Nassari asusia kikao cha baraza la madiwani kupinga ugawaji wa viwanja

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,351
2,000
Baada ya kamati ya uchumi ya baraza la madiwani Arumeru kudhamiria kuingia na hoja ya kuuza viwanja(square meter kwa Tsh 22'000). Mheshimiwa mbunge machachari amesusia kikao cha madiwani (full council) ili asiwe historia ya kuhalalisha ufisadi wa viwanja huko Meru.
 

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
2,000
baada ya kamati ya uchumi ya baraza la madiwani arumeru kudhamiria kuingia na hoja ya kuuza viwanja(square meter kwa Tsh 22'000).mheshimiwa mbunge machachari amesusia kikao cha madiwani(full council) ili asiwe historia ya kuhalalisha ufisadi wa viwanja huko meru.
Ana sababu za mzingi za kugoma au basi tu kutenkeleza sera za chama chake za kugomea kila kitu?
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,518
2,000
Mhh meru mmezidi nakumbuka vya duluti eti mlikua mnauza sq meter sh 24000,kuna mmeru mwenye uwezo wa kununua?
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,171
2,000
Ana haki maana unakuta hawa mafisadi wamezidi kujilimbikiza mali na wakiwaacha wanainchi wakiwa hoi wajamani!
Nassari nakuunga mkono!
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Baada ya kamati ya uchumi ya baraza la madiwani Arumeru kudhamiria kuingia na hoja ya kuuza viwanja(square meter kwa Tsh 22'000). Mheshimiwa mbunge machachari amesusia kikao cha madiwani (full council) ili asiwe historia ya kuhalalisha ufisadi wa viwanja huko Meru.

Safi sana .................. komaa kamanda ili kuonyesha kieleweke
 

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,057
1,500
Hana jipya atimize ahadi ya kusambaza maji aliyoitoa muda unayoyoma!

kwa taarifa yako ahadi anazitimiza kwa kwa kasi ya ajabu
-ameweza kutimiza ahadi ya maji ngabobo sehemu ambapo ni kama jangwa.
-maroroni maji tayari
-kikwe napo ni katika hatua za mwisho
-leguruki na kingori mpango unafanywa kuchukua maji wilaya ya hai..
Mkuu usikurupuke fanya utafiti kwanza
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,151
1,250
Inawezekana kuwa ni mwanzo mzuri kama madiwani wote ni wa vyama other than where he belongs......

1. Lakini baada ya kutoka yeye alternative plan yake ilikuwa ni shilingi ngapi kwa square meter moja

2. Bei ya soko kwa square meter hapo mahali ni shilingi ngapi???

3. Kuna bei elekezi katika masuala haya hapo wilayani kwake????

Hii falsafa ya kuwa eti mimi sikuwa sehemu ya maamuzi inabidi tuiangalie kwa jicho la tatu sababu kama ni sehemu ya maamuzi au la bado wananchi wataumia kwa yatokanayo.....so suala la kutoka linampa yeye credo kuliko kuwasaidia wananchi husika..........thus atakuwa kautumia mgogoro kujipandisha hadhi kuliko kuwasaidia wananchi.....hili si sawa...ni bora kukaa na kujenga hoja mpaka dakika ya mwisho kuliko kutoka


A retreating soldier has nothing good to serve......................neither for himself, people nor the nation at its large..................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
2,000
Mara ngapi Bungeni Chadema wanakomaa kutetea maslahi ya Taifa hili lakini kwa sababu ya uchache wao wamebezwa na ccm na Watanzania wengine wanaonufaika na ufisadi na hujuma zinazofanywa na ccm.
 

LOMAYANN

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,165
1,250
akishiriki wakipitisha kwa kuwa wako wengi. watasema nayeye alipitisha hata kama atapinga.

Umenena mkuu madiwani wetu waliingia na kupinga matumizi makubwa ya Uzinduzi wa jiji la Arusha baadaye wakasema wamemtambua meya wa Kichina( feki) na sasa wanaendesha propaganda chafu dhidi yao, Safi sana kamanda Nassari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom