Kuzunguka eneo la IFM kuna barabara tatu kubwa. Barabara ya Tanga, pembeni kote kumejaa, labda umng`oe mtu, hapo andaa kama 5m kwenda juu ili upate barabarani, line ya nyuma ni chuo. Barabara ya Bagamoyo kuanzia Msata mpaka Kiwangwa imejaa kabisa, ila waweza kumng`oa mtu, opposite na chuo kabisa eka moja line ya pili inacheza 2m kwenda juu. Line ya kwanza mafisadi walishagawana zamani.
Kuna barabara ya upande wa Machweo, inaingia Madesa na Mkoko, kwa mara ya mwisho eka iliuzwa 1m ya usoni na chuo, line ya pili ilitembea kwa laki tano. Upande wa nyuma wa chuo, huko hata laki tano unapata eka moja, shida miundo mbinu kama maji na umeme. Mashamba yaliyo nje ya eneo la chuo tunanunua kwa laki tatu.
Njia ya Bagamoyo, maji na umeme wameweka, njia ya Madesa maji yapo bado umeme.
Kama unaweza kwa bei hizi sema nikupe simu ya katibu wa kamati ya ardhi ya kijiji. Wakati wa kununua kamati nzima inafika shamba na unazunguka nao, kila mmoja analipwa 30,000/ kisha kwa pamoja wanasaini. VEO anapelekewa document na ten percent. Hakuna longo longo.