Madiwani Meatu wamuangukia Waziri TAMISEMI, wataka ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha za Halmashauri, wahofia uwepo ufujaji wa fedha za wananchi

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
HALMASHAURI ya Wilaya ya Meatu kama ilivyo maeneo mengine ya

Serikali za Mitaa inasimamiwa na kuongozwa kwa kuzingatia

Sheria mbalimbali za nchi ikiwemo Sheria ya Serikali za Mitaa ya

mwaka 1982 na Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya

Meatu za Mwaka 2014 ambazo zinaelekeza mambo mbalimbali ya

kuzingatia.

Kwa kipindi kirefu sasa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya

Meatu Mhe. Antony Philipo Athumani na Mkurugenzi Mtendaji

wa Halmashauri Ndugu. Msoleni Juma Dakawa wameshindwa

kumudu nafasi zao kwani kumekuwepo na usimamizi dhaifu wa

shughuli za Halmashauri, uzembe, upendeleo na matumizi

mabaya ya fedha za umma hali inayopelekea kurudisha nyuma

maendeleo ya wana Meatu.

Aidha kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na

Taratibu zilizowekwa katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli

za Serikali hali ambayo inaiweka halmashauri pabaya kila leo

ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma, miradi kutelekezwa,

kukosekana kwa uwiano wa miradi ya maendeleo na gharama

kubwa za miradi.

CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MEATU

1. Usimamizi na utekelezaji dhaifu wa miradi ya maendeleo

Utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye fedha za Serikali na

wahisani kwa mwaka wa fedha 2021/22 kuna miradi ambayo

imetekelezwa kwa kiwango cha chini sana, kuchelewa kwa

utekelezaji wa miradi, fedha kupelea na miradi kutelekezwa na

kuachwa magofu, baadhi miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-

(i) Ujenzi wa Kituo cha Afya Iramba Ndogo na Mwasengela

ilikuwa ukamilike tangu Aprili 2022 kwa awamu ya kwanza lakini

hadi sasa miradi hiyo haijakamilika na fedha zimepelea

kukamilisha miradi hiyo pia tangu fedha za awamu ya pili kiasi

cha Tsh 500,000,000 ziletwe Mwezi Mei, 2022 hadi leo ujenzi

haujaanza katika vituo hivyo vya afya.

Sababu za kupelea fedha na kukwama kwa ujenzi wa miradi hiyo

hazieleweki hadi sasa na hazikuwahi kutolewa taarifa hapo awali.

(ii) Ujenzi wa Sekondari mpya za Mwandu Itinje na Mwamanimba

ambazo zililetewa fedha kutoka Serikali Kuu kwa awamu ya

kwanza kiasi Tsh 940,000,000 yaani kiasi cha Tsh 470,000,000

kwa kila shule. Fedha za utekelezaji wa miradi hii zimepelea na

ujenzi umesimama na kuacha magofu. Awali menejimenti licha ya

kujua kuwa fedha zitapelea lakini haikutoa taarifa Wizarani,

Baraza la Madiwani wala uongozi wa Kata husika ambako mradi

unatekelezwa na hakuna mkakati wowote uliowekwa kumalizia

miradi hiyo.

(iii) Miradi ya WASH- ujenzi wa vyoo inayotekelezwa katika

Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa miradi mingi fedha

zimepelea na ujenzi umesimama na kuacha magofu ya miradi

hiyo ambayo haitoi huduma iliyokusudiwa. Hakuna taarifa

iliyotolewa juu ya kupelea na kusimama kwa miradi hiyo na

hakuna mkakati uliowekwa wa kukamilisha miradi hiyo.

Kitendo cha kuanza kutekeleza miradi kwa fedha pungufu,

kuchelewa utekelezaji wa miradi bila sababu za msingi,

kukosekana kwa mikakati madhubuti ya kumalizia miradi hiyo na

Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kushindwa kutoa

taarifa sahihi kwa Wahisani, Wizarani, Baraza la Madiwani na Kata

husika kunazua maswali mengi yasiyo na majibu. Lakini pia

kwanini mradi usitekelezwe kwa awamu na kwa ukamilifu badala

ya kubaki na gofu lisilotumika.

2. Kubadilisha mpango wa bajeti bila idhini ya Baraza la

Madiwani

Mnamo Tarehe 8.02.2022 Baraza la Madiwani lilifanya kikao

maalum kwa ajili ya kupitia na kupitisha bajeti ya halmashauri ya

mwaka wa fedha 2022/23 bajeti ya Halmashauri hupitishwa kwa

kuzingatia Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa namba 9 ya

mwaka 1982 kifungu cha 43 (i), ilani ya uchaguzi ya CCM ya

mwaka 2020 na ahadi za viongozi za wakati wa uchaguzi.

Katika vikao vya Kamati za Kudumu za Halmshauri ya Wilaya vya

robo ya kwanza imeonekana kuna ukiukwaji mkubwa sana wa

sheria na kanuni katika utekelezaji wa bajeti ambapo imeonekana

miradi mingi iliyopitishwa na baraza la madiwani haikupangiwa

fedha na kupendekezwa kupewa fedha miradi mingine mipya

ambayo haikuidhinishwa na kupangiwa fedha na Baraza la

Madiwani katika kikao halali cha kupitisha bajeti mwaka wa fedha

2022/2023. Baadhi ya maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Baraza la Madiwani lilipitisha fedha za lishe Tsh 109,000,000

na Fedha za Kilimo na Ushirika za Mapato ya ndani Tsh

50,000,000 jumla ya Tsh 159,000,000 Baraza lilipitisha fedha hizi

ziende kukamilisha miundombinu katika Zahanati 10 ili ziweze

kufunguliwa na kutoa huduma kwa wananchi na kila zahanati

ilipangiwa Tsh 15,900,000 kila moja Zahanati hizo ni (i) Itaba, (ii)

Mwanzugi, (iii) Mwageni B, (iv) Semu, (v) Malwilo Mnadani, (vi)

Igushilu, (vii) Makomangwa, (viii) Tindabuligi, (ix) Nata (x)

Itongolyangamba. Fedha hizi hazikupangwa katika bajeti kama

Baraza la Madiwani lilivyoamua kinyume na bajeti ilivyopitishwa.

(ii) Katika kupitisha Bajeti ya mwaka 2022/2023 Baraza la

Madiwani lilipitisha Tsh 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa mradi

wa Kituo cha Afya cha Iramba ndogo na Mwasengela yaani kila

kituo cha afya kilipangiwa kiasi cha Tsh 250,000,000. Fedha hizi

hazikuingizwa katika bajeti na badala yake zilibadilishiwa

matumizi bila idhini ya Baraza la madiwani na kupangiwa maeneo

mengine kama ifuatavyo:-

(a) Ujenzi wa nyumba ya mtumishi Zahanati ya Masanga Tsh

50,0000,000

(b) Ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Mwandu Kisesa

Tsh 50,000,000

(c) Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi zahanati ya Semu Tsh

50,000,000

(d) Ujenzi wa nyumba mtumishi Zahanati ya Mwabagalu Tsh

50,000,000

(e) Ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili vituo vya afya Tsh 300,000,000

Miradi hii iliyoonyeshwa (a) hadi (e) yenye thamani ya Tsh

500,000,000 haikupitishwa na Baraza la Madiwani na wala Baraza

halijawahi kupewa taarifa ya mabadiliko hayo ya mpango wa

Bajeti hadi hii leo Oktoba 2022, uamuzi uliofanywa na

Menejimenti wa kubadilisha mpango wa bajeti bila kibali na idhini

ya Baraza la Madiwani ni kinyume cha Sheria ya Fedha na Sheria

ya Bajeti.

