Natafuta binti Salaf wa kuoa

Natafuta binti Salaf wa kuoa

SALAFI YA NYOKO....MOJA KATI YA WATU HATARI NA WA HOVYO SANA KATIKA SUALA ZIMA LA NDOA,NI HAWA WANAOJIITA SALAFI.....🙌🤣 MSAADA WA USHAURI SI UKACHUKUE KWA SALAFI WENZIO HAWAKOSI MADADA YAKHEEE😁🤝
Kwanini Una-generalize Mambo.
Unapokutana na watu wawili au watatu wenye Tabia hiyo.

Bila kufanya Utafiti wa kina Usilifunge jambo. Kwamba watu furani Ndio walivyo.

Ilihali watu Uliokutana nao wenye hiyo Tabia katika hilo kundi hawafiki 10.

Na wao wapo maelfu kwa maelfu.
 
Inaruhusiwa

Inaruhusiwa
Swali: Hii leo kumeenea mialiko na fatwa zinazojuzisha kumuoa mwanamke mjamzito ambaye si mke wa mtu. Ni mamoja anayemuoa ni huyohuyo aliyempa ujauzito au mtu mwengine. Mambo haya yameenea na tunataraji kutoka kwako muheshimiwa utatuzi, kuwazindua watu juu ya ukhatari wake na ubainifu wa hukumu ya Shari´ah juu yake. Allaah akujaze kheri.

Jibu: Haijuzu kumuoa mjamzito mwenye ujauzito unaotokana na uzinzi au usiotokana na uzinzi mpaka kwanza atwahirike. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapojifungua mimba zao.” (65:04)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asimwagilie maji juu ya mazao ya mwingine.

Bi maana manii yake.

“… mazao ya mwingine.

Bi maana ujauzito wa mwingine.

Ikiwa ujauzito huu ni wa mwanamke aliyeachika au ambaye amefiliwa, basi haijuzu kwake kumuoa mpaka kwanza ajifungue.

Ikiwa mimba hiyo inatokana na uzinzi, haifai vilevile kumuoa – si mwanamke huyu mzinzi wala mwenginewe – mpaka azae. Kwa sababu mimba hii ni yenye utata kwa tone la manii ambalo halinasibishwi si kwa yule mwanamme mzinzi wala mwengine. Mtoto huyo atanasibishwa kwa mama yake. Mtoto hanasibishwi kwa yule mwanamme mzinzi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtoto ni wa kitanda na mzinzi anastahiki [kupigwa] jiwe.”

Mtoto ni wa mama akiwa ni wa nje ya ndoa na yule mwanamme mzinzi anastahiki kusimamishiwa adhabu ya ki-Shari´ah.

Mwanamke akishika ujauzito na bado hajaolewa basi haijuzu kumuoa kabisa katika nchi yoyote ile mpaka kwanza ajifungue. Akishajifungua basi itafaa kumuoa. Hayo yafanyike baada ya kutubia, kurejea na kutujia kwa Allaah. Basi hapo itafaa kwa muislamu kumuoa baada ya kutubia.


  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom