Natafuta Baba wa Hiari anisimamie Ndoa

Natafuta Baba wa Hiari anisimamie Ndoa

musa_ali

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
377
Reaction score
386
Wakuu,

Majuzi nilipost kuhusu kufuatilia chimbuko la Baba yangu huko Kigoma, wengi mkashauri ni bora nijenge tu maisha ya yangu/nitafute hela, mwenye shida na mimi atanitafuta mbele ya Safari...nimekubaliana na huo Ushauri. Pia kuna mliopendekeza ni bora nitafute Baba wa Hiari atakaye simamia mchakato wangu wa kuingia kwenye Ndoa/Harusi.

Kwahiyo nawasilisha kwenu, hasa watu wazima wenye familia na umri umeenda mlioko Dar, mmoja wenu ajitolee kuwa Baba wa Hiari (ni baada ya mimi kumpa full story) kisha awe tu kama Mlezi/Baba wa Hiari...kama vile ilivyo kwa "Baba wa Kiroho"...nadhani Waroma wataelewa zaidi maana hata Ubarikio mtu huwa na Wazazi sijui wa Ubarikio...sijui sana ila nshaskia.

Natarajia kuoa mwisho wa Mwaka huu, Mchumba tayari ninae japo sina Uhakika nae (nimekutana nae Dar), hivyo Baba wa Hiari, atakuwa na nafasi ya kurecommend binti, au kunishauri pa kuoa au wa kumuoa...NAFASI HIYO ANAYO.

Kuhusu gharama za Ndoa/Harusi, naweza kujichanga hata kama sitachangiwa na mtu hata mmoja. Nimeshaanza kusave.

Uzi uliopita ni huu:
Naomba mchanganuo wa Bajeti ya kutoka Dar to Kigoma. Naenda kutafuta Chimbuko la Baba yangu.

cc Shunie Mshana Jr ISIS Nyani Ngabu Erythrocyte Bavaria BAK Sakayo Mama Sabrina elvischirwa fredy18 Thad Sky Eclat thA goD @kanungila MAGACHA na members wote.
 
Mtoa mada hio avatar unayotumia kuna shoga/punga alikua anaitwa padri mcharo humu jf alikua anaitumia,ulikua unamfahamu?

Utakosa msaada sababu ya hio Avatar boss.
 
Kwanini unaamini sana watu wa mitandaoni?
Hauna ndugu au watu tuu ambao kwa njia moja au nyingine mnafahamiana zaidi?
 
Natarajia kuoa mwisho wa mwaka huu, Mchumba tayari ninae "japo sina uhakika nae"

Are you serious comrade????[emoji848]
Nilifikiri nimesoma vibaya

Yaani mtu ambaye ndiye unajenga nae family huna uhakika nae?

Ukaenda mbali ukasema hata ukichaguliwa ni sawa!?
Mmh

[emoji252] [emoji479]
 
Wazee wa mtaani wanamfahamu alivyokuwa chakaramu, anatafuta wa kwenye mitandao ambao ni strangers ambao hawajui issue zake.

Jitokezeni wazee.
Hahaha wachina wanasemaga "ukweli mchungu"

Halafu huyu ni 'padri mcharo' new id, asije akakucharukia kaka yangu.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Wazee wa huku tabia zao ndio kama hizo hizo za wa mtaani bz hawatoki kwenye sayari tofauti na hii mkuu.
Tofauti ni kua wazee wa huku hatumjui background yake, si umeona kasema atasimulia story yake kwa hiyo lazima aipambe tofauti na wazee wa mtaani kwake wanamjua nje ndani.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
kwahiyo wewe huna, wajomba, binamu, babu, baba mdogo, au hata majirani? mpaka upate baba wa hiari huku ambae hamjuani kwa lolote, hebu kuwa serious, na huna mchumba bwana, huwezi kutuambia una mchumba lakn huna uhakika nae, na ukamalizia kwamba uko tayari kuchaguliwa mchumbwa mwingine, mean uko tayari kumuacha huyo binti ulienae wakati wowote kisa tu baba wa hiari kakwambia, something is very wrong with u
 
Wazee wa huku tabia zao ndio kama hizo hizo za wa mtaani bz hawatoki kwenye sayari tofauti na hii mkuu.

No, uzuri wa wazee wa huku watapewa story kutoka kwako tu, hawatakuwa na negatives zako.

Wale wa mtaani wanakujua na hawako tayari kukudhamini, kama ukipitia thread yake aliyoweka link anasema alishawahi kuoa ila wakaachana kwa sababu alioa akiwa bado mdogo, sasa ukute kulikuwa na issue za kupigana nk ambazo zinasababisha wanaomjua wasimdhamini.
 
Mtoa mada hio avatar unayotumia kuna shoga/punga alikua anaitwa padri mcharo humu jf alikua anaitumia,ulikua unamfahamu?

Utakosa msaada sababu ya hio Avatar boss.
Simjui na siijui. Basi wacha nibadili Avatar. Thanks
 
Tofauti ni kua wazee wa huku hatumjui background yake, si umeona kasema atasimulia story yake kwa hiyo lazima aipambe tofauti na wazee wa mtaani kwake wanamjua nje ndani.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.

Yes, hapo ndo point ilipo.
 
Back
Top Bottom