3. Kutokutolewa kwa fedha za miradi ya maendeleo 40%

ya mapato ya ndani

Taarifa ya Mapato na matumizi ya kipindi cha Julai hadi Septemba

2022 inaonyesha kuwa fedha ya maendeleo 40% ya mapato ya

ndani iliyokuwa imetolewa ilikuwa kiasi cha Tsh 259,856,910

badala ya kiasi cha Tsh 481,984,136 iliyopaswa kutolewa kwa

kipindi hicho.

Kiasi cha fedha kilichokuwa kimekutumika ni Tsh. 103,000,000

kwa ajili ya mikopo ya akina mama, vijana na wenye ulemavu kati

ya fedha Tsh 259,856,910 zilizokuwa zimepokelewa huku Tsh.

156,856,910 zikibaki kwenye akaunti ya maendeleo.

Hapa kuna zua maswali mengi bila majibu sababu ya fedha za

miradi ya maendeleo 40% ya mapato ya ndani kukusanywa na

kutokupelekwa kwenye akaunti ya maendeleo ni zipi? Sababu ya

fedha kukusanywa na kuachwa kwenye akaunti badala ya

kupelekwa kutekeleza miradi ya maendeleo ni nini? Kwa miezi 4

sasa miradi inayotekelezwa kutokana na 40% ya mapato ya ndani

haijapelekewa fedha na utekelezaji wa miradi hiyo ni Sifuri.

Sababu za kutokutekeleza miradi ya maendeleo kama baraza

lilivyoidhinisha hazijulikani na hazijawahi kutolewa. Ingawa katika

vikao vya hivi karibuni mkurugenzi amekuja kuwasilisha

mapendekezo ya kubadili matumizi ya fedha za miradi ya

maendeleo kiasi cha zaidi ya Tsh 405,000,000 na kupendekeza

ziende kwenye kuanzisha miradi ya biashara ya ufyatuaji matofali,

shule ya chekechea na ujenzi wa maghala ya chumvi.

Hivyo kwa kipindi cha miezi 4 Mkurugenzi Mtendaji amekaidi

kupeleka fedha za maendeleo katika miradi iliyopitishwa kwenye

bajeti kwa lengo la kufanikisha nia yake ya kubadili matumizi ya

fedha hizo kwa malengo anayoyajua yeye.

4. Upendeleo na mipango mibovu katika ugawaji wa

fedha za maendeleo

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

wamekuwa na tabia ya kuzipendelea baadhi ya kata kuzipa fedha

nyingi za miradi ya maendeleo huku kata zingine zikibaguliwa kwa

kuwa madiwani wa kata hizo hawaendani na mtizamo wa

viongozi hao. Pia kuna upendeleo wa dhahiri wa wajumbe wa

Kamati ya Fedha hapa ipo mifano mingi kama ifuatavyo:-

(i) Kata ya Mwangudo inayoongozwa na Mwenyekiti wa

Halmashauri Mhe. Anthony Philipo Athumani miradi iliyopewa ni

ujenzi wa kituo cha afya Iramba ndogo Tsh 500,000,0000, ujenzi

wa Ofisi ya Kata Mwangudo Tsh 11,000,000, Ukamilishaji wa

Bweni Shule ya Sekondari Makao Tsh 20,000,000, ukamilishaji wa

Bwalo la Chakula Shule ya Sekondari Makao Tsh 30,000,0000,

ukalimishaji wa nyumba ya mtumishi Shule ya Msingi Mbuyuni

50,000,000

(ii) Kata ya Mwasengela inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati

ya Uchumi, Ujenzi, Hifadhi na Mazingira, Mhe. Mlangale Sakumi

Sayi miradi iliyopewa ni Ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasengela Tsh

500,000,000, Ujenzi wa Bweni la Wasichana Lingeka Sekondari

Tsh 73,000,000, ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi

Ng’hanga Tsh 25,000,000, ujenzi wa madarasa mawili Shule ya

Msingi Ng’hanga Tsh 40,000,000, ukamilishaji wa Jengo la OPD

na nyumba ya mtumishi katika Zahanati Mwamhongo Tsh

148,000,000.

