Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka!

STORY YA BABU DC HII HAPA JUU YA KISA HIKI


Ndugu wadau wa jukwaa letu tukufu,

Kama mtakumbuka, week iliyopita nilirusha thread iliyokuwa inaripoti kisa cha Nasra Mohamedi wa Bunda aliyegongwa kwa gari na mume wake na kuburuzwa kama mita 100 hivi. Story yenyewe hii hapa:

Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka!


Hivi karibuni, nimepata bahati ya kuongea na mtu ambaye alikuwa maeneo yale ya tukio ingawa hakushuhudia live jinsi tukio livyotokea. Hata hivyo ameweza kunipatia story za ndani kuhusu mkasa wenyewe.

Inasemekana kuwa Nasra na mume wake walikuwa na ndoa nzuri sana. Ilikuwa ni couple ya kupigiwa mfano. Hata hivyo, mume wa Nasra alipitiwa na shetani akatembea nje ya ndoa; na kwa bahati mbaya Nasra alimfumania. Baada ya tukio hilo, ndoa yao haikuwa na amani tena; na Nasra aliamua kutafuta mwanamume wa nje na kutembea naye wazi wazi. Hatimaye walitengana ila Nasra aliendelea kumfuata fuata mume wake kwa kumuonyesa wazi wazi kwamba anatembea na huyo bwana wake mpya. Inasemekana mume wake ni mpole sana na alijitahidi kumpuuza. Hata hivyo vituko vilizidi kiasi kwamba mume alikuwa anafuatwa hata kwenye baa anakoenda. Na mara zote, Nasra alikuwa akifika na huyo bwana mpya. Na kwamba, alifikia mahali pa kukaa meza ambayo iko karibu na mume wake ili amkere. Pia alianza kufanya vituko ili mume wake wa zamani amfumanie, ili naye aumie kama ilivyotokea kwake!

Inasemekana pia kwamba Nasra alifungua kesi mahakamani kuomba talaka na kwamba wagawane mali za ndoa. Taarifa zinasema kwamba, kabla ya kutengana, mume alikuwa amemnunulia Nasra gari. Pia wakati wanatengana, mwanamke aliondoka na pesa za mume kiasi cha shilingi 10mil. Haya yalizidisha uchungu kwa mume ambaye alianza kuwaambia marafiki zake kwamba atamuua huyo mke kisha naye ajiue.

Siku ya tukio, inasemekana Nasra alimkuta mume wake standi ya bus Bunda na kuanza kumtukana matusi machafu sana, tena mbele ya watu wengi waliokuwepo hapo. Baadhi ya mambo aliyomkashifu ni kwamba mume huyo hana nguvu za kiume za kutosha na pia kuwa watoto waliozaa si wake! Inasemekana yule baba aliondoka kwa muda ili kuepuka shari za mke wake. IHata aliporudi tena baada ya muda kidogo, bado Nasra aliendelea kumtukana. Ndipo mwanamume akamuita apite upande wa pili wa gari ili waongee (wakati wote huo, yule baba alikuwa kwenye gari), na hapo hapo mwanamume aliondoa gari na kumburuza hadi karibia na kituo cha polisi. Alipofika hapo, akamtelekeza pomoja na gari na kupotelea kusikojulikana.

Kwa ufupi, huo ndio upande mwingine wa hili tukio ambalo kweli linasikitisha sana,


Babu DC!!
 
kipindi cha nyuma nilikuwa sijawahi kuishi karibu na hawa jamaa wa Mara, nilipo sasa kuna jamaa tunaishi naye nimeapa kabisa siwezi kumshauri au kumuruhusu dada au mtu wa karibu aolewe na hawa jamaa yani kwao mwanamke hawamweshimu kabisa jamaa anampiga mke wake mbele ya watoto na wapangaji,,, aibu tupu.

i always see them like animals!
 
hayo maumivu sio ya kawaida aise aliyokuwa anapata huyo mama
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema
Na huyo mwanaume ni katili kiasi gani aise unajua kabisa umemgonga mtu na then bado unaendelea kudrive mita mia na hamsini kwenye lami aise
So sad

Halo Mr Rocky. Ogopa kitu kinaitwa pesa. Kama kwa bahati mbaya akili yako ikiwa nyepesi halafu ukamiliki pesa, waweza pata kichaa cha pesa. Ndivyo navyomwona huyu bwana. Kiburi chake ni hela mingi! Huyo mwanamke wakati anaburuzwa lazima alikuwa anapiga makelele mengi ya kuomba msaada na huruma toka kwa mumewe lakini pesa zilimgeuza huyo bwana kuwa simba wa porini! Kiburi hiki nakionaga sana kwa baadhi ya wanaume wanaomiliki utajiri mkubwa. Hawana mahusiano mema na wake au watoto wao! Niliona kwa macho yangu msichana mmoja alichumbiwa na tajiri. Baba wa msichana akamkataza bintiye kuolewa na huyo bwana ila msichana aling'ang'ania kuolewa. Akaolewa ila baada ya mwaka mmoja, akiwa na katoto ka miezi minne, msichana alipigwa sana na mumewe mpaka akapofuka kwa kipigo! Huyo bwana wala hakuangaika kumpeleka mkewe hospitali ila alioa mwingine! Kelele za ndugu wa aliyekula kipigo mpaka akapofuka hazikufika popote. Huyo bwana anadunda mpaka leo na mke mpya! Fedha hiyo aisee!
 
