Natafuta Baba wa Hiari anisimamie Ndoa

Natafuta Baba wa Hiari anisimamie Ndoa

Inamaana hko unapokaa kaka hata kanisani umekosa wazee wenye busara kwel mpaka uje hapa jf je hata unakoabudu wamekosa kwel au we mwenzangu unakaa na watu wa aina gan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Majuzi nilipost kuhusu kufuatilia chimbuko la Baba yangu huko Kigoma, wengi mkashauri ni bora nijenge tu maisha ya yangu/nitafute hela, mwenye shida na mimi atanitafuta mbele ya Safari...nimekubaliana na huo Ushauri. Pia kuna mliopendekeza ni bora nitafute Baba wa Hiari atakaye simamia mchakato wangu wa kuingia kwenye Ndoa/Harusi.

Kwahiyo nawasilisha kwenu, hasa watu wazima wenye familia na umri umeenda mlioko Dar, mmoja wenu ajitolee kuwa Baba wa Hiari (ni baada ya mimi kumpa full story) kisha awe tu kama Mlezi/Baba wa Hiari...kama vile ilivyo kwa "Baba wa Kiroho"...nadhani Waroma wataelewa zaidi maana hata Ubarikio mtu huwa na Wazazi sijui wa Ubarikio...sijui sana ila nshaskia.

Natarajia kuoa mwisho wa Mwaka huu, Mchumba tayari ninae japo sina Uhakika nae (nimekutana nae Dar), hivyo Baba wa Hiari, atakuwa na nafasi ya kurecommend binti, au kunishauri pa kuoa au wa kumuoa...NAFASI HIYO ANAYO.

Kuhusu gharama za Ndoa/Harusi, naweza kujichanga hata kama sitachangiwa na mtu hata mmoja. Nimeshaanza kusave.

Uzi uliopita ni huu:
Naomba mchanganuo wa Bajeti ya kutoka Dar to Kigoma. Naenda kutafuta Chimbuko la Baba yangu.

cc Shunie Mshana Jr ISIS Nyani Ngabu Erythrocyte Bavaria BAK Sakayo Mama Sabrina elvischirwa fredy18 Thad Sky Eclat thA goD @kanungila MAGACHA na members wote.
Asante tuwasiliane
 
Back
Top Bottom