(iii) Kata ya Lingeka inayoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya

Fedha, Mhe. Joseph Nyanza Sayi miradi iliyopewa ni ukamilishaji

madarasa 4 na ofisi 2 Tsh 50,000,000, ukamilishaji wa madarasa

2 na ofisi 1 Shule ya Msingi Masanga Tsh 40,000,000, ujenzi wa

maabara Shule ya Sekondari Masalinge Tsh 73,000,000, Ujenzi

wa Sekondari mpya Masalinge (Maalum) Tsh 600,000,000

Na hii haingii akilini katika bajeti Shule mpya ya Sekondari

Masalinge (Lingeka) imepangiwa kiasi cha Tsh 600,000,000 kwa

ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine ikiwemo

maabara lakini wakati huo huo tena inapangiwa kiasi cha Tsh

73,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara. Pia Kata

ya Lingeka imepangiwa kiasi cha Tsh 100,000,000 kwa ajili ya

ujenzi wa OPD na nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya

Masanga.

(iv) Kata ya Mwandoya ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha,

Mhe. Basu Kayungilo imetengewa Tsh 130,000,000 kwa ajili ya

ujenzi wa Wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Mwandoya wakati

Kituo cha Afya cha Mwandoya kina wodi ya Wazazi haya

yanafanywa kukiwa na mahitaji makubwa ya miundombinu ya

afya katika maeneo mbalimbali. hiyo ni mifano michache tu ya

baadhi tu ya kata zilizopendelewa

Baadhi ya Kata zinazobaguliwa na kutokupangiwa miradi

inavyostahili ni Kata ya Kabondo, Kata ya Mbugayabanhya, Kata

ya Mbushi, Kata ya Mwabuzo, Kata ya Mwabusalu, Kata ya

Tindabuligi, Kata ya Mwakisandu, Kata ya Imalaseko, Kata ya

Nghohoboko n.k

Kata ya Mbushi kwenye Bajeti Baraza lilipitisha Tsh 600,000,000

kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata na fedha hizo

zimeondolewa na hazijulikani zilipo.

Kata ya Mbugayabanhya kata hii haina sekondari mpya katika

kupitisha bajeti ya mwaka wa 2022/2023 Baraza la Madiwani

lilipangia Tsh 80,000,000 kwa ajili ya kuanzisha Sekondari mpya

lakini fedha hizo zimeondolewa.

Kata nyingine ni Tindabugili ina magofu mengi na yalikuwa

yamepangiwa fedha katika Bajeti lakini kwa sasa fedha

hazionekani tena. Hii ni mifano michache lakini ziko baadhi ya

kata nyingi zilizobaguliwa kwenye miradi ya maendeleo.

5. Ukiukwaji wa taratibu za uundwaji wa Kamati ya

Fedha, Utawala na Mipango.

Katika kuunda Kamati ya Fedha, utawala na mipango, Mwenyekiti

wa Halmashauri na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya

Meatu wamekiuka Kanuni Namba 40(5) kinachosema Mwenyekiti.

wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango na kuyaleta

ndani ya Baraza la Madiwani na kupitishwa kwa kura na baraza la

madiwani lakini kamati iliyochaguliwa ndani yao wajumbe 6

walipaswa kupigiwa kura na baraza la madiwani lakini mwenyekiti

na mkurugenzi hawakufanya hivyo na kamati hiyo

iliyopendekezwa na mwenyekiti wa halmashauri hadi sasa

inaendelea na vikao na ziara kama kawaida na wanalipwa stahili

zao kama kawaida hapa kuna ukiukwaji mkubwa sana wa kanuni

tajwa hapo juu.

Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri hakuleta orodha ya

wajumbe aliowapendekeza kwenye baraza la halmashauri ili

yapigiwe kura kama kanuni zinavyoelekeza badala yake ameteua

yeye hivyo kukiuka kanuni na kutumia madaraka yake vibaya.

