Nataka kuacha kazi .

Nataka kuacha kazi .

Ki ukweli hawamu hii watu wengi wanakufa kwa msongo wa mawazo na ndiyo maana kuna ongezeko la misiba mingi sana kwa sababu ya waTz wanatikisika kinamna yake si mfanyabiashara,si mtumishi wa Mungu,si mtumishi wa umma wote wapo hoi.
Habari za asubuhi wana jukwaa.

Mie ni mtumishi wa umma na niliajiriwa mwaka 2013.Nina watoto wawili wa kiume,Nina viwanja vitatu ambapo kimoja nimejenga nyumba iliyoishia kwenye linta.

Toka aingie mkulu maisha yamekuwa magumu Sana,si furahii kazi yangu hata kidogo naenda tu kazini kuonekana nipo.Na siyo kuwa ni mpiga madili Wala,zamani tulikuwa tunapata hata viextra duty vinatuboost mwezi unaisha,ila saivi Nina mwaka wa tatu siijui posho.Tulikuwa tunaenda kazini hadi jmos angalau tupate chochote tulishe family.

Nimejaribu kuuza kiwanja kimoja at least nimalizie nyumba nihamie,manake Kodi inanitesa Sana huku nilikopanga ila nimekosa mteja.wanangu wanasoma mmoja baby class na mwingine class one.Bado mfanyakazi kumlipa hapo hujasaidia ndugu wanao ona nalipwa mamilioni ilihali mwisho wa mwezi napokea laki mbili na ishirini(220,000) ambayo haikidhi mahitaj yote.

Am a single parent kwahiyo mimi ndiyo baba na mama kwa wanangu.Baba yao tuliachana akaoa,na alitaka wachukua watoto ila sikuwa tayari kuacha wanangu wa under 7 years walelewe na mama wa kambo,hivyo kawasusa hatoi hata Senti tano kwaajili yao,so am their only hope.

Naona napoteza muda,nimeshafikiria hata kujirusha ghorofan ili nitoweke duniani ila nikiwafikiria wanangu roho inauma naona sitawatendea haki.So nimewaza nikaona si bora niache kazi,niuze Kila nilichonacho ingawa wateja wanakuwa tabu,nihame mji,nende sehemu nyingine nikaanze upya.Nimewaza pia kufanya nite business at least watoto wale na nipate Kodi ya nyumba,sema dhamira inakataa.

Mkuu hata Kama tulikuudhi tusamehe,tunadhalilika na familia zinateseka.Binafsi sioni faida ya kuitwa mtumishi wa umma ilhali Kuna wakati nakosa hadi nauli ya daladala kwenda kazini.Pia toka nimeajiriwa sijawahi panda cheo.

Naombeni ushauri wadau nifanyeje?je niache kazi?then niende wapi ama nifanye Nini baada ya kuacha kazi,Ningekuwa Sina watoto ningeshaondoka kitambo,tatizo mustakabali wa maisha ya wanangu utakuwaje,nikiwaza Hilo nachoka,naishia kumwaga machozi kama mtoto.
 
Huu uzi pm zitakuwa nyingi sana ..wapenda miteremko tunawaona tu
Teh teh teh wangejua nimepigika hadi najichukia,naichukia hata kazi yangu
Laiti ningalijua nisingeajiriwa serikalin,nilikuwa private Kwa mwaka mmoja ,walipotangaza ajira kiherehere nikajitosa,kumbe naingia pori la miiba
Halafu plot zenyewe ni potential sema hamna wanunuzi,kimoja Cha makazi nilichojenga,kingine nilipanga kujenga mjengo wa kustaafia sema naona dream zi ebadilika na upepo,na Cha mwisho ni industrial plot hiki,nilipanga nipate mwekezaj tuingie partinership sema disko limeingia mmasai.
 
Una kipindi kigumu kama changu.
2016 September nilikopa 10 millions, million moja nikaitumia kwa family matters, million 6 nikapata viwanja 2 na 3 million nikafungua duka na likafa au nikaliua baada ya kuona linanitesa, yaani Mimi nikageuka kulihudumia badala ya kunihudumia .
Ila sasa nakopesheka ingawa si hela nyingi, nilipitia kipindi kigumu sana mpaka nilipanga chumba cha elfu 30 kwa mwezi hapa dar ilhali nina familia.
Sasa napumua Mungu kanifungulia mlango mwingine naishi kwa uhuru kiasi.
Pole, jipe moyo yatapita.
Ushauri:Mtafute dalali auze kiwanja chako kimoja kwa bei ya shiida kisha fungua biashara za contracts kama bodaboda, saloon za kiume n.k
Hapa namaanisha msimamizi utakubaliana naye akuletee fixed amount kila wiki au siku.
Awamu hii kuna biashara usithubutu kuzifanya kama hutoweza kusimamia mwenyewe 24 hrs.
 
Usiache hiyo kazi kama bado hakuna uhakika na unapo paangalia UTASAGA MENO
 
Hivi mtu unamaliza shule unaenda kuajiriwa na SERIKALI?

Hakuna majitu dhalimu na system dhalimu dunia hii kama kitu kinachoitwa SERIKALI!

Ni dude linaloendeshwa kwa matakwa ya wanasiasa!

It is a murder engine!
Acha tu,nilikuwa na ndoto nyingi nzuri tu
Saivi nimejikatia tamaa,hata ofisini kutwa nashinda nimejiinamia
 
Teh teh teh wangejua nimepigika hadi najichukia,naichukia hata kazi yangu
Laiti ningalijua nisingeajiriwa serikalin,nilikuwa private Kwa mwaka mmoja ,walipotangaza ajira kiherehere nikajitosa,kumbe naingia pori la miiba
Halafu plot zenyewe ni potential sema hamna wanunuzi,kimoja Cha makazi nilichojenga,kingine nilipanga kujenga mjengo wa kustaafia sema naona dream zi ebadilika na upepo,na Cha mwisho ni industrial plot hiki,nilipanga nipate mwekezaj tuingie partinership sema disko limeingia mmasai.



CHOMA MOTO MELI WEWE
 
Kwani shida iko wapi unalipwa mshahara ambao huufanyii kazi effectively? Unafika ofcn unacheza gemu kwa komputa mwisho wa mwezi unaenda ATM kutoa mshiko, shida iko wapi?
Sijawah cheza game ofisin kamwe
Nina vyeti 2 ,kimoja Cha mfanyakazi bora,kingine Cha best performer katika fani yangu Kwa mwaka 2017/18
 
Ni vile nchi yetu maskini tu..mie mdogo wangu anasema anajuta hata kupeleka cv huko...ovyo sana...alafu watumishi wamekuwa wanyoooongeee..tena mwez huu qwngine mshahara umechelewa sana sana kutoka..shenzy kbs
Acha tu tumekuwa wanyoonge hadi basi
Ila nahisi nilikuwa na ndoto kubwa sana na elimu yangu,tatizo kuzishusha ziwe average nashindwa
 
Kama unaweza kuwaza kufanya nite business kwanini usiwaze kudanga mchana na wanaume za watu?,maana km moyo wa kimalaya unao kabisa ni ujasiri kidogo tu unahitajika.

Ukiuza hivo vitu na kuacha kazi ndo inasaidia Nini???
 
Back
Top Bottom