Last edited by a moderator:
tobaaa yailahi...lakini hadi afikie uamuzi huyo lazima huyo bwana awe ameumizwa sana na kuamua kufanya kisasi!!!!
Lakini kisasi gani hiki?!?!? Lakini watu wengine wakatili tuuu jamaniiii

Nna sharomeni wa kutoka huko Mara ananipigia mahesabu ya ndoa .........wacha nifikirie mara mbili mbili yasijenikuta mie!!!:israel:
 
Huyu mwanaume hastahili kuhurumiwa ila kutokana na story yenyewe wakati mwingine sisi wanawake tunachezea kichapo...au wanasema kuuliza makofi polisi.

Mtu yeyote akiwa provoked anaweza kupoteza hali ya ubinadamu...tuchunge sana midomo na matendo yetu ili kujiepusha na unyama kama huu.
 
Kuna jirani yetu nikiwa mdogo alikuwa akimpiga mkewe anamvua nguo zote afu anamtoa nje...imagine mama mwenye watoto wakubwa anatolewa nje uchi wa mnyama..na si mara moja wala mbili ndio life style yao.

Sijuhi ni nini asili ya ukatili huu.

Hata wazazi wangu walinambia NK ukiolewa na hao watu tutakupa zawadi ya sanda. Tumeishi nao sana tunawafahamu vizuri. Kupiga kuko damuni..wanapiga hata watoto wao kwa mikanda ya jeshi.

mi hata mabinti wangu nimewaambia kuliko kuolewa na watu wa MARA HERI WAISHI NA MBWA KAMA WAZUNGU!! I AM SORRY KAMA NI nimekukwaza
 
Hivi Paloma kwa akili yenye akili nzuri, mtu anaweza fanya unyama huu kama si mwehu, kichaa, taahira ya ubongo,wendawazimu na kupagawa juu yake?....Hata kama NINGEMFUMANIA MKE WANGU siwezi fanya hivi, ni bora tuachane kwa amani.
 
ukatili uliofanywa kwa huyu mwanamke hauvumiliki kwa sababu zozote zile; but then kama ni kweli kwamba marehemu naye alianza tabia ya kumfuata fuata na kumtukana mwenzake, naye pia hakutenda sawa
 
Its sad watu waliowahi kupendana wanapogeuka maadui na kudhurihiana

Roho yake ipumzike kwa amani baada ya miezi sita ya maumivu makali
 
MUNGU AILAZE ROHO YA HUYU MAMA MAHALI PEMA PEPONI,
cha pili inawezekana vipi mtu akutukane stand ya mabasi na kujaza umati halafu umuite pembeni muongee eti hebu zunguka upande huu tuongee (hivi mnajua maana ya TEMPER ? ) BADO sikubaliani na story hii nitakachoomba hiyo picha ya huyo jamaa tuisambaze kwenye fb na yahoo atakamatwa tu, ila naye alichemka, kwa huyo Mama (samahani Nasra) ilikuwa sio saizi yake mbona angeingia tu mitaani kujipoza na hasira? (MMENISAMEHE?)
 
tobaaa yailahi...lakini hadi afikie uamuzi huyo lazima huyo bwana awe ameumizwa sana na kuamua kufanya kisasi!!!!
Lakini kisasi gani hiki?!?!? Lakini watu wengine wakatili tuuu jamaniiii

Nna sharomeni wa kutoka huko Mara ananipigia mahesabu ya ndoa .........wacha nifikirie mara mbili mbili yasijenikuta mie!!!
:israel:

sio wote Paloma, mbona mimi ni wa MARA but don't have those things, olewa tu na jamaa kama yupo siriaz, usimnyime mke jamaa kisa samaki mmoja akioza wameoza wote,
 
Last edited by a moderator:
mi hata mabinti wangu nimewaambia kuliko kuolewa na watu wa MARA HERI WAISHI NA MBWA KAMA WAZUNGU!! I AM SORRY KAMA NI nimekukwaza

you are not serious! yaani unasema ni boRa binti yako aolewe na mbwa kuliko na mtu wa MARA???!!!
 
Back
Top Bottom