6. Matumuzi mabaya ya fedha za Serikali

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmshauri wamekuwa na desturi

ya kutumia vibaya fedha za Halmshauri bila idhini ya Baraza la

Madiwani kinyume na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa. Ipo

mifano kama ifuatavyo:-

(i) Katika miradi ya UVIKO-19 Mwenyekiti wa Halmshauri na

Mkurugenzi wametumia vibaya fedha za Serikali kwa kuagiza

mabati katika miradi yote bila idhini ya Baraza la Madiwani na bati

moja lilinunuliwa kwa Tsh. 40,000 na wakati huo bei ya juu kwa

bati hizo katika soko ilikuwa ni Tsh 35,000 kwa kila bati la gage

28 maamuzi haya yalikiuka Sheria, Kanuni na miongozo

iliyowekwa.

(ii) Katika ujenzi wa Zahanati 4 za Makomangwa, Mwanyahina,

Sapa na Mwandu Kisesa ambapo kila zahanati ilipewa Tsh Milioni

50 na jumla ya Tsh Milioni 200 zilitumika kwa kukiuka utaratibu

wa Force Account ambapo mikataba ya ujenzi huo ilisainiwa na

Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya badala ya Kamati

za vijiji husika zilizopewa hiyo miradi.

(iii) Katika utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2021/2022 Mwenyekiti

na Mkurugenzi wamekiuka kanuni kwa kuhamisha fedha Tsh

Milioni 25 kutoka Igushilu na fedha Tsh Milioni 25 toka Mwanzugi

ambazo zilikuwa za ukamilishaji wa miundombinu ya Zanahati

katika vijiji hivyo na badala yake fedha hizo zote Tsh Milioni 50

zilipelekwa Kijiji cha Dakama kujenga nyumba ya mtumishi katika

zahanati hiyo ambayo haikuwa katika bajeti.

(iv) Kuanza kutekeleza majukumu na kulipwa posho wajumbe 6

wa Kamati ya Fedha ambao si wajumbe halali wa Kamati ya

Fedha, Utawala na Mipango kwani wajumbe hao hawakupigiwa

kura na Baraza la Madiwani hivyo kutumia vibaya jumla ya Tsh

Milioni 4.8 kwa mchanganuo ufuatao:-

(a) Kikao (i) @ 250,000 x 6 = 1,500,000

(b) Ziara (i) @ 550,000x 6 = 3, 300,000

7. Utoaji holela wa mikopo ya akina mama, vijana na

walemavu

Kumekuwepo na utoaji holela na upendeleo wa mikopo ya akina

mama, vijana na wenye ulemavu kwa vikundi vinavyopata mikopo

katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu hali inayopelekea vikundi

vingi vya uzalishaji mali kukosa mikopo huku vichache vikinufaika

kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa utaratibu wa mikopo ya

aina hii. Baadhi ya mifano katika mwaka wa fedha 2021/2022

mikopo iliyotolewa kwa vikundi ni kama ifuatavyo:-

(i) Kikundi cha vijana cha Heroes Group chenye wanachama

watano kimepewa mkopo wa kununua Min Bus yenye thamani ya

Tsh 72,000,000 huku muda wa kurejesha ni miaka 4

(ii) Kikundi cha akina Mama cha Hapa Kazi Tu chenye wanachama

watano kimepewa mkopo wa Trekta wenye thamani ya Tsh

74,150,000 umri wa mkopo ni miaka 7

(a) Mkopo huu ni mkubwa sana kutolewa kwa kikundi kimoja

kulingana na mapato yanayopatikana kila mwaka katika

halmashauri, wastani wa 4% ya mapato ya ndani kwa mikopo ya

vijana ni Tsh 100,000,000 tu hivyo ukitoa mkopo kwa kikundi

kimoja cha Tsh 72,000,000 umebakiwa na Tsh 28,000,000 tu kwa

vikundi vyote kutoka vijiji vyote vya Wilaya ya Meatu.

