Natafuta Fundi wa LED Tv

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
54,884
120,015
Habari wana jamvi.

Natafuta fundi mzuri na anaejielewa wa LED tv yangu. Ina miaka miwili na ushee ghafla juzi imeanza kuonesha nusu screen mistari chenga chenga na nusu ingine inaonesha clear kabisa.

Anaemjua fundi mzuri, kwa hapa Dar hasa maeneo ya kuanzia kinondoni,mwenge,makumbusho,sinza,magomeni,msasani anijulishe. Sio mbaya hata wa maeneo mengine nikikosa itabidi nimfuate, tafadhali niwekee contacts zake.

f67eadd.jpg
 
tatizo dogo ilo, nabadilisha screen tu kwa bei poa kabisa...!!!
 
Nimeenda kumuona huyu fundi, kaicheki kasema screen imeshakufa ni ya kubadilisha. Bei ya screen ni nusu ya Tv mpya kwahio naona bora ninunue ingine tu.
hakuna njia nyingine kioo ni lazima kibadilishwe, hakuna njia nyingine mkuu.
kakwambia tsh ngapi?
 
tatizo lako inaoneka ni kwamba spika either za subwoofer au za kawaida umeziweka karibu saana na TV yako, madhara yake ndio huwa haya. Next time, usiweke hizo mambo karibu asee.....!!
kupunguza gharama
 
500,000/-
ngoja nkushauri kitu..
nenda mwenyewe kko, kama uko kwa Makonda...
tafuta kioo mwenyewe halafu mpelekee akufungie na kioo nadhani hakizid hata laki 3, ukienda online utaona dola kinaenda dola 40 tu!
 
Miaka miwili si hapa kaipimishe scraper jipange chukua nyingine wachina washatufanya wateja wao sasa tufanyeje havidumu kama zamani
 
ngoja nkushauri kitu..
nenda mwenyewe kko, kama uko kwa Makonda...
tafuta kioo mwenyewe halafu mpelekee akufungie na kioo nadhani hakizid hata laki 3, ukienda online utaona dola kinaenda dola 40 tu!
Ok, unaweza kunitajia mitaa yalipo maduka ya vioo vya TV?
 
tatizo lako inaoneka ni kwamba spika either za subwoofer au za kawaida umeziweka karibu saana na TV yako, madhara yake ndio huwa haya. Next time, usiweke hizo mambo karibu asee.....!!
kupunguza gharama
Mkuu zikiwa kimnya bila ya kuwashwa pia ni shida?.
 
tatizo lako inaoneka ni kwamba spika either za subwoofer au za kawaida umeziweka karibu saana na TV yako, madhara yake ndio huwa haya. Next time, usiweke hizo mambo karibu asee.....!!
kupunguza gharama
Ingawa hio picha sio halisi ila ni kweli iko karibu na speakers. Asante kwa kunielimisha. Swali speaker zinauaje screen? Vibration inaweza kulegeza vitu lakini vinaweza kufungwa tena.
 
tatizo lako inaoneka ni kwamba spika either za subwoofer au za kawaida umeziweka karibu saana na TV yako, madhara yake ndio huwa haya. Next time, usiweke hizo mambo karibu asee.....!!
kupunguza gharama
Ni umbali upi halisi unaotakiwa kuweka kutoka ilipo TV hadi kwenye Subwoofer na Spika?
 
Hizo LG zinaonekana kuwa na tatizo hilo kwani Mar 2016 LG yangu ilikuwa ikiweka mistari nikawaleta mafundi kutoka LG Dealers ya Kisutu wakaifungua wakagundua hitilafu lakini siyo Kioo na ikahitajika kupata spare ambayo kwa TZ ilikosekana. Wakaifunga nikawa natumia hivyo hivyo lakini baada ya wiki mbili nikaona inaonesha vizuri mpaka leo hii ila sasa ikawa imejiondoa kwenye mode ya 3D na kuwa ya kawaida.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom