Nassari Agawa CD Kwenye Mkutano wa Kampeni

Nassari Agawa CD Kwenye Mkutano wa Kampeni

Umeona payroll za November mkuu? Kuna chochote kimeongezeka huko upande wenu?
Maisha bora haya jengwi kwa mshahara mkubwa?? vinginevyo uniambie ni kanuni ipi ya kiuchumi inasema hivyo ''ni kuulize swali'' Kiasi gani cha mshahara wakilipwa watumishi kitawatosha??? na ni lini watumishi wangelipwa wewe ungelizika??
 
View attachment 633640

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemnadi kitofauti mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa.

Nassari aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani hapa huku akiwataka wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa kudai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Nassari amefafanua kwamba pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo, Nassari amesema kwamba wakati hao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa,” alisema Nassari.
Yaani badala ya kuongea sera za kwa nini achaguliwe yeye anazambaza cd??
 
Uhitaji huu wa mkate kasababisha nani kama sio ccm ??? Alafu leo unakebehi kama alivyozoea magufuli kutukebehi na kauli zake chafu,ndicho alichowatumeni nanyi mtufanyie !! Lolote baya,ovu,chafu lililo wakuta na linaloendelea kuwakuta wananchi limesababishwa na utawala wa ccm.miaka yote kuwa madarakani kwa kujinufaisha wao na sio kunufaisha wananchi !! Hapo kosa la Nasari ni lipi kama sio unawaza kinyume cha maumbile yako ?? ccm ni janga sio siri,na hakuna mnapofaa wala kupendwa,licha ya kutokubalika ! Ni wasiojulikana tu ndo wanawawekeni madarakani.
Kwa hiyo utatuzi wa hayo mabaya ya CCM ni kuwagawia wananchi CD bila deki?
 
Maisha bora haya jengwi kwa mshahara mkubwa?? vinginevyo uniambie ni kanuni ipi ya kiuchumi inasema hivyo ''ni kuulize swali'' Kiasi gani cha mshahara wakilipwa watumishi kitawatosha??? na ni lini watumishi wangelipwa wewe ungelizika??
Ishu sio mishahara mikubwa au midogo. Ishu inakuwaje mtanzania namba moja anaahidi kitu kwa mbwembwe wakati anajua kabisa uchumi umeyumba hataweza kutekeleza? Alitegemea angepata wapi hela za kuongeza mishahara?

Kwanini asiwe mkweli tu ikajulikana moja?

By the way maisha bora hujengwa na mishahara mikubwa na maisha ya dhiki, chuki na uovu hujengwa na mishahara midogo kama ulikuwa hujui
 
Hizi akili mkaa? CD 500 ni pesa nyingi kwanini asifanye jambo la maendeleo ili wananchi wawachague Chedema kwa mazuri yao? Akili zingine bhana haya TUTACHAGUA CCM hadi mtakapo badilika.
Duuuu
 
Hizi akili mkaa? CD 500 ni pesa nyingi kwanini asifanye jambo la maendeleo ili wananchi wawachague Chedema kwa mazuri yao? Akili zingine bhana haya TUTACHAGUA CCM hadi mtakapo badilika.
Mazuzu kama wewe idadi yenu inazidi kupungua sishangai ukijinadi hadharani kama unavyofanya lkn kwa hakika mmebaki wachache mno. angalia mikutano ya kampeni ya chama mpaka mpakie watu kwa nagari kutoka vijiji jirani hiyo ni ishara kuwa mmechokwa sana kama sio polisi na tume mlishashindwa miaka kadhaa iliyopita
 
Halafu anakuja kututangazia kabisa
Alafu mi nikajua cd yenye nondo za sera zao, kumbe upuuzi!
Rasta wa zamani aka mvuta bangi nae yuko bize kusambaza sera za ETI yuko tayari kuuza figo badala ya kuwaambia wananchi watafanya nini ili kuwashawishi wawachague.
Hovyo sana hawa watu, naona anguko lao kubwa sana maana wananchi hawataki ujinga ujinga.
 
Ni Tanzania pekee panapo patikana siasa za kipumbavu na kirofa.



#nakwenda_zimbabwe
 
Back
Top Bottom