Nassari Agawa CD Kwenye Mkutano wa Kampeni

Nassari Agawa CD Kwenye Mkutano wa Kampeni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
nasari.jpg

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemnadi kitofauti mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa.

Nassari aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani hapa huku akiwataka wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa kudai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Nassari amefafanua kwamba pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo, Nassari amesema kwamba wakati hao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa,” alisema Nassari.
 
sasa kama chama kimeishiwa hakiwajali madiwani, madiwani wamegeuka kuwa bidhaa, ni hatari sana. SWALI KWA NASARI '' je kwa madiwani hawa wapya anao wanadi atawasaidia vipi ili wasirubuniwe??? kwa nini tusichague wale sasio rubunika kirahisi rahisi, kwa kuwa madiwani wa CHADEMA wana njaaa, tuchague wasio na njaaa
 
Hizi akili mkaa? CD 500 ni pesa nyingi kwanini asifanye jambo la maendeleo ili wananchi wawachague Chedema kwa mazuri yao? Akili zingine bhana haya TUTACHAGUA CCM hadi mtakapo badilika.
walionunu madiwani kwa pesa za umaa na kutumia mamilioni kurudia uchaguzi na kupandishwa vyeo hiyo ndio akili?
 
sasa kama chama kimeishiwa hakiwajali madiwani, madiwani wamegeuka kuwa bidhaa, ni hatari sana. SWALI KWA NASARI '' je kwa madiwani hawa wapya anao wanadi atawasaidia vipi ili wasirubuniwe??? kwa nini tusichague wale sasio rubunika kirahisi rahisi, kwa kuwa madiwani wa CHADEMA wana njaaa, tuchague wasio na njaaa
Jaribuni tena kuwarubuni ndio mtajua chadema imelala au inajua inachofanya
 
Back
Top Bottom