Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,599
TBC1 wamerusha habari kuhusu tukio la ajabu sana, ambalo linahusisha ukatili wa hali ya juu. Nasra Mohamedi mkazi wa Bunda, Mara amelazwa hospitali ya Bugando baada ya mume wake kumfanyia vitendo vya ukatili wa kutisha. Huyo mama amesimulia kuwa mume wake alimgonga na gari na kisha akamburuza kwa mita kama 100 hivi. Amevunjika mbavu 7, mguu na ana vidonda vya kutisha sehemu mbali mbali za mwili. Pia sikio lake moja limekatika. Nasra amekaa ICU kwa siku 21 na sasa anaendelea vizuri. Hata hivyo, bado mume wake anamtumia vitisho kwamba lazima ammalize.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto; Sophia Simba amemtembelea Nasra hospitali na kuomba polisi wamwongezee ulinzi. Amesema kuwa pamoja na kwamba mume wake Nasra ametoroka na haijulikani yuko wapi. Hata hivyo, polisi wataendelea kumsaka hadi wamkamate.

Nimesikitika sana kwa kitendo alichofanyiwa huyu mama!

Babu DC!
 
Mura tata, baba Ghati hana mcheso.

So sad, nimeiona hiyo taarifa. Bora hizi taarifa zianze kuibuliwa maana akina mura wanachosha wanavyowafanyia wanawake kwa kweli.

Siku moja ntasimulia kisa cha jirani yangu wa kikurya, lol they are heartless sometimes.
 
Ninahitaji dakika moja tu na huyo jamaa. Dakika moja tu itanitosha.

Unajua Kaka, sijaamini na sitaki kuamini kwamba mtu unaweza kumfanyia binadamu mwenzike (acha mke) unyama kiasi hicho...!!

Bahati mbaya TBC1 hawakueleza sababu ambazo zimemfanya huyo bwana afikie hapo..Ila hata kama wangezitaja, hakuna kitu kinaweza kuhalalisha unyama wa namna hiyo!!

Babu DC!!
 
Hakuna kabisa kitu kinachoweza kuhalalisha unyama uliopitiliza kama huo.
 
unaweza kuta alichelewesha chakula au aliwaacha ng'ombe wakala shambani kwa watu.

Kwani wana sababu za maana basi?

Unajua Kaka, sijaamini na sitaki kuamini kwamba mtu unaweza kumfanyia binadamu mwenzike (acha mke) unyama kiasi hicho...!!

Bahati mbaya TBC1 hawakueleza sababu ambazo zimemfanya huyo bwana afikie hapo..Ila hata kama wangezitaja, hakuna kitu kinaweza kuhalalisha unyama wa namna hiyo!!

Babu DC!!
 
Kitu mura mbuya saguru ghati! haya kina mwita chacha,wankuru,ni mambo gani haya mnafanya?
 
halafu anaendelea kutoa vitisho...! atambue tu kuwa malipo ni hapahapa chini ya jua,
 
Tabu mtu kuoa hajui mana ya mke na thamani ya mke.

Wako wengi wanamna hio, inabidi tuwaombe kwa mungu usiku na mchana wajue nini thamani ya mke.

Mtu kama ana mheshimu mama yake, lazima atamheshimu tu mke wake, huyo jamaa kuna dalili kubwa sana hata mama yake mzazi alikuwa hamheshimu.
 
jamani jamani jamani!!! Eti huyo mtu nae atatafuta wakili wa kumtetea....dah!!!

kama mimi ndio wakili mwenyewe namshindilia kisheria mpaka asipatikane na hata nafasi ya kuhurumiwa kidogo! Nyambaaaf. Kwa maudhi gani alofanyiwa hata atake kumtoa roho mwana wa mwenzie?
 
Duh huyo Dada amepona kumbe...

Ah Mungu wake mkubwa, hii stori niliiona mda kidogo Channel 10...

Mambo ya nyumba ndogo haya, unapewa mambo hadi familia yako unaiona haina thamani kabisa
 
kama mimi ndio wakili mwenyewe namshindilia kisheria mpaka asipatikane na hata nafasi ya kuhurumiwa kidogo! Nyambaaaf. Kwa maudhi gani alofanyiwa hata atake kumtoa roho mwana wa mwenzie?

Ningekuwa ndio hakimu; hata kama nina hadhi ya Jaji...haki ya nani ninge-force uhamisho na kwenda huko ili ninunue kesi!! Ile huyo mume kukimbia tu, ninge-conclude kwamba kweli alimgonga makusudi na hakuna cha ushahidi wala cha kuendesha kesi......siku hiyo hiyo hiyo nasoma kesi na hapo hapo hukumu.
 
kama alicheat namuunga mkono msela kwa maamuzi yake but otherwise tat is too harsh a punishment
 
kama alicheat namuunga mkono msela kwa maamuzi yake but otherwise tat is too harsh a punishment

Ni wivu wa kijinga tu. Inasemekana hawa wawili walikuwa wameshatengana muda mrefu. Kwa hiyo hakuna swala la cheating hapo. Kila mmojawao alikuwa huru na mambo yake.
 
Back
Top Bottom