(b) Kutolewa kwa mkopo huu kwa kikundi kimoja cha vijana

kutoka Kijiji cha Mwanhuzi Bomani na kikundi kimoja cha

wanawake kutoka Kijiji cha Bukundi kulipelekea vikundi vingi vya

akina mama, vijana na wenye ulemavu kukosa mikopo katika

Wilaya ya Meatu. Vikundi vingi viliomba mkopo lakini

havikufanikiwa kwa maelezo ya upungufu wa fedha, sababu za

kupendelewa vikundi viwili kwa gharama za wana Meatu wote ni

nini?

(c) Gharama ya kununua Min Bus ni Tsh 62,000,000 kwa nini

mkopo umetolewa wa Tsh 72,000,000? Imekuwa ikohojiwa

kwenye vikao mbalimbali vya halmashauri lakini hakuna majibu

ya uhakika yanayotolewa.

(d) Sababu ya vikundi hivi kujipatia Mikopo ya Min Bus na

Matreka kupitia mikopo ya akina mama, vijana na wenye ulemavu

ilikuwa ni nini kwani mikopo ya aina hiyo ingewezwa kuombwa

kupitia Taasisi za Fedha badala ya kupitia halmashauri ambazo ni

fedha kidogo kwa ajili ya wananchi wanyonge.

(e) Tathimini ya utoaji wa mikopo hiyo inaleta mashaka makubwa

kama vikundi hivyo vitaweza kurejesha mikopo hiyo kwani uimara

na muda wa uchakavu kwa mashine na mitambo ni wastani wa

miaka 3 mpaka miaka 5 hayo marejesho ya miaka 7

yatarejeshwaje wakati mitambo itakuwa haipo.

(f) Hakuna uthibitisho wa tathmini ya kitaalamu uliyofanywa

kujiridhisha uwezo wa vikundi hivyo kurejesha mkopo kwa muda

uliowekwa. Hakuna maoteo ya taarifa za fedha yanayothibitisha

vikundi hivyo kumudu kurejesha mkopo huo. Kushindwa kufanya

marejesho kwa vikundi hivyo kutaleta hasara kubwa kwa

Halmashauri na Serikali kwa ujumla lakini pia itazorotesha zoezi la

utoaji wa mikopo kwa wananchi.

Haya mambo yote yamefanywa na Divisheni ya Maendeleo ya

Jamii kwa kibali na Baraka za Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti

wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

3.0 HITIMISHO

Halmashauri ya Wilaya ya Meatu inaendeshwa kwa ukiukwaji

mkubwa wa Sheria, Kanuni na Taratibu na matumuzi mabaya ya

madaraka hali inayopelekea upotevu mkubwa wa fedha za umma

na hasara kubwa kwa taifa.

Kuchelewa na Kukwama kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo

kunachelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi, udhaifu huu

unathibitisha kuwa kwa kiwango kikubwa Mwenyekiti na

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

wamepwaya na wameshindwa kumudu majukumu yao.

Lakini pia kutokana na udhaifu huu mkubwa wa usimamizi na

uendeshaji CAG afanye ukaguzi maalum kwa Halmashauri ya

Wilaya ya Meatu.

Mwisho.

ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WANAOUNGA

MKONO HOJA HII:-
  • Seni Sitta - Diwani Kata ya Itinje - Simu Na. 0621 139 000​
  • Daudi M. Sollo – Diwani Kata ya Mwakisandu – Simu Na. 0621 944 915​
  • Masumbuko Pesa – Diwani Kata ya Mbugayabanhya – Simu Na. 0712 342 564.​
  • Charles Lunjini – Diwani Kata ya Mwabuzo – Simu Na. 0785 542 427.​
  • Tabu Magembe – Diwani Kata ya Tindabuligi – Simu Na. 0626 131 569.​



 
Walivyomuangukia hawakumuumiza,kanchi haka bure KABISA.
 
Back
Top Bottom