Laiti ningelijua mapema, nisingelinunua lile shamba

ormystatus

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
262
Reaction score
464
Ni takribani miaka 8 tangu niliponunua pori lenye ukubwa wa ekari 10 katika kijiji cha Nnyengedi mkoa wa Mtwara na kuligeuza kuwa Shamba la Mikorosho.

Shamba ambalo halipo mbali sana na barabara kubwa na makazi ya watu. Lilozungukwa na Mashamba ya wanakijiji na Wawekezaji wengine kutoka mjini.

Fauka ya yote, hiyo imekuwa kama msumari wa moto moyoni mwangu, na si faida kwani imenitenganisha na fursa ya Unenepeshaji na ufugaji wa Wanyama kama Ng’ombe na Mbuzi katika Shamba hilo.

Inanilazimu kuingia gharama kubwa ya kutafuta eneo lingine zuri mbali na mashamba ya wakulima, karibu kabisa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Malisho

Je, Ni Vijiji/Maeneo Gani Mkoani Mtwara Yametengwa Rasmi Kwa Ajili Ya Malisho ?

Maongezi yetu yalimalizika huku nikiachiwa swali hilo.
 
Sijakuelewa ama ni vile bado sijapata lunch nna wenge ?

Shamba baya?
Linakupa hasara ?
Mikorosho hailipi ?
Upo karibu na makazi ?
Unataka kufuga ?
Ama kuuza ?
Nilidhani pekeyangu ndiyo sijamwelewa.

Hata hivyo mleta mada ormystatus hiyo Nyengedi uliyoitaja ipo Mkoa wa Lindi na si Mtwara. Tena ni Kijiji kilichopo Jimbo la Nape-Mtama.
 
Ni takribani miaka 8 tangu niliponunua pori lenye ukubwa wa ekari 10 katika kijiji cha Nnyengedi mkoa wa Mtwara na kuligeuza kuwa Shamba la Mikorosho.

Shamba ambalo halipo mbali sana na barabara kubwa na makazi ya watu. Lilozungukwa na Mashamba ya wanakijiji na Wawekezaji wengine kutoka mjini.

Fauka ya yote, hiyo imekuwa kama msumari wa moto moyoni mwangu, na si faida kwani imenitenganisha na fursa ya Unenepeshaji na ufugaji wa Wanyama kama Ng’ombe na Mbuzi katika Shamba hilo.

Inanilazimu kuingia gharama kubwa ya kutafuta eneo lingine zuri mbali na mashamba ya wakulima, karibu kabisa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Malisho

Je, Ni Vijiji/Maeneo Gani Mkoani Mtwara Yametengwa Rasmi Kwa Ajili Ya Malisho ?

Maongezi yetu yalimalizika huku nikiachiwa swali hilo.
Omba ushauri kwa mrembo na nuru ya taifa mkulima namba moja mwenye uzuri wa aina yake kwaanzia unyayo hadi utosini.

Screenshot_20260315_150856_Instagram.jpg

min -me MamaSamia2025

adriz de mbusii
 
Back
Top Bottom