamoja na ndugu. Sikukaa tamaa, nilifanya mpk biashara ambazo degree yangu ilibdi ifichwe uvunguni.
Mkopo niliokuwa nimechukua ulikufa siku moja, mwezi mmoja baada ya kuuwekeza, can u imagine the situation nilikuwa nayo?
Sikutaka kuacha kazi katika kipind hiko, lakin nia ilikuwa siku moja naacha kuwa mwajiriwa. Na nilianza kazi mwaka mmoja na wewe 2013. I tell u ndoto ilitimia. Tangu mwaka huu uanze Rasmi sipo kazini. Nafanya maisha yangu na kipato changu kwa wiki ni zaidi ya hiyo pesa niliokuwa napewa kwa mwezi. Na nnasonga.
Hivyo, usiache kazi ila tafta kitakachokuwa nguzo ukiacha kazi.
2. Umesema upo dar, hivi kweli dar unakosa kazi ya ziada ya kuzalisha cha ziada. Nawashangaaga sana wakazi wa mji huu. Mimi nikiingiaga hapa nafanya kazi napata pesa mpk najishangaa. Maana kila kitu dar ni fursa hata kuuza tu utumbo wa kuku


Unafeli wapi sasa?
3. Kwakuwa una liability zisizozalisha, zigeuze kuwa asset. Liability zako zote zinaweza geuzwa kuwa asset, unafeli wapi?
Unasema unaanzisha sasa kampuni, duuh nimejiuliza na sijui upo hapa ku joke? Yan huna ela, then uanzishe kampuni

unaanzisha na nini? Kampuni zitalipiwa kodi, utalipa na nini? Napata picha ya kuona unapenda mambo makuu kabla ya kumaliza madogo, na unafanya mambo bila hesabu nyingi thats y una viwanja viwili na pagale na bado ulipanga kuuza kiwanja umalizie pagale lako. Hatari kabisa hii.Jaribu kubadili watu wanaokushauri. Ama jinsinunavyojishauri

think clear always.Mwisho nikutakie kila la heri. Katika ushauri wangu fanyia kazi dots nilizoweka, najua nnachoongea na nmekuwa mtumishi na mwenye mshahara wenye makato na bank, na bodi, tena niliepitia majanga makubwa. Lakini nimepenya.
Kila la heri.

