Natafuta Shamba

Natafuta Shamba

Asante nimepita hukop leo bado yapo. Nikapata muda wa kuingia ndani zaidi wananihakikishia yapo ya kutosha ila watu wanavyonunua sio muda aidha beoi itapanda au yatapungua. Eka kuanzia laki 2.5-3. Karibu sisi tumeenda kama 6 na kakikundi kanazidi kukua kila mtu anashika anazoweza.

OK! Nashukuru sana Mama Joe, nami ngoja nifanye michakato, Mungu akipenda tutajumuika huko pamoja.
 
samahani huko ekari wanauza sh ngapi na usafiri ni wa uhakika kwenda huko?
 
Usafiri upo unaweza panda basi za Bagamoyo/Msata pale Mwenge wakifika njiapanda ya msata nadhani ni kijiji cha kwanza kushoto. Au unaweza panda hiace Mbezi mwisho stand mpya za msata kabla ya kufika njiapanda unashukia Mazizi sijaipitia hii njia ila ipo. Kutoka Mwenge hadi kijijini kilometa 140. Bei laki 2.5-3. Karibu

Mama joe nami naweza pata kashamba huko?
 
Utapata natokea huko saahizi. Watu wameshika zaidi barabarani na hasa hii mpya ya msata, huku kwenye kona kuelekea Morogoro hawakujua sana. Karibu

Bei nzuri mananasi vp yanakubali?
 
Kwakweli mimi nilitaka zaidi maji na mitiki. Mananasi kwavile yanakubali sana kata ya Kiwangwa hata hapa nadhani yatakubali. Nitaulizia tena kwa wenyeji kwani huku watu wa nje wachache wamelima mitiki na wana ng'ombe wenyeji nnavyoelewa wanalima mahindi tu sio nanasi
Bei nzuri mananasi vp yanakubali?
 
Kwa eka moja ilikuwa Tsh 50,000/ kwa eka, juzi nilisikia imepanda mpaka 80,000/ kwa eka. Naamini baada ya hawa jamaa kutoka mashariki ya kati kuvamia itakuwa inacheza kwenye laki moja hivi.

Nikirudi Dar mwisho wa mwaka tutafutane tukatembee mitaa ya kule.

Mambo vp Mkuu upo?
 
Msata,ipi.
Je ni Kihangaiko, au Madesa, au hii njia ya kuja Bagamoyo? Mimi niko Madesa kuelekea Mkoko. Siku twende pamoja dada.

Mkuu yaani mimi nimepata shamba eneo la mkoko huko msata, heka 20 (si haba). Tena wiki jana nimetoka kuangalia ujenzi wa kibanda. Umeme bado, nitaanza na solar kama Jirani yangu mmoja huko shambani.
Pia kuna mtu mwingine jirani huko shamba ameshaanza kilimo cha nanasi.
Nafuatilia sana post zako, Asante kwa elimu nzuri kwenye jukwaa hili.
 
Ni Mazizi kwa kweli ni njiapanda kijiji kiko kama km 3 kutoka njia panda ya Msata unakuwa unarudi Moro ukitokea Kiwangwa, kushoto. Nadhani patanifaa ingawa bado nafanya utafiti zaidi, udongo ni mzuri sana mitiki, migomba, mahindi, miembe na nanasi vimekubali. Na bei sio mbaya ila naangalia maji kwa mifugo kama yao ingawa kuna ngombe wengi mtu kafuga. Tutatafutana ukaone.

wanauzaje huko?
 
Kwakweli mimi nilitaka zaidi maji na mitiki. Mananasi kwavile yanakubali sana kata ya Kiwangwa hata hapa nadhani yatakubali. Nitaulizia tena kwa wenyeji kwani huku watu wa nje wachache wamelima mitiki na wana ng'ombe wenyeji nnavyoelewa wanalima mahindi tu sio nanasi

Mananasi yanachagua sana.

Kiwangwa yenyewe sio yote inaota mananasi
 
Karibu mkuu wanaanzia laki 2.5 hadi laki 3. Maji yaliyopo ni bomba ingawa sijalifatilia bado, mie nimeona migomba, mitiki, mahindi na wansema matikiti ila kiukweli hapa ni mapori eneo kubwa hakuna anaelima. Wachache wanavishamba vidogo vya mahindi ingawa udongo ni mzuri uko tifu kwa hiyo kwa maji ya bomba au kisima waweza lima chochote. Kwa mvua za msimu mahindi yanakubali na tikiti inapoishia mvua
 
Usafiri upo unaweza panda basi za Bagamoyo/Msata pale Mwenge wakifika njiapanda ya msata nadhani ni kijiji cha kwanza kushoto. Au unaweza panda hiace Mbezi mwisho stand mpya za msata kabla ya kufika njiapanda unashukia Mazizi sijaipitia hii njia ila ipo. Kutoka Mwenge hadi kijijini kilometa 140. Bei laki 2.5-3. Karibu
Mkuu Mama Joe hapo kwenye laki 2.5-3 unamaanisha nn?
 
samahani huko ekari wanauza sh ngapi na usafiri ni wa uhakika kwenda huko?
Kuhusu usafiri hauna haja ya kupitia Bagamoyo kwa sababu itakulazimu ulipe nauli kubwa na hata unaweza ukaunga mabasi...Kama uko Dar nenda Ubungo pale stand ya vidala dala kwenye njia ya kutokea kule yanakosimama magari ya msasani na mwananyamala pembeni yake utayaona magari ya UBUNGO/MBEZI-MSATA yanapakia..Nauli ni sh 4500/- mpaka hapo Mazizi
 
Sorry namaanisha eka moja inauzwa kwa laki mbili na nusu hadi laki laki tatu kutegemea na umbali na shamba pia

Inamaana nikiingia ndani zaidi naweza kupata kwa bei nafuu zaidi?

Hapo ulipo wewe umbali gani kutoka barabara kubwa?
 
Back
Top Bottom