Zipo Gwata mbili, mimi nazungumzia Gwata ya Kisarawe. Kama ukifika Mzenga, kuna njia inakwenda Mafizi kupitia Mwanamsekwa, Nyani hadi Gwata. Gwata pana watu wengi sana,wakulima na wafugaji,usafiri wa bus kuja Buguruni upo kila siku, usafiri wa tren upo. Ardhi ipo nzuri sana kando ya mto Ruvu. Lipo gulio kubwa kwa siku nne mfululizo,la mifugo zaidi. Biashara ya nyumba za wageni inalipa sana kuanzia alhamisi mpaka jumapili.
H/shauri ya Kisarawe wanataka kujenga mnada wa kisasa pale,viwanja vimepanda bei vibaya baada ya plan hiyo kuwekwa peupe. Mimi nilifuata ardhi ya kuotesha cocoa. Jamaa zetu Waarabu wamekomba mapande ya ardhi kinoma. Sijasikia ugomvi wa ardhi kule. Maji ni mto Ruvu, ni nguvu yako. Na migomba inamea pia.
Gwata ya pili iko Migindu huko Chalinze,
Swali lingine kaka!!!!!!!