Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 500
- 488
Hakika nimehudhuria ndoa nyingi ila hii ndoa ya jana ilikuwa ni kiboko sana, baada ya rafiki yetu kuwa mgumu sana kwenye kuoa, hatimaye tulifanikiwa kumshawishi aoe, maana ilikuwa kila siku anasema anajipanga kujitafuta yeye kwanza ili awe na maisha mazuri, tulimshinda kwa hoja ya msingi kuwa kama hatafanikiwa kuwa na maisha mazuri maana yake hataoa? Mwisho tulikubaliana maisha mazuri hayahusiani na kuoa ila ndoa inaweza kuwa chachu ya maisha mazuri au kuyumbishwa kwa maisha mazuri, kuoa ni kama elimu ambayo unaweza kuongezea maarifa yako ya kupata maisha mazuri.
Tulijipanga kumpa ushirikiano wa kutosha rafiki yetu hivyo tulishiriki kikamilifu zoezi zima la ndoa, kikubwa yeye na bibi harusi walioneshana upendo mkubwa sana kiasi cha kubaini kama marafiki zake na hata kwao na bibi harusi walijua hilo hivyo haikuwa ngumu kupatiwa ushirikiano wa kutosha kuhusu ndoa, baada ya nderemo nderemo na vifijo kama ujuavyo ndoa za siku hizi zina mbwembwe nyingi zenye tofauti za tamaduni za kiafrika na nchi za Ughaibuni, yaani ni kawaida kukuta mchanganyiko wa mandhari ya kihaya na Uingereza ndani ya ukumbi mmoja au mandhari ya kimakonde na kiarabu kwenye ndoa moja.
Kikubwa watu tulikula vizuri na kunywa vinywaji mbali mbali zikiwemo sharubati za kila aina, tulifurahi sana, tulitoa zawadi za kila aina, hakika bibi harusi na bwana harusi walipendeza sana, hatimaye ulifika wakati wa kutoa neno la shukrani na husia hivyo walianza wanandoa kutoa shukrani kwa watu wote wakiwemo na wazazi, hatimaye ilifika zamu ya baba mkwe kutoa neno kwa niaba ya wazazi wa bibi harusi, ukumbi ulitulia kidogo, naye baba akaanza kwa kusalimia kisha kujitambulisha yeye ni mstaafu wa jeshi akaendelea kwa kusema nimewafunza wanangu kwenye malezi ya kiaskari.
Hivyo mkwe wangu mke niliyekukabidhi yuko timamu kwa mapambano, watu tulipoa kama vile anatupiga mikwara, tukawa tumemkazia macho rafiki yetu, akasema mapambano ninayokusudia hapa ni ya kujenga familia, kwenye uwanja wa medani ya kivita kuna wakati tuliishiwa silaha ila tulivuka, nanyi kuna wakati mtaishiwa pesa au mali ila mtatakiwa kusonga mbele, pia kuna wakati askari mnazidiwa mbinu hivyo mnapaswa kurudi nyuma kujipanga, katu kwenye maisha yenu ya ndoa msione aibu kuanza upya pindi mnapoyumba, kuna wakati askari anajeruhiwa ila katu hakati tamaa, nanyi kuna wakati mtaumizwa na walimwengu katu msikate tamaa, kuna wakati mtakuwa wenye furaha baada ya ushindi askari huwa hawatengani, nanyi msitengane kwa kushiba furaha.
Kanuni za jeshi mpaka linakuwa na nidhamu ya hali ya juu ni kuwa kiongozi Mkuu hakosei na akikosea rejea kanuni ya kwanza, hivyo hushauriwa tu kwa busara na wasaidizi wake, katika familia mnayoenda kuijenga kumbukeni kiongozi mkuu ni mume na mshauri Mkuu ni mke hivyo, mkifanikiwa kufanya hivyo hata wafuasi wenu watakaozaliwa watajengwa na misingi ya nidhamu yenu na hatimaye mtatuletea jamii iliyo na nidhamu sana, kwa maana mafanikio makubwa ya jeshi ni nidhamu.Haya ninayoyaeleza mkawafundishe na watoto wenu kwa maana mnaenda kujenga jamii bora kwa kutuletea watoto bora.
NDOA SIO FIMBO YA KUUMIZANA BALI NI KIWANDA CHA BINAADAMU
"watoto ni matunda mazuri yaotao mti wowote, yakinge yasishambuliwe na wadudu"
Dr.Zack ✍️